bahati mbaya
JF-Expert Member
- Oct 23, 2012
- 578
- 193
Pole sana maana tumepoteza ndugu na jamaa zetu kwa ugonjwa huo.
Wewe punguani, hata ujumbe mushrik hasamehewi na Qur'an imeshasema hilo, kaisome vizuri.
Kwanza yakupasa uelewe kwamba ukimwi si ugonjwa,ukimwi ulikuwapo tangu enzi za Nuhu,Yesu Kristo na mtume Muhammad,ukimwi hauui bali kinachoua ni ugonjwa fulani unaoingia mwilini baada ya kinga ya mtu kushuka(mfano TB,Malaria nk),ukimwi hausababishwi na HIV kama ulivyodanganywa hapo zamani.Ukimwi ni suala la zamani sana lakini sasa werevu wenye uroho wa pesa wameupachika ukimwi jina jipya na kanuni mpya kwa lengo la kuuza ARVs na madawa yanayoendana nayo.Miaka hiyo wengi hatukuwa na "uelewa" juu ya mambo ya UKIMWI,dalili zake ......
Kwa sasa hakuna asiyejua kwamba hizo dalili ulizotaja hapo juu ni dalili za TB,exactly ilikuwa ni TB na pia hakuna ubishi kwamba alimwambukiza na mtoto wake pia hiyo TB.Hivyo basi alikuwa na maambukizi ya TB na si maambukizi ya ukimwi.Kwani wewe hujui kwamba ukimwi hauambukizwi?Homa za hapa na pale na kikohozi cha muda mrefu kilimsumbua dada.Alikuwa tayari na mtoto mmoja ambaye naye bahati mbaya alizaliwa akiwa na maambukizi......
Hata baada ya kukatwa na kunyweshwa maji ya pango la mti,dada aliendelea kukohoa sana sana.Akodhoofika na kukonda mno.Dada aliteseka,alikonda na kuisha sana.Ilifikia wakati nami nikimtazama ninatoa machozi.Ama hakika UKIMWI na mateso yake ya wakati huo ya bila ARV yasikie tu kwa jirani.
Hata anakufa hakuna aliyejua ulikuwa ni UKIMWI,wengi walilaani juu ya "uchawi" na jini lililotupiwa familia.Na ama hakika Waganga walisisitiza kuwa "jini" hilo bado linazungukazunguka..Litaondoka na mwingine.......
hadi kufikia jioni majipu yakawa ni TB kwa wote wawili,......
ikabidi ni mtoto wa dada aende kupimwa,naye tukamsafirisha mpaka mjini.Tobaaaa!Mtoto akakutwa na UKIMWI alioachiwa na mama yake,hivyo Mama na Dada waliambukizwa TB sababu hawakuwa na tahadhari ya kumuhudumia marehemu....
Kumbe haikuwa jini kama wale waganga walivyosema,ulikuwa ni UKIMWI kwa marehemu na kwa mama na fada ilikuwa ni TB............Mwisho wa siku wote tukapona,haikuwa jini kwa dada wala kwa Mama,bali ni UKIMWI na TB.....
Isingalikuwa mtumishi yule wa Mungu,basi "ujinga" wa kuamini jini ungeendelea.....
Kwa hiyo mkuu Deception hakuna kitu kinaitwa UKIMWI??Na hakuna watu wanaokufa kwa UKIMWI??sasa hao tunaoambiwa wamekufa kwa ukimwi ni uwongo?Kwanza yakupasa uelewe kwamba ukimwi si ugonjwa,ukimwi ulikuwapo tangu enzi za Nuhu,Yesu Kristo na mtume Muhammad,ukimwi hauui bali kinachoua ni ugonjwa fulani unaoingia mwilini baada ya kinga ya mtu kushuka(mfano TB,Malaria nk),ukimwi hausababishwi na HIV kama ulivyodanganywa hapo zamani.Ukimwi ni suala la zamani sana lakini sasa werevu wenye uroho wa pesa wameupachika ukimwi jina jipya na kanuni mpya kwa lengo la kuuza ARVs na madawa yanayoendana nayo.
