Jinsi ninavotamani siku zirudi nyuma ili niyafute haya...

Mdogo wangu,

Pole kwa yote yaliyotokea maisha mwako. Ilipangwa iwe hivyo ili uwe unavyotakiwa kuwa, usiumie. Kuna wengi wamepitia mara mia yako!!! Ni kwamba tu hawajashea kama ulivyoshea wewe.

Usisikilize wanaokuponda kwenye uliyopitia. Laiti kama watu wote tungeandika historia ya wanawake/wanaume tuliokuwa nao mpaka sasa ninahisi huenda ungesema afadhali yako! Watu wana story za kutisha zaidi.

Cha kuomba TU uwe na afya salama. Usisikitike wala kujidhuru kwa haya yanayokuumiza nafsi, ni suala la muda TU utasahau na maisha mengine yataendelea.

Asante kwa kushea nasi na nikutakie kila la heri kwenye maisha yako.

With love,
-Lizard-
 
Back
Top Bottom