Jinsi nilivyokwepa mishale

Jinsi nilivyokwepa mishale

Muuza simu used

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2017
Posts
4,393
Reaction score
7,108
Wanawake wengi hasa wa kiafrica kama ilivyo kawaida yao kupiga mizinga tena ya mwendo kasi ndani ya mwaka mmoja 2019 nimefanikiwa kusave milioni 3.5!

Wa kwanza baada ya kujipigia mara mbili alinipiga mzinga wa laptop [emoji335] ambayo thamani yake ilikuwa laki 7, nikachukua hiyo laki 7 nikaweka kwenye kibubu nikafanya kama vile nimehonga na muhusika akachezea block matata.

Wa pili alijilengesha mwenyewe kwa vile aliniona nina mwenekano wa pesa baada yakuchakata mara moja na yeye akawa analilia simu Tecno ya laki 3,nikampiga kalenda hadi mwenyewe akakata tamaa sasa tumeishia tu ku review status kwenye WhatsApp nikachukua laki 3 nikaweka kwenye kibubu nikafanya kama vile nimehonga

Wa tatu huyu tulikutana kwenye mitandao ya kijamii huku na huku njoo tujuane mtoto alivyokuja akaliwa siku ile ile nikamsindikiza night kali nakuta sms baby kuna ndugu yangu anaumwa sana inahitajika laki 2 ya operation nikamwambia usijali kaka yangu ni daktari bingwa wa magonjwa yote kesho nitakuunganisha nae ndugu yako atapata matibabu yote bure,asubuhi yake nampa hi kisha nikamwambia tayari nipo na doctor hapa tukukute wapi akawa ajibu tena sms nikaona yes nimeshakwepa tena mshale mwingine nikachukua tena hiyo laki mbili nikaweka kwenye kibubu nikafanya kama vile nimehonga!

Nilifanya hivyo hivyo kupangua mishale ya mizinga kwa mwaka mzima wote wa 2019 nimekuja kuvunja kibubu hiki kipindi cha corona nimejikuta nina milioni tatu na laki 5 ndio natumia kipindi hiki cha mpito kwa raha mustarehe hadi lockdown zinaisha sitatoka kama nimechakaa nitatoka kama vile nimetoka kupekea mafao ya NSSF [emoji851]
 
Kama ukihonga hela halafu kiasi hicho hicho nacho ukamtumia mama yako mzazi baada ya mwaka utakuta mama kajenga chumba na sebule ila demu kajaza mawigi ndani na sura imepigwa mkorogo
 
Back
Top Bottom