Jinsi nilivyonusurika kutapeliwa!

hv kweli mtu na akili zako timamu unamuamini vp mtu anaekwambia atakupa milion kwa kumsindikiza tuu??

wajinga ndo wanaoliwa siku zote
Well done mkuu, ukiyafikiria hayo pia fikiria kuna nguvu ya tamaa..
 
Sasa maelezo mbona yanakinzana na uhalisia.Yaani aogope kwenda Posta wakati kuja hapo mlipokutana hajaogopa?
Kwa akili za kawaida huoni kwamba hii ni stori ya kutunga tu?
Usilolijua ni kiza kinene mkuu.
 
Sawa mkuu, Share experiences unajikinga vip?
 
Pole sana mamy
 
hv kweli mtu na akili zako timamu unamuamini vp mtu anaekwambia atakupa milion kwa kumsindikiza tuu??

wajinga ndo wanaoliwa siku zote
Wanakuhadaa kwanza kabla ya yote bila shaka huwa na nguvu ya ziada jamani
 
Wako hivyo.

Mlimani City siku moja nakunywa Kahawa mule ndani opposite bank ya Exim zamani. Akatokea mama mweupe akanisalimia. Akaketi akidai aelekezwe ofisi ya Buzwagi kule Masaki akauze dhahabu. Nikamwelekeza kwani nilipafahamu.

Ghafla kijana mmoja meza ya pili akadakia. "Mbona huko mbali! Hapo TRA, karibu na Kanisa la ....... , Mwenge yupo mchungaji ananunua dhahabu."

Nikamwambia, "basi mpeleke mama!" Akasema, " nipo kazini, mimi ni dereva wa benki ya ........" Akaniomba, "We mpeleke sio mbali."

Akapiga simu kwa yule Mchungaji mnunuzi kwamba tunakwenda atupokee. Tukaondoka na yule mama ndani ya gari yangu hao mpaka karibu ya lile Kanisa. Tukafika tukapaki mita 20 hivi toka getini.

Baada ya muda akatokea mtu amevaa suti ya Kaunda na msalaba. Akafika na kunisalimia kikristo. Nikamjibu. Akapanda ndani ya gari. Mama akatoa kimkebe kimejaa mawe yaliyofanana na dhahabu.

Yule "mchungaji" akatoa kifaa mfukoni kama bisibisi akaipima ile "dhahabu." Akasema hasa hii ni "dhahabu" nitanunua. Mimi nami niliamini kuwa ni dhahabu kweli.

Akamgeukia mama akamwuliza, "Unayo akaunti benki?" Mama akajibu, "sina!" Yule "Mchungaji" akanigeukia, "wewe ndugu msaidie mama huyu. Unayo akaunti benki?" Nikasema, "ndiyo ninayo." Akaniagiza, "tupatie namba basi!" Ndipo nikapata mashaka.

Nikamwambia yule mama,

"Mama unafanya biashara hii huna akaunti benki? Siku zote unategemea akaunti za watu wengine? Iweje mniombe nikulete hapa kisha nigeuke kuwa wakala wa malipo. Benki wakiona kuna sh milioni 50,000,000 zimeingia ghafla Je, hawatashangaa zimetoka wapi. Unafanya mauzo ya aina hii hata gari huna kweli?"

Nikawashusha kutoka kwenye gari nikaondoka nimenusurika kuibiwa kwa njia waliokuwa wakiijua wao.

Mama alidai alikuwa anawakilisha umoja wa kina mama wachimbaji toka wilaya mpya moja kule Tanga. Utapeli mtupu.

Nimeandika kukazia hii mbinu ameitaja mleta mada - kuwepo kwa mtu wa pili- ambaye hujitokeza wakati muafaka kuchochea njama za kitapeli. Yule dereva katika tukio langu ndiye aliyekuwa mtu wa pili. Ukiona mtu wa pili anajitokeza ujue basi huo ni wizi.
 
Mbinu zao ni kama zina mfanano hivi

Unakuta wamejipanga zaidi ya mmoja kufanikisha utapeli

Duuh pole sana kaka
 
Hakika mkuu nimejifunza,

Kaka next time husisaidie mtu yoyotee yule ...awe mmama au mbabu...we fanya mambo yako....matapeli wa namna iyo ni wengiii sanaa sikuiziii...nashangaa yaani imekuaje kuaje mpaka wamekutoa nje ya bank bila ww kuwagutukiaaa....yna wamejazana sana mjinii kua makini....me sikuiz nishasema bora nionekane nna roho mbaya tu....nikiitwa na mtu yoyote sirespond naendelea na safar yangu....una bahat sana maana kuna wengine ukiongea nao tu wanakua washakuekea madawa
 
Shukrani mkuu,

Unajua hizi mambo unaweza ziona simpo, lkn ni mambo magumu sana, ukizingatia wengine wanatumia mpaka nguvu za giza kufanikisha utapeli!
kweli kabisa mkuu hata mimi nilishawahi tapeliwa kwenye ofisi yangu kwa njia ya hizi za nguvu za giza yaani unajikuta mwenyewe unatoa pesa yaani akili inapotea kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…