Kwa sasa hakuna asiyejua kwamba hizo dalili ulizotaja hapo juu ni dalili za TB,exactly ilikuwa ni TB na pia hakuna ubishi kwamba alimwambukiza na mtoto wake pia hiyo TB.Hivyo basi alikuwa na maambukizi ya TB na si maambukizi ya ukimwi.Kwani wewe hujui kwamba ukimwi hauambukizwi?
Narudia,kukohoa na kukonda sana ni dalili ya wazi kabisa ya TB,pia ulisema kuwa alikuwa na homa za mara kwa mara,hii hakika ilikuwa ni TB.Sasa kwa kuwa tumewaamini sana wazungu,hivyo hatuwezi kujiuliza kwamba TB ilikuwapo tangu zamani,ila sasa hivi iepewa jina jipya kama itaambata na kijidudu HEWA kiitwacho HIV.Ukiwa na HIV(hewa) basi magonjwa yako HALISI hayatapewa kipaumbele na hata ukifariki watu watasema umekufa kwa HIV/UKIMWI.Hakika ujinga ni kitu kibaya sana.
Narudia,haukuwa ukimwi,ilikuwa ni TB,ukimwi hauui na haudhoofishi,TB ndio imemdhoofisha na kumwua,TB inatibika.Pia fahamu kwamba huwezi kupata TB mpaka kinga yako ishuke(yaani uwe na upungufu wa kinga mwilini/UKIMWI).Hivyo basi,watu wote wenye TB wana UKIMWI bila kujali kama wamepimwa HIV+ au HIV-,umeelewa?Ukitibu TB waliyonayo kwa usahihi lazima wapone na kuendelea na maisha.Ujinga pia ndio huwapa waganga wa kienyeji(wa matunguli) sifa zisizo za msingi,kwa kuwa TB inaambukizwa,hivyo wengine katika familia wakiugua mtaanza kusema kwamba "mganga alituambia kuwa ni jini" bila kujua kama TB ndio jini lenyewe.
Exactly,nilijua kwamba ni TB,na wote hawa wawili ndio walimuuguza dada yako,hivyo wliambukizwa TB kutoka kwa dada yako,very straightforward,dada alikufa kwa TB,na kama angetibiwa hiyo TB angepona kama walivyopona mama yako,lakini kwa kuwa kipindi hiko ujinga ulikuwa mwingi na tulileweshwa na hadithi za wazungu wenye uchu wa fedha,basi kwenye bongo zetu neno UKIMWI ndilo lililotawala kumbe adui wetu halisi hakuwa ukimwi.
Unaona tatizo la kukosa uelewa?Yaani mama na dada yako wameambukizwa TB lakini mtoto kaambukizwa ukimwi.Kwa ugonjwa unachagua nani wa kumwambukiza nini.Narudia,mtoto pia kafa kwa TB,na kama angetibiwa TB angepona,lakini kwa kuwa mlishaleweshwa na neno UKIMWI,basi hamkuwa na la kufanya kwa kuwa mliambiwa kwamba ukimwi hauna tiba.
Unaona unavyochanganya mambo?Narudia,ukimwi hauui na ukimwi si ugonjwa,ukimwi hauambukizwi kwa njia yoyote ile.Kama huamini muulize daktari yeyote yule.Narudia,dada yako kafa kwa TB.Kama angepata tiba ya TB mapema na kwa usahihi lazima angepona kama ninyi mlivyopona.
Unajua UJINGA ni hatua tu ya uelewa,unaweza ukatoka kwenye ujinga wa hatua fulani lakini ukahamia kwenye ujinga wa hatua nyingine katika jambo hilohilo.Wewe sasa hivi huamini jini lakini unaamini UKIMWI au VVU.Ni kwamba umetoka kwenye ujinga mmoja na kuhamia kwenye ujinga mwingine.Ili ujinga ukutoke kabisa kwenye suala hili inabidi usome sana na kudadisi/kutafiti ili ujue kwamba Ukimwi sio tishio,ulikuwapo tangu zamani,ila tofauti ya sasa ni kwamba umedanganywa kwamba unasababishwa na mdudu ambaye hajawahi kuonekana na daktari yoyote duniani aitwaye HIV.
