Jinsi nilivyomzidi ujanja mbwa wa Polisi wa doria nikamfungia ndani hahaha

Xavier Africa

Senior Member
Oct 4, 2017
180
384
Kwanza poleni na majukumu ya weekend
Nisiwachoshe leo nimeamua kisimulia tukio lililotokea uswazi ninapo ishi ilikuwa hivi

Kuna polisi wa kike alikabwa na vibaka usiku alikuwa anatokea kazini wakampora na kumchania shati

Sasa kitimu timu kesho yake polisi field force wakaja na kufunga mtaa wote wakitembeza adhabu wakiwa na mbwa wao aina ya German sherphed

Watu wote wakawa wamejifungia ndani mimi sina habari nafua na mtoto wa mwaka mmoja yupo pembeni anacheza

Ghafla naona mbwa anakuja kasi usawa wa mtoto anataka kumng'ata nikaacha kufua na kumkimbilia dogo na kumuweka pembeni mara mbwa ashafika nikasimama strong namtizama usoni huku mlango nimeacha wazi akawa ananishitua ili nitikisike kanitisha mara ya kwanza siku tishika mara ya pili nikatishika akanirukia nikamkwepa akazama ndani ya nyumba nikafunga mlango hahahahha akaanza kubweka kwa sauti gafla polisi hao washafika wanaulizia mbwa wao anabwekea wapi wakasikia sauti inatokea ndani kwangu wakaniuliza haroo wewe ndo umefungia mbwa wetu ndani nikajibu ndiyo alitaka kumdhuru mwanangu

Wakaniuliza " wewe ni mwanajeshi"? Nikajibu hapana ni raia tu wakasema unafanya kazi gani nikajibu ni mfanya biashara nikafungua mlango wakabeba mbwa wao wakaondoka ila wakiwa na wasiwasi na kujiuliza huyu jamaa ni nani haswa hahahaha

TRUE STORY from temeke dsm
 
Mwanaumee WA darr!
 
Story yako inasisimua inanikumbusha miaka ya nyuma huko mbeya mbabe mmoja aliitwa mwasimba siku moja kwenye mechi ya mpira zilizuka vurugu basi polisi wakaachia mbwa wao akaruka kumwelekea mbabe mwasimba alichvfanya mwasimba alimkaba roba yule mbwa akaanza kutoa ulimi basi kilichofuatia polisi ikabidi wamuombe msamaha mbabe mwasimba ndipo akamwachia lakini mbwa alikuwa hoi.
 
Back
Top Bottom