Jinsi serikali ilivyopoteza 'opportunity' ya kushika wadaiwa sugu wa 'Loan Board' (bumu)

Tangantika

JF-Expert Member
Aug 12, 2018
4,941
6,191
Japo wengi hawatapenda!

Katika zoezi la uandikishaji NIDA ndio kipindi pekee serikali ingeweza kuwabaini na kuwakamata wadaiwa sugu wa Bodi ya Mikopo ya chuo.

Serikali ingejipanga vizuri nusu ya wadaiwa wangebainika walipo. Kuna wadaiwa sugu hawajaajiliwa serikalini wala taasisi binafsi wanaendelea na Mishe zao na wengine wametusua wana uwezo wa kulipa Ila wanapiga chenga.

Huwa nashangaa kusikia bodi inatangaza majina ya wadaiwa sugu ilihali kuna njia nyingi sana za kuwakamata. Huenda serikali haina nia ya kuwakamata.

Vilevile huwa nashangaa watu waliokopa bumu kukwepa kurudisha, hivi serikali kwa nini isiunde mfumo wa kuwatosa bumu watoto wa wadaiwa sugu ili iwe fundisho, kuna kauli ibasema 'like father like son!'.
 
Serikali kusomesha wananchi ni jukumu lake.. ndio maana mkopo wa bodi hauwekewi dhamana.. na serikali ikidai kwa ubabe dunia itawashangaa wananyanyasa wanachi wake..

Bila kusahau hao viongozi wao walisomeshwa buree pia bila kudaiwa.. so wanaona aibu kudai dai maana hata wao wanadaiwa
 
Ulichokiongea ni cha kweli kuna mafala wengi tunawaona wana run tu ....hata kama hawajaajiliwa wafanyie utaratibu wa kulipa mbn watumishi wanalipa?

Walivyokuwa naenda club ,kunywa pombe ....mkopo urudishwe wawatafute sasa hivi wamesajili simu kuna mfumo wa nida kuwapata na kuwadaka ni faster tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
We pambana na hali yako fala mwenyewe, hizi hasira za kukatwa kijimshahara chako usihamishie kwetu. Umesikia shughuli za hii nchi zinakwama kisa wadaiwa wa loan board?
Ulichokiongea ni cha kweli kuna mafala wengi tunawaona wana run tu ....hata kama hawajaajiliwa wafanyie utaratibu wa kulipa mbn watumishi wanalipa?

Walivyokuwa naenda club ,kunywa pombe ....mkopo urudishwe wawatafute sasa hivi wamesajili simu kuna mfumo wa nida kuwapata na kuwadaka ni faster tu

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ulifurahia kupata ajira ukatuacha mtaani wewe katwa mpaka akili ikae sawa.
Acha tuwapige chenga angalau nasisi tufanye maendeleo. Mtoto wa masikini nianze kuhangaika kulipa 20M kwa usawa huu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu punguza wivu, Wewe kama unalipa endelea kulipa kama una dhamana yao mfano ajira. Serikali haiwezi dai watu kulipa madeni wakati haina takwimu ya vipato vyao. Hata nyenyew ina mkopo kibao inaishia tu kusamehewa au kulipwa taratibu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
shida ni kwamba kama bado unasaka ajira na haujaanza kulipa kuna adhabu, sasa siku ukianza kazi ndio unakutana na kitu 17m na wewe ulitumia 9m tu.

huu ni uonevu kwa sababu huyu mtu hakupenda akae kitaa muda mrefu bila ajira

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Serikali kusomesha wananchi ni jukumu lake.. ndio maana mkopo wa bodi hauwekewi dhamana.. na serikali ikidai kwa ubabe dunia itawashangaa wananyanyasa wanachi wake..

Bila kusahau hao viongozi wao walisomeshwa buree pia bila kudaiwa.. so wanaona aibu kudai dai maana hata wao wanadaiwa
Ninani kwambia Mkopo wa Elimu ya juu hauna dhamana? Ulisoma chuo gani wewe? Au ulilipiwa na wazazi wako ndo maana haya huyajui?
 
Ninani kwambia Mkopo wa Elimu ya juu hauna dhamana? Ulisoma chuo gani wewe? Au ulilipiwa na wazazi wako ndo maana haya huyajui?

Nimesoma udsm.. wakati mimi nasona hakuna dhamana yeyote katika fomu ya mkopo.. nimemaliza 2011
 
Nimesoma udsm.. wakati mimi nasona hakuna dhamana yeyote katika fomu ya mkopo.. nimemaliza 2011
Ulisoma UDSM ndiyo nini?

Aisee wewe vp? Ni nani akupe mkopo bila dhamana acha kudhalilisha chuo chako na serikali bila sababu. Hata kama Serikali na mapungufu yao waliweka utaratibu wa mdhamini. Kabla ya kupewa mkopo ni lazima ulikuwa unajaza mkataba ambao ulikuwa na sehemu ya wadhamini kujaza majina yao na sahihi.

Kama ni wazazi au walezi au mtu wako wa karibu alikuwa anathibitishwa na mwenyekiti wa serikali za mtaa wako na baadaye form hiyo ya mkataba unaipeleka mahakani au kwa mwanasheria ili kuthibitisha ulichokijaza ni sahihi au la?

Sasa pamoja na haya hapo UDSM kwenu palikuwa na utaratibu tofauti wa ule ulioandaliwa na Serikali kupitia Loans Board? Mbona Unaidhalilisha UDSM bila sababu ya Msingi wewe?
 
Back
Top Bottom