Ukifuata ushauri wangu utakuja kugundua kwamba HIV/AIDS ni upuuzi mtupu na kwamba watu hufa kwa magonjwa yaleyale ya zamani bila kujali kama wana huyo HIV(feki) au hawana.
1.Ugonjwa gani unachagua nani wa kumwambukiza hata kama wote wako kwenye level sawa za risk ya kupata?
2.Tumeambiwa huambukizwa kwa njia ya ngono zembe,lakini kuna familia nyingi utakuta mume au mke ana HIV lakini mwenzake hana na wamezaa watoto na watoto pia hawana,ugonjwa gani wa kipumbavu huu?
3.Tumeambiwa kwamba bila ARVs lazima ufe mapema,lakini hadi sasa kuna rundo la watu wameambiwa wana HIV na hawatumii ARVs kwa zaidi ya miaka 20,Je,unataka kuishi miaka mingapi hapa duniani kama unaweza kuishi na mdudu huyu feki kwa zaidi ya miaka 20 bila kutumia ARVs?
4.HIV hajawahi kuonekana hata kwa kutumia electron microscope,hata wale wanaosema kwamba wamemgundua HIV hawajawahi kumuona na wanakiri kwamba hawajawahi kumuona,sasa picha yake wamepata wapi?,wamejuaje kwamba yeye ndiye sababu ya ukimwi?
5.Tumeambiwa vipimo vinapima HIV,lakini ukweli ni kwamba vinapima kinga ya mwili na sio HIV,Je,wangapi wanajua upumbavu huu?Leo hii ukiambiwa wewe ni HIV+ kwa vipimo hivi uta panic na kufa hata kabla ya kunywa sumu zao(yaani ARVs).
6.Wangapi wanajua madhara ya ARVs humu?Kama kuna mtu hajui basi atafute mitandaoni au vitabuni.Kwa urahisi zaidi chukua kikopo cha ARVs na ndani yake utaona karatasi ya maelekezo,soma karatasi hiyo kwa makini sana na utagundua kwamba side effect zilizotajwa humo ndizo zinazoua watu na si HIV(hewa) kama anavyosingiziwa.
Watu huwa hawasomi karatasi hizo kutokana na rundo la maneno yaliyomo,lakini nina uhakika kama wangesoma na kuzielewa basi wasingekubali kula ARVs katika maisha yao na woga huo ndio ungewaokoa.
-ARVs husababisha cancer
-ARVs husababisha kisukari
-ARVs husababisha presha/matatizo ya moyo
-ARVs husababisha upungufu wa damu
-ARVs husababisha matatizo ya figo
-ARVs husababisha matatizo ya Ini.
Matatizo yote haya anasingiziwa HIV(hewa).
Ama kweli "watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa".
Ukishirikisha HIV na mambo ya kimungu/dini basi ujue umeshaumia na si rahisi ukaja kuelewa ukweli huu uliojificha.Hawa jamaa wamepenye dhana hii ya HIV katika taasisi za dini kwa makusudi wakiwa na lengo la kukusanya wateja wengi zaidi na wakudumu wa ARVs.
Mwenye masikio na asikie.
Juu huko msiba mkubwa ulikutokea 1993 kati hapo 1994.
Halafu umemaliza form 4 unangoja majibu ya kwenda form 6.
Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?
Pole sana......Hili jambo limkute jirani yako tu,likiikumba familia ni majonzi na mtihani mkubwa sana.Hatukuwa tumewahi kufiwa na mmoja wa wanafamilia,kwa maana ya kaka au dada wa tumbo moja na baba mmoja.Misiba mingi ilikuwa ni kwa ndugu na jamaa tu wa karibu.Msiba huu wa dada yetu aliyekuwa "kichwa" na msaada mkubwa kwa familia ulitokea mwezi March 1993 wakati huo mimi nikiwa nimemaliza kidato cha nne nikisubiri matokeo ya kwenda kidato cha sita.
