Jinsi nilivyojinasua na mtego wa Al Shabaab

Jinsi nilivyojinasua na mtego wa Al Shabaab

cutelove

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2017
Posts
3,586
Reaction score
8,389
Ilikuwa mwezi wa 11/2019 nikiwa zangu kwenye mitandao ya kijamii,hasa Instagram, kuna mdada alini-follow lakini nikamsoma jina ila sikumjua ni nani, nikahisi haya ni mambo ya mtandao kila mtu anajivinjari kwa raha zake.

Baada ya wiki moja yule mdada anaitwa Husna alinitext basi nami nikareply, basi tukaanza kuchat nikamwambia nipo Tanzania yeye akaniambia yupo Mombasa, tukawa tunachat kawaida kama marafiki wa mitandaoni na kupeana namba za WhatsApp.

Siku moja akanitumia SMS WhatsApp, akanambia kuna mchongo wa hela kama unaweza nikushirikishe maana huu mchongo hauhitaji pesa kutoka kwako yaani ni wewe tu, na wala si kazi ya kuuza mwili lah! Hasha ni kazi fulani hivi ya kufanya kazi kwenye kampuni ya Fulani hapa Mombasa.

Ghafla akanitumia picha zake akiwa kwenye nyumba fulani ya kiwango na gari akiniambia kutokana na kazi anayofanya kwenye hiyo kampuni ya usafirishaji sasa hivi ana magari 3 ya kutembelea, nyumba tatu za kiwango na moja ipo Tanga.

Baada ya siku kama tatu hivi akanitumia sh laki moja za Kitanzania kwa airtel money, na akanambia kwa vile wewe shost yangu kila wiki hasa jumamosi lazima anitumie laki 120000 ya kula, nikawa naanza kumwamini huyo mdada.

Tarehe 23 mwezi Desemba aliniomba niende tukutane Arusha, ila kwa sababu ya shughuli za hapa na pale nikamwambia fanya tarehe 3 January, basi akakubali, kama tarehe 28 hivi Desemba akanitumia laki 3 nauli.

Tarehe 1 nikawa Arusha, nilipofika Arusha nikamtext nimeanza safari, na yeye akasema basi na mimi ngoja nianze safari.

Kesho yake asubuhi akaniambia hawezi akaja Arusha mjini badala yake tukutane Namanga, nikakubali,akaniuliza kama nimefika Arusha mjini nikamwambia nimefika.

Asubuhi nikachukua usafiri nikafika Namanga, akaniambia nivuke boda niende upande wa pili, nikaenda tukakutana naye ila alikuwa na wadada wawili wenye asili ya kisomali, basi tukapanda kwenye gari lake tukaondoka kama km 2 hivi tukaingia hotel moja hivi.

Akaagiza supu ya nyama kuku tukawa tunakula pale basi tukizidi kufahamiana zaidi, akanambia wale wadada wengine ni marafiki zake wanaofanya kazi kampuni moja ila wao wanakaa Nairobi Estate Nairobi city.

Naye akanitambulisha kwao, akawambia ni rafiki yangu Mtanzania anakaa Mwanza kwa sababu ni rafiki yangu nataka tumuingize kwenye kampuni yetu si ndio jamani, wale wakaitikia ni kweli Manager hamna shida.

Tukiwa tunaendelea na ile breakfast Dada mmoja akapokea simu, akawa anaongea kisomali nikawa nasikia maneno kama Nairobi, Kisumayu na Lamu na salamu ya asalam allekhum.

Baadae wakaanza kuongea hicho Kisomali, nikawa najiuliza kwa nini hawaongei Kiingereza na huku ni Wakenya au Kiswahili lakini sikupata jibu.

Wakanigeukia mimi, mmoja anaitwa Ashura akaniambia sasa sister tutaenda Nairobi na wewe ili tukafanye mpango wa kukuingiza kazini, na ukishaingia kazini manager atakupa pesa utarudi Tanzania ili ufanye mpango wa kuhamia Mombasa kikazi, nikasema hamna shida.

Yule Husna akatoa nauli, akampa Ashura sh elfu 50 za Kenya akampa Aisha sh elfu 45 na mimi akanipa elf 30, yeye akadai kuna mambo anayaweka sawa hapo Namanga, ila akawambia kwa kuwa mimi sina passport inabidi nisiwe muongeaji sana kwenye basi, na mtu akaniuliza nisijibu, hao wengine watanijibia, nisiwe na wasiwasi.

Itaendelea

Basi baada ya dakika chache basi la shuttle likafika likawa linatokea Arusha ,tukapanda tukaanza safari

Baada ya saa mbili hivi basi likawa linakaribia kufika Nairobi city,wale madada wakaomba konda watushushie sijui sehemu gani sikuipata vizuri,nje kidogo ya mji ,baadae wakaita tax tukapanda,Tax ikaanza kuingia mjini mara wapite Uhuru street, mara nasoma kibao Lagos street,mara Kimanth road,nikawa nafikiria kichwani sasa hapa tunaenda wapi

Mara wale wadada wamwambie dreva pita Nkrumah ukatokee Spanish sjui nini dah!,kwa kuwa ni mgeni wa Nairobi sikujua nakoelekea ni wapi

Baada ya saa moja na nusu hivi ubao niliosoma wa mwisho ni Machakos filling station,baada ya dakika 10 tukashuka tukatembea kwa mguu kama dakika 15 hivi tukaingia kwenye mji mmoja mkubwa na geti kubwa,wakabonyeza kengele mlinzi na mdada mmoja wakaja wakafungua na wakatupokea tukaingia ndani ya nyumba hiyo

Baada ya Muda mfupi wale wadada wakaaga,huku wakiniambia nisiwe na wasi wasi niwe huru, kwamba watakuja baadae kunichukua

