Jinsi "Spritual Bonds" zinavyotesa ndoa za sasa

Jinsi "Spritual Bonds" zinavyotesa ndoa za sasa

waneemayote

Member
Joined
Oct 20, 2019
Posts
56
Reaction score
153
Nimekuwa nikifuatilia mafundisho ya dini na makala tofauti tofauti huku JamiiForums, leo ninanvyoandika Uzi huu nimeona makala inayosema kuchunguza ma-Ex za wake watu something like that nimeusoma ule Uzi nikaunganisha na yale masomo ya dini kuhusu ndo niliyoyasoma miunganiko ya kihoro. Uzi wa hapo juu mwandishi ameelza jinsi wake za watu wanavyoliwa karne hii na ma-Ex zao

Ukweli ni kwamba, unaposex na mtu unatengeneza Spiritual Bond naye, unasimamisha madhabahu pamoja na huyo mtu, sasa ikitokea umeolewa na mtu mwingine au umeoa na mtu mwingine bila kuvunja madhabahu ile kwa njia ya maombi na sadaka basi tambua ni rahisi kuja tena kushirki ngono na yule mtu tena endapo itatokea nafasi tena ya kufanya hivyo

Kwa mtazamo wangu ukitaka kuwa na ndoa yenye furaha na amani na mibaraka tele mbali na zile funguo tatu jitahidi sana katika ujana wako usijiingize katika ngono kwa namna yoyote ile na ikiwa umeshafanya hivyo omba toba kwa Mungu na vunja miunganiko ya kiroho na mtu au watu hao ulioshirikii nao ngono

Endapo utakuwa unataka kuoa omba sana kwa bidii Roho Mtakatifu akuongoze kuchagua mtu sahihi. Fuatilia historia ya mtu huyo na pia ombeni wote kwa pamoja kuvunja miunganiko yote ya kiroho na tabia za kurithi na madhabahu zozote za uk. Zaidi ya yote Ombeni Mungu awape hekima ya kuongoza Ndoa zenu vizuri


Karibuni kwa michango na nyongeza
 
Shukrani sana mtoa mada, natamani hili somo liwafikie wengi na walifanyie kazi, Usaliti umekuwa tatizo kubwa sana kwenye Ndoa na Mahusiano ya sasa,
tunahangaika kulaumiana na kutafutiana mchawi kumbe ni 'spiritual bonds' zishafanya yake..!
 
Wengine wanaolewa na kuoa sababu umri umeenda na wenzake wa Rika lake wapo kwenye ndoa sio kwa mapenz
 
Unakuta mke wa mchungaji anayekesha maombini anamegwa na houseboy au bodaboda, mchungaji nae anapita na wanakwaya. Wanakwaya kwa wanakwaya wanaseviana. Ndoa za wachungaji na wanakwaya maarufu zinavunjika kama ungo.... INA MAANA HAWA HAWAJUI KUFUNGA NA KUOMBA? Kuoa bikra sio guarantee kwamba hatochepuka. HIZI mambo za sijui spiritual connections, sijui madhabahu za nini ni kuongezeana hofu tu.
 
Unakuta mke wa mchungaji anayekesha maombini anamegwa na houseboy au bodaboda, mchungaji nae anapita na wanakwaya. Wanakwaya kwa wanakwaya wanaseviana. Ndoa za wachungaji na wanakwaya maarufu zinavunjika kama ungo.... INA MAANA HAWA HAWAJUI KUFUNGA NA KUOMBA? Kuoa bikra sio guarantee kwamba hatochepuka. HIZI mambo za sijui spiritual connections, sijui madhabahu za nini ni kuongezeana hofu tu.
Ni mtazamo wako pia tunaheshimu

Kwa jinsi ulivyoeleza unamaanisha wachungaji wake zao walkuwa mabikra, siokweli!!!!!

Anyway ukweli ni kwamba siku zote utavuna unachopanda soma wagalatia 5:22

Usitegemee kamwe uwe mchepukaji utaoa mke ambae hachepuki kamwe nasema kamwe ...

Utachepuka hatogundua na atachepuka hutogundua
 
Huenda unachokisema kina ukweli kwa kiasi chake; lakini kuchepuka kwenye ndoa kunasababishwa na tabia ya mhusika.

Hakuna kitu au sababu nyingine inayoweza ku-justify. Kuna watu wengi tu walikuwa na wapenzi kabla ya ndoa, hawajaomba wala kutoa sadaka, na hawachepuki baada ya kuingia kwenye ndoa.

Lakini pia kuna watu wengi tu walikuwa na wapenzi, wakafunga ndoa Kanisani na wakaombewa; lakini wameingia kwenye ndoa na wanachepuka kama kawaida.

Kuchepuka ni tabia ya mhusika tu. Nothing less, nothing more.
 
Back
Top Bottom