Kwanini dalaldala za Mawasiliano ziliandikwa simu 2000?

Kwanini dalaldala za Mawasiliano ziliandikwa simu 2000?

Manyanza

Platinum Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
21,755
Reaction score
57,215
Kwanza kabisa usahihi ni "SIM 2000" na siyo "SIMU 2000". Kosa la kuandika "SIMU 2000" badala ya "SIM 2000" yaani kuongeza herufi "U" kwenye neno "SIM" na kuja kusomeka "SIMU" lilifanywa na linaendelea kufanywa na wale wanaopaka rangi za mikanda ya daladala. Daladala za mwanzo wakati wa ufunguzi wa kituo kile zilikuwa zimeandikwa "SIM 2000" na siyo "SIMU 2000". Eneo lile lipo SINZA,tena jirani na SINZA MADUKANI kwa hiyo watu waliamini "SIM 2000" ilikuwa ina maanisha "SINZA MADUKANI 2000". Kumbuka namba za nyumba zote maeneo hayo mpaka kule shule ya Mugabe mpaka upande wa huku MADUKANI zina anza na neno SIM...... Kwa mfano utakuta nyumba imeandikwa SIM 45, SIM 96, SIM 32 nk. Eneo hilo la SIM 2000 lilikuwa linamilikiwa na shirika TPTC (Tanzania Post and Telecommunication Cooperation),Shirika La Posta Na Simu ambalo baadae liligawanywa na kutoa TTCL,TCRA na POSTA. Eneo hilo lilikuwa na antena nyingi za simu kama zile zilizokuwa pale nyuma ya stesheni ya TAZARA (Kiwalani) ambazo zilikuwa ni za RTD au zile zilizokuwa pale kituo cha uwekezaji cha Benjamin Mkapa (External) maarufu kama EKSITENO nazo zilikuwa ni za RTD,au kama zile zilizokuwa pale Ukonga Minazi Mirefu, maarufu kama BANANA,ambapo pamejengws makao makuu ya Mamlaka Ya Hali Ya Hewa. Sasa eneo lile la "SIM 2000" lina maana ya "SINZA MAWASILIANO 2000" yaani kuanzia kiwanja namba 2000 na kuendelea. Kama unaelekea Mwenge,kabla ya Mlimani City,upande wa kulia utaona jengo la TCRA ambapo eneo hilo lote ndiyo linazagaa mpaka hapo.
IMG_20240421_141644_247.jpg
 
Nakumbuka ilinipa shidasana zamani nilikuwa naenda dar likizo tu 😀😀
Kunasiku nilienda kukutana na rafikiyngu akaniambia nipande hizo gari nikashuka nitakota stand nikatembea kidogo akaniuliza uko wapi nilivoona zile ghorofa nikamwambia nipo Mlimani city aisee alinicheka sana😂😂😂😂
 
Nakumbuka ilinipa shidasana zamani nilikuwa naenda dar likizo tu 😀😀
Kunasiku nilienda kukutana na rafikiyngu akaniambia nipande hizo gari nikashuka nitakota stand nikatembea kidogo akaniuliza uko wapi nilivoona zile ghorofa nikamwambia nipo Mlimani city aisee alinicheka sana😂😂😂😂
Na ndio maana huwa tunasema Mawasiliano na sio SIMU 2000
 
Sisi wa Mchambawima tukae pembeni tusubiri majibu.
Mateja wa Ubongo Bus Terminal pale panapojengwa Maduka 2000 ya Wachina, wale mateja wauzaji wa Sabuni enzi hizo wakijifanya wanakuuzia Simu ukiingia line umeliwa wanajua kwanini pale panaitwa SIMU 2000
 
Back
Top Bottom