Basi tukabaki na yule dada niliyemkuta kwenye ile nyumba kubwa zaidi aliye nambia nimuite mama Mariam anakaa na mume wake hapo

Baadae kidogo mume wake akaja kama mtu mzima hivi akajitambulisha kama Mr Khan 60s,akanikaribisha vizuri ghafla Husna akanipigia sim akanambia hapo ni nyumbani kwao nisiwe na wasi wasi,basi nikahisi kuna usalama hapa

Kuna mdada mwingine alikuwa anaishi kwenye ile nyumba aliniambia anaitwa Rara,alinisimulia maisha yake walivyo hangaika kutoka Djibouti hadi Uganda na walivyokutana na mama mwenye nyumba kwenye mitandao ya kijamii,na ana wiki tatu hivi tangu aingie kwenye ile nyumba akitokea Uganda

Kupitia huyu dada ndo nikahisi hapa huenda si salama

Akanambia "Tulipokutana na huyu dada kupitia Facebook tukaanza kufahamiana,yeye mwenyewe akanifuata nyumbani kwetu Busia na akawambia wazazi wangu kuwa nakuja kufanya kazi kwenye shirika la utangazaji lakini nilivyoingia kwenye hii nyumba baada ya siku mbili wanilazimisha niwape sim yangu,nikawapa,tangu hapo siruhusiwi kutoka nje wiki ya tatu sasa nimo humu ndani kazi siioni" Ingawa alikuwa anaongea kiswahili kibaya kibaya hivi akichanganya na kiarab ila nilkuwa namuelewa

Alivyonambia hiyo stories nikahisi hapa sidhani kama kuna usalama,nikaingia WhatsApp haraka nikamwambia ndugu yangu mmoja "Nipo Nairobi kwa ajili ya kazi lakini hapa nilipofikia sidhani kama kuna usalama"

Ikawa jioni hivi saa 1 yule Mzee khan akaniita sebuleni kwake akanambia kwa lugha ya kiingereza kuwa nimpe sim yangu,halafu nichukue passport amenitafutia ya kusafiria Kenya na kwingineko" Nikawa nasita akanikodolea macho makali ikabidi nifanye anavyotaka,nikampa akanipa passport ile nisome ,akanambia kuanzia sasa wewe utaitwa Nadia raia wa Djibouti, akaniomba passport ile kuwa anitunzia

Basi hapo nikaanza kujawa na hofu,nikaanza kujutia kiherere changu cha kutaka kufahamiana na watu wenye pesa

Muda kama saa 8 za usiku tulikuwa tumelala mimi na Rara tukaamshwa tukaambiwa tutakuwa na safari ya Mombasa hivyo tujiandae ndani ya dakika 20 tuwe tayari,alituambia Mzee Khan

Tukaoga na wakawa wametuletea nguo zingine za kuvaa,na wakatupa hela kila mtu Ksh 20000 akatuambia kuna gari litakuja kuwachukua msubiri kidogo, baada ya muda mchache gari aina ya Rv4 nyeusi ikaja tukapanda,alikuwemo dreva tu tena wa kike mwenye asili ya kiarabu

Tukapanda gari likaanza kukata mitaa,mimi na mwenzangu tukakaa siti za nyuma kama dreva alivyotuambia tukae nyuma yeye akae mwenyewe mbele

Kama dakika kadhaa hivi tangu tuingie katikati ya mji,ghafla akaanza kwenda speed mara aende barabara fulani mara apinde kona aingie mtaa mwingine kwa speed lakini mara akachukua sim akaanza kuwasiliana kwa kiarabu ,mwenzangu si anakijua,akaninong'oneza inasemekana gari hili kuna wanausalama wanalifuatilia,duh moyo ukalipuka mungu wangu!

Akakata kona akaingia barabara nyingine Mombasa road akasimama pembeni akasema tushuke tusimame hapo atarudi kutuchukua atupeleke bus stop ya Mombasa,tulivyoshuka tu Rara akanambia mwenzangu,hapa hapa nikuondoka,tukaondoka speed kutoka pale tukaita Tax ,Rara akamwambia tupeleke Ushanga karibu na Fire

Tax ikaanza kutembea,tukafika maeneo hayo tukashuka,mwenzangu akaanza kuniambia nina wasi wasi wale watu si wema,kama si Al shabaab ni bahati maana sometimes walikuwa wanaongea kiarabu cha kuficha ili nisiwaelewe lakini kwa uelewa wangu niliong'amua kuna ualishabu pale maana kuna siku walisema kwa kiarabu tupelekwe sehemu moja Jeezira ,wazo likaja Jeezira si ni Somalia,tufuate nini somalia"

Kwa kuwa hatukuwa na sim tulimuomba dada fulani pale mtaani baada ya kusimulia yaliyotupata,Rara akapiga sim kwao,kwao wakamwambia kuna ndugu yao hapo Nairobi atakuja kuwachukua

Saa 12 asubh akaja na gari lake akatupeleka kwake ,tukamsimlia yaliyotukuta akatuhurumia sana ,akatuonya tuwe makini na watu tusio wajua,akaninunulia sim na laini ya aitel ya Kenya,nikatafuta ndugu zangu nikawasimulia nikawambia nipo salama

Kesho yake yule kijana na Rara wakanisindikiza mpaka Namanga nikapanda gari hadi Arusha kesho yake nikaondoka Arusha nikarudi kwangu

Kuanzia sasa interaction na watu kwenye mitandao nimeacha,huwa najikuta nawaza hivi tungekamatwa na usalama sijui nini kingetokea kwenye maisha yangu,ila mungu ni mkubwa
 
Back
Top Bottom