Hahahahahaha ulifanya la mbolea mkuu, afu ni kama ukiendelea kuwasikiliza wanakupumbaza zaidi yani!Hao hawakuwa tofauti na wale wanaotembeaga na pambo la dhahabu halafu mwingine anajifanya eti ni mshamba hajui kama ni dhahabu kuna siku kuna walinifata mitaa ya lumum ba Mwanza niliwatia adabu maana niliwakwanyua mitama ya kutosha,watu wa namna hiyo usiwakubalie hata kuwasikiliza.
Lukwafya
Asanteh Mkuu,Dada hii ingekula kwako vibaya sana, inasikitisha na kina mama au dada sasa wamejiingiza kwenye hii michezo michafu, ole wao wakikamatwa uswazi, kule watachomomwa moto tu..
Yaani muda wote huo ulikuwa hujahisi kitu? Yaani mpaka unatia huruma kwa upoyoyo wako. Hongera lakini kwa kusave hii kitu maana ulikuwa unaibiwa kitoto sana."Dollar iko sawa" yule dada aliongea, na sijui kwanini kila jambo yule dada alianza kuongea yeye( nahisi yule dada na yule kaka lao moja)
Duuh! Aisee Asanteh sana mkuuHapo shukuru Mungu ulikua sehemu ya wazi ndio maana uliweza kuondoka sababu hawakua na ujanja wala ucjisifu kama umewashtukia...kitendo cha kukubali kuondoka nao tayari ulishajimaliza...yani hapo inaonekana walijua huwezi kuwasumbua ndio maana wakakupeleka kwenye mazingira ya kawaida next time ukikubali kuondoka na matapeli ujue umekwisha, watatumia diplomatic way kama hyo ya kukuomba uache pesa ukizingua wanachukua kwa nguvu na kipigo juu...the best oprtion ni kuacha tamaa....
Shukrani mkuu,Yaani muda wote huo ulikuwa hujahisi kitu? Yaani mpaka unatia huruma kwa upoyoyo wako. Hongera lakini kwa kusave hii kitu maana ulikuwa unaibiwa kitoto sana.
Hakika mkuu, chamuhim hapo ni kufanya kazi nasio kutegemea pesa ya chap-chap.. kama nilichokifanya mimi.Hakuna hela rahisi hivyo kaa mbali na hao matapeli kwa kweli................ mimi sio muumini wa hela chap chap isiyokuwa na chanzo kamwe..........................
Ni kweli. Hongera kuporochoka hapo..ukizingatia wengine wanatumia mpaka nguvu za giza kufanikisha utapeli!
Hawafai mkuu, wakiona umesanuka wanatoka nduki kubwa..Mimi watu kama hawa nilikutana nao natoka ndani ya Tanzania Postal Banki. Stori zao ni namna hiyo hiyo hata approach zao ni hivo hivo na mara nyingi wanaviziavizia karibu na mabenki. Mimi niliponea chupuchupu kama huyu jamaa, nilikuwa nishatowa benki tsh 2 455 000/=!!!!