Kipenzi Changu
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 57,913
- 133,926
Lesson learned
Wale jamaa pamoja na ujanja-ujanja wa mjini lakini nahisi walikuwa wanatumia dawa.
Ilivyokuwa
Saa 10 asubuhi nikawa Ubungo tayari kuisubiri saa 12 bus liondoke kuanza safari ya kurudi kijijini. Hii ilikuwa 2007 likizo ya semister ya kwanza baada ya kujiunga Chuo Kikuu. Wakati nasubiri muda wa kuondoka nikawa nje ya bus na wahuni wa stend tukipiga stori.
Muhuni mmoja akanitonya ana simu ya Nokia ya GPRS. Anasema kwa kuwa nimekuwa mshikaji anaweza kuniachia kwa elfu 50 tu bei ya kishikaji. Nikamwambia sina mpango wa kununua simu. Jamaa akaanza kunitamanisha, akaanza kunionyesha mapicha ya X kwenye hiyo simu, kumbuka sijawahi kumiliki simu ya GPRS. Nikaanza kubadili mawazo, nikienda na hii simu kijijini watanieleza nini!!
Nikapiga hesabu kichwani akiba haikuruhusu, nilikuwa na elfu 20 tu, elfu 30 nyingine nilipewa na mama mkubwa nimpelekee bibi kijijini. Bado nikaona kuchukua simu sio maamuzi sahihi. Tukaendelea na stori na yule jamaa.
Ikafika saa 11.50 gari ikaanza kuingia kwenye foleni, ikabidi nipande. Kumbe yule mwana ananisoma. Nilipokaa tu naye akaingia, akaniambia mwanangu basi chukua tu hii simu hata kwa elfu 30. Nikaona isiwe taabu nikaingiza mkono mfukoni nikampa hela. Akanipa simu ikiwa kwenye bahasha. Ile akili niliyokuwa nayo mwanzo kwamba nichukue tahadhari na kuhakikisha napewa simu ikionekana ikayeyuka yote, kipuuzi kabisa nikakubali kuchukua simu kwenye bahasha.
Jamaa wakati ananiaga akaniambia usifungue sasa hivi si unajua hizi ni simu za wizi. Anasema hayo huku anaondoka na gari inaondoka. Baada ya kushuka tu ndio akili ikarudi. Pasipo kufungua simu akili zangu zikarudi na kuhisi hapa tayari nimetapeliwa. Hiyo ilinifanya nisifungue kabisa ile bahasha maana abiria mwenzangu niliona akinichora.
Nilienda kufungua ile simu Dodoma tuliposhuka porini wakati wa kuchimba dawa. Hapo nikajiridhisha nimeuziwa kopo la simu, ndani lina sabuni na shilingi ishirini kadhaa kutia uzito.
Kuanzia hapo nikaacha kuwadharau watu wanaotapeliwa kwa kuuziwa simu za mche na dhahabu.
Nilichojifunza ni kwamba wale jamaa wanatumia dawa za kupumbaza, ili umuepuke usifanye naye mazungumzo. Ukimruhusu kupiga naye stori umekwishaa