Huyu dada aliugua kwa muda mrefu sana na hata mimi nilipokuwa narudi likizo kijijini kwetu baada ya kufunga shule nilikuwa namkuta anazidi kudhoofika.Miaka hiyo wengi hatukuwa na "uelewa" juu ya mambo ya UKIMWI,dalili zake na hata "uzoefu" wa kuuguza mgonjwa huyu.Homa za hapa na pale na kikohozi cha muda mrefu kilimsumbua dada.Alikuwa tayari na mtoto mmoja ambaye naye bahati mbaya alizaliwa akiwa na maambukizi.
Hivyo baada ya dada kufariki huyu mjomba wangu alidumu kwa miaka miwili naye tukazika.A young talented boy!Alitumia mkono wa kushoto kuandika na kucheza mpira.Ama hakika UKIMWI umeenda na wapendwa wetu wengi na umekatiza ndoto za watu wengi. Kwa maisha ya kijijini na elimu duni ya afya na huduma mbovu ya afya kijijini,dada aliishua kupewa dawa za yale magonjwa nyemerezi tu lakini haikufua dafu.
Maana Kituo cha afya kilichokuwepo hakikuwa na vipimo.Ilikuwa ni kituo kilichojengwa kwa msaada wa Masista wa kanisa katoliki.Ambao zaidi ya kujitolea kwao sbb ya "usista" wao na nadhili zao za kutumikia jamii inayowazunguka,hawakuwa na elimu darasa ya mambo ya tiba.Kama ada ya maisha ya wengi vijijini wazo kubwa lilikuwa ni dada kurogwa.Haikuingia akilini mtu kuugua kiasi kile bila kupata nafuu na kudhoofu.
Sababu ya kukohoa sana,shangazi alitoa wazo kuwa inabidi dada akatwe "kilimilimi" maana mabibi pale bush wanasema hicho ndio kitakuwa kinamsababisha akohoe sana,na baada ya kukatwa ili kidonda kile kipone haraka alitakiwa kunyweshwa maji yaliyopatikana kwenye pango la mti na hasa mbuyu.Siku kadhaa akaja bibi wa pale kijijini ambaye ni mtaalamu wa kukata vilimi.Dada,siku moja alfajiri na wembe mpya wa topaz alikatwa kilimilimi,maana ilisemwa ni lazima kikatwe kabla ya jua kuchomoza.
Hata baada ya kukatwa na kunyweshwa maji ya pango la mti,dada aliendelea kukohoa sana sana.Akodhoofika na kukonda mno.Tukiwa wenye imani ya dini ya Katoliki kila jioni nilipokuwa likizo ya kidato cha nne dada aliniita na kusali nae rozari ili Mungu ampe afya njema.Hata kwa elimu yangu ya kidato cha nne nami sikuwa najuwa kuwa ule utakuwa ni UKOSEFU WA KINGA MWILINI.Dada aliteseka,alikonda na kuisha sana.Ilifikia wakati nami nikimtazama ninatoa machozi.Ama hakika UKIMWI na mateso yake ya wakati huo ya bila ARV yasikie tu kwa jirani.
Ziliuzwa ng'ombe na mbuzi kuzunguka kwa waganga kujua hasa "mbaya wetu" ni nani? Huyu mlozi wa familia ni nani? Hakuna hata mmoja aliyekuwa na wazo la kwenda mjini kwenye vipimo vikubwa.Na waganga wote tuliopita hakuna hata mmoja aliyeacha kutuambiwa kuwa "huyu karogwa kwa kutupiwa jini".Madawa na mitishamba ilijaa ndani kwa wingi bila kuleta matokeo chanya.Siku zikaenda na hali ya dada inazidi kuwa mbaya na ya kukatisha tamaa.Tulisafiri mpaka Morogoro sehemu za Vidunda kufuata mganga,lakini hakukuwa na uafadhali.
