Jinsi nilivyojinasua na mtego wa Al Shabaab

Ilikuwa mwezi wa 11/2019 nikiwa zangu kwenye mitandao ya kijamii,hasa Instagram, kuna mdada alini-follow lakini nikamsoma jina ila sikumjua ni nani,nikahisi haya ni mambo ya mtandao kila mtu anajivinjari kwa raha zake.

Baada ya wiki moja yule mdada anaitwa Husna alinitext basi nami nikareply,basi tukaanza kuchat nikamwambia nipo Tanzania yeye akanambia yupo Mombasa, tukawa tunachat kawaida kama marafiki wa mitandaoni na kupeana namba za WhatsApp

Siku moja akanitumia SMS WhatsApp,akanambia kuna mchongo wa hela kama unaweza nikushirikishe maana huu mchongo hauhitaji pesa kutoka kwako yaani ni wewe tu,na wala si kazi ya kuuza mwili lah! Hasha ni kazi fulani hivi ya kufanya kazi kwenye kampuni ya Fulani hapa Mombasa,ghafla akanitumia picha zake akiwa kwenye nyumba fulani ya kiwango na gari akiniambia kutokana na kazi anayofanya kwenye hiyo kampuni ya usafirishaji sasa hivi ana magari 3 ya kutembelea,nyumba tatu za kiwango na moja ipo Tanga

Baada ya siku kama tatu hivi akanitumia sh laki moja za kitanzania kwa airtel money, na akanambia kwa vile wewe shost yangu kila wiki hasa jumamosi lazima anitumie laki 120000 ya kula,nikawa naanza kumwamini huyo mdada

Tarehe 23 mwez disemba aliniomba niende tukutane Arusha,ila kwa sababu ya shughuli za hapa na pale nikamwambia fanya tarehe 3 January ,basi akakubali,kama tarehe 28 hivi desemba akanitumia laki 3 nauli

Tarehe 1 nikawa Arusha,nilipofika Arusha nikamtext nimeanza safari,na yeye akasema basi na mimi ngoja nianze safari

Kesho yake asubuhi akanambia hawezi akaja Arusha mjini badala yake tukutane Namanga,nikakubali,akaniuliza kama nimefika Arusha mjini nikamwambia nimefika.Asubuhi nikachukua usafiri nikafika Namanga,akanambia nivuke boda niende upande wa pili,nikaenda tukakutana naye ila alikuwa na wadada wawili wenye asili ya kisomali,basi tukapanda kwenye gari lake tukaondoka kama km 2 hivi tukaingia hotel moja hivi,akaagiza supu ya nyama kuku tukawa tunakula pale basi tukizidi kufahamiana zaidi,akanambia wale wadada wengine ni marafiki zake wanaofanya kazi kampuni moja ila wao wanakaa Nairobi Estate Nairobi city,naye akanitambulisha kwao,akawambia ni rafiki yangu Mtanzania anakaa Mwanza kwa sababu ni rafiki yangu nataka tumuingize kwenye kampuni yetu si ndio jamani,wale wakaitikia ni kweli manager hamna shida

Tukiwa tunaendelea na ile breakfast Dada mmoja akapokea simu,akawa anaongea kisomali nikawa nasikia maneno kama Nairobi,Kisumayu na Lamu na salamu ya asalam allekhum,
Baadae wakaanza kuongea hicho kisomali, nikawa najiuliza kwa nini hawaongei kiingereza na huku ni wakenya au kiswahili lakini sikupata jibu

Wakanigeukia mimi, mmoja anaitwa Ashura akanambia sasa sister tutaenda Nairobi na wewe ili tukafanye mpango wa kukuingiza kazini,na ukisha ingia kazini manager atakupa pesa utarudi Tz ili ufanye mpango wa kuhamia Mombasa kikazi" nikasema hamna shida,

Yule Husna akatoa nauli,akampa Ashura sh elf 50 za Kenya akampa Aisha sh elf 45 na mimi akanipa elf 30,yeye akadai kuna mambo anayaweka sawa hapo Namanga,ila akawambia kwa kuwa mimi sina passport inabidi nisiwe muongeaji sana kwenye basi,na mtu akaniuliza nisijibu,hao wengine watanijibia ,nisiwe na wasi wasi .......Itaendelea

Sent using Jamii Forums mobile app
njoo bundesliga tumalizie chenji!!
 
Mamutu ya kwa mama Kagoma ni majitu basi baba .Majongo ajabu.
 
Nahisi ni chai..but let me wait
Wala usihisi. Hii ni chai 100%. Hili ni dume wala siyo jike. Huwa linakuja hapa na story za alinacha mara kwa mara!
Ona hii:
 
Ninaweza kukuamini maana ndivyo wanavyo recruit watu kwa njia ya mtandao na wame recruit watu wengi sana sana kwa stye hiyo

Mkuu wanawake huwa wanatumia kwa kukamata au hata kuuwa kabisa wakihitajika
Ila mishe kama hizi zinazochukua mda mrefu kumshawishi mtu hawawezi kutuma mwanamke kwani wana tamaa na wanaweza kushawishika na kumpenda huyo wanaetaka akafanye mabaya
Wanawake walitumika sana kutaka kumuuwa Fidel Castro na wakubwa wengi hata wauza ngada wakubwa wanatumiwa wanawake yaani misheni inaisha haraka na ikishindikana mara moja hana kazi tena



Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Mtandao huu huu? Ukutane na MTU akusafirishe hadi Kenya? Tukutane Arusha? Sawa, Tukutane Namanga? Sawa! Tukutane upande wa pili, sawa! Panda gari; sawa! Tunywe supu; sawa!

Dah una hatari aiseeeee. Sawa nafuatilia kwa karibu! Weka basi January ya mwaka gani!

Sent using Jamii Forums mobile app
Kaka braza hujawahi kutana na maisha magumu wewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nlizani hadi kutaka kuuza figo kumbe bangi tu,hata mdogo wangu wa la7 anauza bangi mlale morogoro
Ana ajili sana! Niunganishe nae aiseee. Ila ya Moro haiko strong sana kama ya Tanga Handeni, Korogwe na Lushoto
 
Back
Top Bottom