Jinsi Marekani ilivyotandikwa na Japan bandari ya Pearl

N'yadikwa

JF-Expert Member
Aug 10, 2014
5,152
2,000
Shambulizi lililotekelezwa na ndege vita za Japan dhidi ya Marekani katika Bandari ya Pearl huko Hawaii halitakaa lisahaulike na Wamarekani.Walipigwa vibaya.

Kimsingi lilikuwa shambulizi la kushtukiza. Marekani hawakutarajia kilichowatokea.

Shambulio hilo ndilo hasa lilimchagiza Marekani kushiriki Vita ya Pili ya Dunia; pia wadadisi wa mambo ya vita wanadhani hiyo ndiyo sababu ya Marekani kushambulia Hiroshima na Nagasaki. Kwamba alikuwa analipiza kisasi.

SHAMBULIO LENYEWE:

Shambulizi la anga kwenye bandari hii lilifanywa na Japan ikinuia kumzuia Marekani asiingilie wakati itakapokuwa inawatandika Uingereza na washirika wake waliokuwa wakishadidiza kichapo Kusini Mashariki mwa Asia, Kimsingi Uingereza alikuwa na swahiba wake Netherlands...Sasa Japan ikaogopa kwamba isingeweza kuyarudisha nyuma majeshi ya Uingereza na Netherlands bila kumkata makali Marekani ambae angewaunga mkono hao Wamagharibi wenzie.

Bandari hiyo ambayo ilikuwa ngome muhimu ya Marekani kwa vikosi vyake vinavyopaswa kuwa macho katika Pacific iliharibiwa vibaya sana...Takwimu zinaonyesha kwamba;

Raia wa Marekani 2403 waliuawa na wengine 1140 walijeruhika...
Ndege 188 ziliharibiwa kabisa
Ndege 159 ziliharibiwa kiasi cha kadri
Manowari 4 zilizamishwa
Nyambizi 4 ziliharibiwa kabisa
Meli 2 za kawaida zisizokuwa za vita ziliharibiwa

Jumla ya ndege vita na zile za kubeba makombora 353 zilihusika kutekeleza operesheni hiyo ya 'kumtuliza' Marekani iliyoanza mapema saa Moja asubuhi ya tarehe 07/12/1941.

Aidha Japan ilienda kushambulia kisiwa cha Guam kile alichotishia Kim juzijuzi hapa kwamba atakitwanga...Kisiwa hiki ikumbukwe ni milki ya Marekani pia...

Rais wa Marekani wakati huo Franklin D Roosevelt alijitetea kwamba Marekani imebafuliwa kwa sababu Mshambuliaji hakutangaza vita bali alifanya shambulizi la ghafla...aliitamka Disemba 7 kuwa siku ya kukumbuka.

Baada ya kichapo hicho Marekani mnamo tarehe 08/12 /1941...yaani siku inayofuata wakatangaza vita na Japan...

MTAZAMO NA HOJA YA SWALI : Je,Jambo kama hili Korea Kaskazini hawezi kulifanya na hatimae akamchokonoa Mmarekani WWIII ikaanza?...Wababe acha watunishiane sie yetu macho.

COPYRIGHT RESERVED na Wikipedia
USS_West_Virginia2.jpg
PICHA : Manowari mojawapo ikizamishwa baada ya kuchapwa kombora kutoka degevita la Jep.
 

Papaa Gx

JF-Expert Member
Oct 10, 2016
6,674
2,000
Nakumbuka sana hilo tukio kipindi hicho niko Marekani aisee ilikuwa noma sana
 

LICHADI

JF-Expert Member
Feb 4, 2015
3,427
2,000
Na ndio vita inavyoanzaga wakuu mi nawaambia tuombe sana haya mambo yasitokee kwani vita huwa inaanza hivi hivi kimzaaa mzaa na siku mkorea anaweza akakosea kurusha hayo makombora kake mwishowe akayaingiza kwenye ardhi ya japan au south korea au gata kwa bahati mbaya yakiangusha ndege itakuwa hatari sana
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom