Jinsi nilivyowahi kuumbuka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jinsi nilivyowahi kuumbuka

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mzizi wa Mbuyu, Jun 16, 2009.

 1. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #1
  Jun 16, 2009
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,499
  Likes Received: 1,080
  Trophy Points: 280
  Nimeona ndugu zangu muipate hii, ni stori ya kweli kabisa iliyo wahi kunitokea, japo kuna jina hapa nimelitumia kama langu lakini siyo. Endeleaaah!

  Katikati ya miaka ya tisini baada yakumaliza kidato cha sita, nilikuwa naishi na wazee wangu maeneo ya Tegeta jijini Dar es salaam huku nikisubiri kujiunga na chuo kimoja hivi jijini DSM, kuna tukio ambalo lilinifedhehesha sana ingawa ni kama nilijitakia, ndugu zanguni hebu fuatilieni tukio hili.

  Nyumbani kwa mjomba wangu maeneo ya Kinondoni kulikuwa shughuli(sherehe) iliyo tukutanisha ndugu wengi hata wale wa mikoani pia walikuja mjini kujumuika na wakawa wanalala palepale kwa mjomba kinondoni.

  Nikipindi ambacho, nilikuwa naanza kujua kunywa pombe, na pale zilikuwepo kibao!
  Basi bwana, pale jirani na kwa mjomba kulikuwa na dada mmoja hivi mzuri ‘ile mbaya’ alikuwa anaitwa Suzy,yeye alikuwa amemaliza kidato cha nne hivyo akawa yupo tu nyumbani kwao.Kwasababu ya shughuli ile aliombwa awe analala pale pale kwa mjomba ili kusaidia kazi mbalimbali na kweli akakubaliwa akawa analala pale.

  Sasa, unajua tena ujana bwana (labda na safari nilizo zitandika), ilikuwa ni muda mrefu sana toka nilipofanya mchezo ule wa kikubwa mara ya mwisho zile za ujanani ilikuwa niko form five! fikiria hapa nazungumzia habari ya baada ya kumaliza form six!! Lilishakuwa jangwa sasa!! Haukuwa ukame wa kawaida!! Mida ya jioni ilipofika ktk pishana pishana nikaanza kurusha ndogondogo,…. Siunajua mie nilikuwa nimemaliza form six yeye form four tuu… basi ikawa ndiyo silaha!
  English nyiingi…you know, eeh if I could do do do, I could be that, then you know, here I am…..yaani akazimia mwenyewe na kulainika maana nilimpigisha shule kali mno!

  Ilipofika saa moja hivi usiku nikapata nafasi ya kusimama nae hivi kwenye kagiza ka michongoma, we bwanaawee ujana hatari kwelikweli! Bunduki ilikuwa imekasirika vibaya sana, kidogo ijifyatue! nikambembeleza sana tumalize hata palepale fasta lakini akagoma kabisa, badala yake akanipa mpango huu; Yaani usiku nisiondoke kwenda Tegeta nyumbani nilale pale kwa mjomba, kisha akanielekeza kona anayolala sebuleni pamoja na akina mama wageni waliokuwa wanalala sebuleni. Ilikuwa ni kona ya kulia ukitoka kwenye korido chini ya swtchi za taa na feni, niende nikamuamshe pale watu watapokuwa wamelala, nikaona ni mpango safi kabisa! Moyo ukatulia kidogo…lakini ile nguzo ya moto ikwa inaendelea kuwaka huku nikihisi inatoa machozi mepesi kwa hasira!!
  Ilipofika muda wa wageni wa hapahapa Dar kuondoka nikapiga chenga hadi ikakubaliwa nilale pale hadi kesho yake asubuhi ndiyo niende nyumbani. Nikaona safi, nikawa hatua moja mbele ya mafanikio.
  Ilipofika muda wa kulala mie nililala chumbani na ndugu wengine wa kiume wageni kwa wenyeji, tulijazana mle. Kutokana na ulevi watu hawakuchukua raundi wakapitiwa na usingizi wa pono! Mie kamanda, waapi nilikuwa mkavu safari hii bunduki ikitweta kwa hasira, baada ya kama saa nzima na nusu hivi nikainuka taratibu na kuanza kunyata kuelekea sebuleni ambako kulikuwa kimya kabisa mudahuo…….nyatu, nyaat! Nyaaatu!...

  Nikafika ile sehemu aliyolala Suzy salama, alikuwa amejifunika shuka nyeupe hivi. Pale mahali palikuwa na kagiza kidogo watu woote mle walikuwa wamelala, nadhani ilkuwa ni fofofo. Nikainama, pale kwenye kona tu kutoka kwenye korido nikampigapiga tarrriibu Suzy kwenye bega,..alishtuka kidogo lakini akaendelea kulala. Nikabadilisha mwelekeo nikampapasa kwenye makalio tarratiibuuu huku niki sema Ssssssuuuzzzyhhh.. (yaani kwa sauti ya chini iliyoelekea kwenye sikio lake moja kwa moja) huku upigaji wa kiwowo chake ukiendelea ila safari hii nikijitaja jina ….ni mimi ‘Masanilo, Masnilooo, Massssannn!’ Sssuuu twende basi! Nikapiga kwa nguvu zaidi baada ya kuona hastuki.

  Hapa ndipo ulipo nikuta mkasa, kwasababu aliinuka ghafla na kuwasha taa.. Dah! Hakuwa Suzy bwana alikuwa shangazi yangu mke wa mjomba! Akasema “pumbavvv kumbe ndiyo michezo yenu hii!” “Yaani wewe una…. Hakumalizia, wala sikumsubiri amalizie…. Nikachomoka kwa spidi ya ajabu! badala ya kutokea mlango wa jikoni, nikatokea palepale kwenye mlango wa sebule na kwa mwendo wa kutembelea vidole gumba vya miguu, amini usiamini walikuwa watu lundo lakini sikumkanyaga wala kugusa mtu! Nahapo ndipo nilipogundua kuwa kumbe ile nguzo kuu haina lolote mbele ya hofu, maana ilanguka ghafla na kwa kishindo tuu!! (Nikaisikia ikipiga kwenye paja langu la kulia inakopenda kulalia!) Kwisha! Ikawa nguzo ya Uji!

  Basi bwana kwa mjomba hakukulalika tena, nikaanza kuhangaika kutafuta mahala pa kulala maana ilikuwa usiku sana, nisingeweza kufika Tegeta usafiri haukuwepo!
  Nisiwachoshe wapendwa, nilikuja gundua baadae kuwa kumbe mke wa mjomba usiku ule akaona ni vema akalala na kina mama wageni pale sebuleni na akachagua ile sehemu ya Suzy kwasababu ilkuwa rahisi kutoka kwenda chumbani ……sasa akawa amemhamisha Suzy pale, agh! Nae Suzy kumbe alikuwa amepanga kutolala ili nikitokea tu kwenye kona aamke anifuate, lakini du! Akapitiwa eti na usingizi!!

  Nasikia kina mama waliamshwa wakapewa kisa kizima,…! Mjomba alipoambiwa alicheka ssanaa! Na mengine meengi yakasemwa. Yaani niacheni tu jamani niliona soni kweli!  “Jina la Masanilo siyo halisi” nimelitumia tu ili story ieleweke sawasawa.
   
 2. F

  Froida JF-Expert Member

  #2
  Jun 16, 2009
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  ha ha ha vijana wengi yamewapata hayo hujatueleza suzy baadaye aliingia laini
   
 3. J

  Joyceline JF-Expert Member

  #3
  Jun 16, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 1,010
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Pole sana, ndo ujana , hiyo aibu uliipeleka wapi?
   
 4. Offish

  Offish Senior Member

  #4
  Jun 16, 2009
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 172
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Du, pole sana Masanilo ingawa umelifedhehesha jina la watu. Nimewahi kutana na Masanilo mmoja alikiuwa na kamchezo hakahaka, ulijuaje? Ungepitia mchezo wa kujificha utotoni ungejua mbinu za kubaini Suzy alipolala...
   
 5. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #5
  Jun 16, 2009
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,499
  Likes Received: 1,080
  Trophy Points: 280
  Waapi bwana, sikuwahi hata kugusa! hali ilikuwa tete maeneo ya kwa mjomba sikuwahi kukanyaga kwa muda mrefu mno! nikawa namtuma mdogo wangu akadodose habari!
  Lakini huyo Suzy sasa nae ni mtu mzima alienda shule na kaolewa, tukikutana tunaishia kucheka tu!
   
 6. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #6
  Jun 16, 2009
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,499
  Likes Received: 1,080
  Trophy Points: 280
  Mh, yaani! nashukuru watu husau.
   
 7. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #7
  Jun 16, 2009
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Pole sana. Ndiyo misanga ya ujanani. Ni sehemu ya makuzi ya mtu.
   
 8. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #8
  Jun 16, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Pole Kamanda mambo ya ujana achana nayo kabisa.....mimi nilisha wahi weka miadi na demu zamani, ikifika saa sita usiku nitupie jiwe juu ya nyumba yao, mamsap atakoka nje tumalizane kwenye kiambaza cha nyumba...nilirusha mawe kama matatu hivi kwenye ile nyumba ajabu akatoka baba mtoto akiwa na gobore.......ilinibidi nilale kwenye majani kwenye shamba la mahindi......huku nikuaibika sana. Demu tulipoonana kanisani akasema dingi ndo alikuwa amerudi toka ulevini.
   
 9. JosM

  JosM JF-Expert Member

  #9
  Jun 16, 2009
  Joined: Oct 11, 2008
  Messages: 684
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  kweli ujana sio mchezo! nashukuru ujana wangu niliutumia vizuri sikupata mikasa kama hii.Pole sana ndugu
   
 10. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #10
  Jun 16, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  hahaha Masanilo afadhali ulijificha maana duh sipati picha.

  nakumbuka wakati nasoma darasa la tatu wakati huo nilikuwa mpole sana kiasi kwamba nlikuwa naambiwa maringa. Siku moja nikiwa naelekea tuition mchana nje kidogo tu ya nyumba yetu nikawakuta vijana majirani zetu wakiwa wamekaa kwenye kijiwe. Mmoja wao alikuwaga ananisumbua sana kunitaka kimapenzi nikawa naogopa kumkatalia (alikuwa mgomvi, mvuta bangi na mkubwa kiasi) nilijua atanipiga na pia sikuweza kumkubali nikaishia kumkimbia kila nikimwona ili asikumbushie ombi lake.

  Basi siku hiyo aliponiona wacha anitolee uvivu kuwa naringa kitu gani kwanza naniliu yenyewe si mali kitu kwani hata nikibania italiwa na nyenyere nitakapokufa. Alipaka kwa nguvu tena bila tafsida. Sikuthubutu kumjibu kwani nilikuwa mwoga sana.

  Fedheha ilinipata nilipogeuka nyuma na kumkuta Mdingi amesimama getini akinitizama!! Mpaka leo huwa sisahau.

  Kuna siku nilikutana na yule mkaka ukubwani (akanambia yeye ni dereva tax - alikuwa na bonge la alama ya panga katika paji la uso- nilisikiaga aliingia kwenye ujambazi) duh
   
 11. D

  Dina JF-Expert Member

  #11
  Jun 16, 2009
  Joined: Sep 18, 2008
  Messages: 2,824
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Pole sana mheshimiwa, ila nimecheka mbavu sina. Jambo moja linalonishangaza, yaani ukakubali risk ya kuruka watu wote hao ukamfuate huyo Suzy pembezoni alikolala? What if watu wengine wangestuka in the process?
   
 12. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #12
  Jun 16, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Dina si wanasemaga ukishakuwa na miadi ambayo lengo ni kumridhisha mkulu baso yote yanawezekana? Wengine huamini kuwa wanaweza hata kupita juu ya maji ilimradi wafike kunako starehe!!

  In short akili huwa inawaza kitu kimoja tu so hizo risk unazoziwaza wewe wao huwa hakuna!! Hushangai wanaodiriki kutoa madudu yao na kufadhaika kwenye madaladala, huwa hawaogopi kuonekana !!
   
 13. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #13
  Jun 16, 2009
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Jamaa ameelezea hii stori vizuri sana. Yani umetuweka katika suspense hadi mwisho. Endelea kutwanga stori maana inaweza kuwa kipaji chako.
   
 14. Consultant

  Consultant JF-Expert Member

  #14
  Jun 16, 2009
  Joined: Jun 15, 2008
  Messages: 5,801
  Likes Received: 6,311
  Trophy Points: 280
  Darasa la tatu na mamtu yalikuwa yanataka kukumega!?
   
 15. D

  Dina JF-Expert Member

  #15
  Jun 16, 2009
  Joined: Sep 18, 2008
  Messages: 2,824
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Na kweli ndugu yangu, ndio maana wanadai hiyo midadi ikichachamaa, kichwani kunakuwa kutupu kabisaaa...
   
 16. Wayne

  Wayne JF-Expert Member

  #16
  Jun 16, 2009
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 663
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Yeah
  The the guy is good.
  Story yake aliyochagua kutusimulia ni kama vile unatazama 24 ya Jack Bauer or Lost ya akina Sawyer,muda wote roho ipo juu unataka kujua what is next.Safi sana.
   
 17. Che Kalizozele

  Che Kalizozele JF-Expert Member

  #17
  Jun 16, 2009
  Joined: Jul 20, 2008
  Messages: 778
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Hongera sana kwa uandishi mzuri na ufundi wa kutumia maneno,the story telling was fantastic.

  Mie nakumbuka kipindi hicho naishi mwanaza mdingi aliwahi kukamata barua niliyokuwa nimemuandikia shori mmoja tuliokuwa tunakaa nae kitaa.Demu alikuwa anaita ile kinoma,basi nikamuandikia barua,nikampa dogo ampelekee kisha mie huyo CCM kirumba kuangalia mechi(Tulikuwa tunakaa bugando)
  Kumbe dogo alimpa yule demu ile barua kukiwa na watu kibao akaona noma si akaipeleka kwa mdingi kama kushitaki.Narudi mpirani nakuta kimewaka ile kinoma.Mbaya zaidi kipindi hicho dingi alikuwa akinifundisha jinsi ya kuandika barua,sasa mother akawa anatia petroli kwenye moto kwa kudai eti nilkuwa nafanya practice.
  Washikaji walikuwa wanajua siku hiyo ningechezeaa kichapo sana,lakini wapi mdingi akanipa adhabu ya kutokwenda kucheza,ilikuwa adhabu kubwa sana kwangu.
   
 18. Che Kalizozele

  Che Kalizozele JF-Expert Member

  #18
  Jun 16, 2009
  Joined: Jul 20, 2008
  Messages: 778
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Unataka kumaanisha nini sasa,kwamba dadaa alikuwa mkali tangu kitambo au vipi?Toka darasa la tatu anatamanisha na anashawishi,si mchezo.ALipofika form one alikuwaje,sipati picha.
   
 19. Buswelu

  Buswelu JF-Expert Member

  #19
  Jun 16, 2009
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 1,989
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Wanaume wameubwa na vichwa viwili....tatizo haviwezi ku oparate at the same time....so kwa kesi ya mshikaji hapo ni kwamba kimoja kilikuwa kinaongoza mwingine...remotely.

  Regards
   
 20. Masanja

  Masanja JF-Expert Member

  #20
  Jun 16, 2009
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 3,595
  Likes Received: 3,763
  Trophy Points: 280
  Duh! Mshkaji umenikumbusha mbali. visa kama hivi vilikuwa common (sijui siku hizi) misibani na kwenye mikesha...ebanaaa eee..nani alishaenda kwenye Mkesha wa Mwenge? Duh..yaani hapo utafanya ufanyalo..hata kama ni kusingizia mwalimu mkuu kwamba anataka wanafunzi wote mwende kuimba kwenye mwenge utafanya hivyo. Sasa ukikutana na mdingi au mlezi noma anaweka ngumu..hakuna kwenda. Basi utafanya ufanyalo..ila lazima uende kwenye mwenge.

  Mimi inanikumbusha story moja ya ajabu kweli....mtaani kwetu aliishi daktari mmoja wa hospitali kuu (kipindi hicho yupo yeye pekee yake wilaya nzima)alikuwa na watoto wa kike wazurii..lakini kwa sababu walikuwa matawi ya juu..kila mtu alikuwa anawaogopa..basi tuko primary bana..mimi kwa utundu wangu nikamwandikia barua ya kumuomba awe rafiki yangu....ee bwana...mdada wa watu si akaenda kuwaonyesha ile barua braza na sista zake? ambao walikuwa wakubwa ofcourse..ngoja wanishukie kama mwewe...yaani hata kwenda shule nikawa naogopa..harafu so zaidi nikaogopa endapo lingesanuka mpaka home au kwa wazazi wake..yaani nilipewa kibano lakini nikashukuru halikusanuka zaidi. Hata kushtaki sikushatki. Nilikaa kimya! Maana kumtokea mtoto wa Doctor sijui ningesema nini mbele ya walimwengu! Mpaka tunamaliza primary demu alikuwa ananidharau sana..well hata uchumi ulichangia..ila before her I was hopeless.

  Basi..tukamaliza primary kila mtu akabahatika kusonga mbele..yule demu tulimaliza Form four mwaka mmoja..ila shule tofauti...basi akatokea akawa mshkaji katika ile likizo ya kusubiri matokeo ya form four..na ofcourse ilikuwa hivi kwa sababu sisi ndo tulikuwa "educated" mtaani..maana wengine waliishia la saba. Hamuwezi amini..nikarusha neno tena..demu akaingia laini bwana..duh...yaliyoendelea ni historia ila..ndo akawa demu wangu wa kwanza kum-do! Mtaa mzima wakawa wananiheshimu....ila kila nikimuona na nikikumbuka kibano nilichopewa na kaka zake..nilikuwa najitahidi ku-compensate huku nikisema...mvumilivu hula mbivu. At the end..ndo nikaenda Form five..safari ya yule demu kielimu ikawa imeishia hapo.

  Demu keshaolewa..na ni mshkaji tuu..tukikutana tunaongea vizuri!

  But ndo vitu kama hivi ukivikumbuka..unaona kabisa maisha ni safari ndefu sana. huwezi jua kesho utakuwa wapi. So just do good as much as you can. You never know.
   
Loading...