KEKO JUU
JF-Expert Member
- Jan 30, 2025
- 592
- 1,835
Damage control ni neno linalotumika kumaanisha juhudi zinazofanywa ili kupunguza madhara, kudhibiti hali mbaya, au kuokoa taswira/nafasi baada ya jambo baya kutokea.
Baada ya mauaji ya halaiki kipindi cha uchafuzi wa Oktoba 29 , serikali ya samuya inatumia mbinu hizi kufanya damage control
Kukataa na Kupunguza Uwezekano wa Mauaji na Ukatili (Denial and Minimization)
Serikali ya Samia imekuwa ikitumia mkakati wa kukataa uwepo wa mauaji au kupunguza idadi yake ili kuepuka kuwajibika. Hii inafanywa ili kutoa picha kwamba matukio ni ya kawaida au yamesababishwa na "maadui wa nchi".
Mfano : Wakati wa hotuba yake ya kuapishwa, Rais Samuya alilaumu "maadui wa nje" (foreign actors) kwa kuwasha ghasia, huku akidai uchaguzi ulikuwa wa haki na uwazi. Hii ilikuwa hatua ya kutoa lawama kwa nje na kutoonyesha kosa la serikali.
Wakati wa ripoti ya CNN kuhusu mauaji baada ya uchaguzi na miili iliyopigwa na polisi, serikali ilitoa taarifa rasmi ikisema inachunguza na kuthibitisha maudhui ya hicho kabla ya kujibu. Hii ilikuwa damage control ya kununua muda bila kukiri au kukataa moja kwa moja, na kutoangalia madai maalum kama makaburi ya pamoja au miili iliyotoweka
BBC: Waziri wa Mambo ya Nje Mahmoud Thabit Kombo alikataa ripoti zilizothibitishwa na picha na video za askari wakipiga risasi kwenye umati, akisema hakuna vifo vilivyothibitishwa, licha ya ushahidi kutoka shirika la haki za binadamu la Kiafrika. Hii ililenga kupunguza shinikizo la kimataifa.
Udhibiti wa Habari na Udanganyifu wa Umma (Censorship and Narrative Control)
Kutoa Takwimu za Kudanganya: Serikali imekuwa ikitoa takwimu za madhara ya mali (kama pikipiki 2,268 zilizoharibiwa) badala ya idadi ya waliouawa, ili kubadilisha mazungumzo kutoka kwa vifo kwenda kwa "hasara za mali". Hii inaonyesha kuwa mali ni muhimu kuliko maisha, na inafaa kwa kutoa lawama kwa waandamanaji kama waharibifu.
Kugeuza mjadala (changing the narrative)
Mfano saiz analeta mjadala wa kuongea na wazee wa mchongo wa dar,ili kuwahadaa watu wasizungumzie kilichotokea kwenye uchafuzi.
Mbinu hizi zote tunazifahamu, sisi sio wahenga wa mi
aka ya tisini