Wakati wote huu dada yangu mdogo na Mama ndio waliokuwa wauguzaji,ama hakika waliuguza bila tahadhari sababu hawakuwa na elimu juu ya mgojwa na namna ya kumuuguza.Baada ya kipindi kirefu cha mateso Dada alifariki.Naukumbuka mchana ule,mchana mgumu kuwahi kuuona katika maisha yangu ya ujana,ama kweli roho itokapo katika mwili mwnadamu hujijua.Dada isivyokawaida aliniita,niliitikia wito,akaniomba nikamate rozari na misale ya waumini,nifungue sala ya wagonjwa na tusali kwa moja.
Akiitikia kwa tabu na kwa kukoroma tulisali pamoja,baada kama ya dakika 15 niliona mtu amekaa kimya na baadae "kuhangaika" hapa na pale.Loooh!Kumbe ndio mwili ulikuwa unaacha roho na dada aliniita kuniaga,tuliagana kwa rozari na mishale ya waumini.Alasiri ya 08/03/1993.Upumzike kwa Amani.Baada ya kuzika maisha hayakuwa kama zamani,sehemu ya ng'ombe zilizotumika kunilipia ada zilipungua sana sbb ya mizunguko ya waganga na hali ya ugonjwa.
Hata anakufa hakuna aliyejua ulikuwa ni UKIMWI,wengi walilaani juu ya "uchawi" na jini lililotupiwa familia.Na ama hakika Waganga walisisitiza kuwa "jini" hilo bado linazungukazunguka..Litaondoka na mwingine.Bila kujua lolote Mama alianza nae kuugua,kwa dalili zilezile za Dada.Mama alikonda sana,nilirudi likizo ya kwanza ya kidato cha nne namkuta mama amelala nje juu ya mkeka amebaki kichwa tu,amekonda na kukondeana.Mtoto wa kiume nililia sana kwa hali ile ya Mama.Nikajisemea hili jini kweli litatumaliza wote.Baadae tena dada yangu aliyeshirikiana na Mama kumuuguza marehemu akaugua,dalili zilezile za Mama tukawa na wagonjwa wawili ndani ya nyumba...tuliuza mpaka ndama kuokoa maisha ya ndugu hawa.Hakuna wazo la hospitali,kila mtu ni kutegua mtego wa jini.
Siku moja akawa amefika Padre kigangoni kwetu,Padre huja mara moja kwa mwezi kusoma misa na kutembelea wagonjwa,baada ya misa ile nilimuomba Padre afike nyumbani kumuombea mama yangu na dada na hakika mama alistahili kuombewa sababu alikuwa mwanachama mzuri wa umoja wa Wanawake Wakatoliki Tanzania (WAWATA),hivyo ilikuwa rahisi kwa Padre kufika na kuwaona.Ndani ya nyumba ya nyasi yenye giza hata mchana wa jua kali Baba Paroko akaingia.Alipowatazama wagonjwa akatokwa na machozi.
Akahimiza waondolewe haraka na atawakimbiza yeye mjini kwa gari yake wakapate vipimo vikubwa...wachache sana waliokubaliana na padre wakijuwa kuwa ule ni ugonjwa wa kurogwa sio wa hospitala,na kuwapeleka hospital ndio mwisho wa mchezo.Nguvu za paroko na ushawishi wake ziskashinda,Mama na dada haraka mjini,hadi kufikia jioni majipu yakawa ni TB kwa wote wawili,na baada ya udadisi wa madaktari ikabidi ni mtoto wa dada aende kupimwa,naye tukamsafirisha mpaka mjini.Tobaaaa!Mtoto akakutwa na UKIMWI alioachiwa na mama yake,hivyo Mama na Dada waliambukizwa TB sababu hawakuwa na tahadhari ya kumuhudumia marehemu.Wakati huo hakukuwa na "Mpango wa kutokomeza Kifua Kikuu" wa kutoa dawa bure,hivyo ilihitaji kugharamia rundo la vidonge.Watu waliuza mifugo kununua dawa kwa shingo upande.Mama na dada wakawekwa hospitali na kunywa dawa kwa kuangalizi mkubwa sana,baada ya miezi mitatu afya zao zilirudi kwa kasi.
Kumbe haikuwa jini kama wale waganga walivyosema,ulikuwa ni UKIMWI kwa marehemu na kwa mama na fada ilikuwa ni TB.Maisha yakaenda na mama akarudi katika hali yake ya afya njema.Nikiwa mbioni kuingia kidato cha sita nikaanza kuugua sana nikiwa shuleni.Kikohozi na jasho kali wakati wa usiku.Kula sana chakula lakini ndani ya nusu saa nasikia njaa.Shule haina vipimo zaidi ya zahanati unayopewa dawa kulingana na dalili za ugonjwa.Niliugua sana sana kumbe nami ilikuwa TB,maana wote hatukuchukua thadhari wakati tukimuuguza dada,bahati nzuri shule ilinipeleka hospitali na kutibiwa mapema,ilibidi niahirishe mwaka mmoja ili nipate afya nzuri.Mwisho wa siku wote tukapona,haikuwa jini kwa dada wala kwa Mama,bali ni UKIMWI na TB.
Miaka miwili baadae mtoto wa dada akafariki,wakati huo hakukuwa na ujuzi wa kuzaliwa bila VVU hata kama mzazi anavyo,wala ARV haikwepo.Bwana mdogo alifariki katika mateso na mahangaiko makubwa sana.Tukamzika pembeni ya kaburi la Mama yake,na juu ya kaburi tukaandika "YEYE ANIAMNIYE MIMI HATAKUFA,BALI ATAISHI MILELE".Ni miaka zaidi ya 20 sasa,Wapendwa wetu wametangulia mbele za haki.UKIMWI ulikatisha maisha yao,ama hakika balaa la ugonjwa huu lisikie kwa jirani.Jamani UKIMWI ni chanzo cha umasikini,lakini elimu ya msingi ya afya ni muhimu kusambaa mpaka vijijini.Isingalikuwa mtumishi yule wa Mungu,basi "ujinga" wa kuamini jini ungeendelea.Hii hali ipo sehemu nyingi,kuona UKIMWI kama ugonjwa wa kurogwa.Wasichekwe wazee wetuu kwa kuamini ktk waganga na tiba mbadala.Tuwaelimishe na kuokoa jahaziNinawapa pole wale wote waliowahi kupoteza wapendwa wao kwa UKIMWI.Tuwaenzi kwa kuepuka gonjwa hili,kuwa waaminifu,kuacha kabisa au kutumia kinga kwa wasioweza kujizuia.
RAHA YA MILELE UWAPE EEE BWANA,NA MWANGA WA MILELE UWAANGAZIE,WAPUMZIKE KWA AMANI AMINA
cc: MziziMkavuWasiliana na MziziMkavu alishatangaza dawa ya UKIMWI.
Kama huna cha kumshauri au kumpa pole kwa yaliyo mkuta ni bora ungepita kimya kimya kwenye thread hii kwani post yako inatia kinyaa kwa watu wanaojielewa humu ndani.Wacha porojo, washakubali watatumika nini zaidi? Wafu nao wanaingia JF? Saa hizi wewe unaejifariji si wao, wao watathaminiwa kwa matendo yao ya hapa duniani walipokuwa hai na si kwa porojo zako.
Ukiwa muongo uwe na kumbukumbu.
Kwa hiyo mkuu Deception hakuna kitu kinaitwa UKIMWI??Na hakuna watu wanaokufa kwa UKIMWI??sasa hao tunaoambiwa wamekufa kwa ukimwi ni uwongo?
Mkuu Deception ulipotea sana, karibu uendeleze pale ulipo ishia.