sasa kumbukeni CCM imetunyonya kwa miaka 50.. lakini wapo watu wanaishabikia.. kama tunakataa wizi huu wa mitandao tukumbuke pia kukutaa wizi wa CCM hapo mwakani 2015
Wewe jina linalokufaa kwa uzi huu ni ''MNAFIKI'!
kwa upande wa bahati nasibu washindi wanakuwa ni wa ukweli. hakuna uchakachuaji wowote unaofanyika...hapa ni uhakika 100%
wakae wababuke m@k@|i0? hili ni kaa la moto!
Mkuu asante kwa taarifa nzuri kwetu. Ungetupatia pia maujanja jinsi ya kujinasua na mitego hii, kwani matumizi ya simu hayakwepeki.
mkuu, ujajanja uliopo ni kwamba usiweke salio kubwa kwenye akaunti yako. nunua vocha nyingi za 500 ukae nazo mfukoni...recharge tu pale unapotaka kununua bundle. ukijipendekeza kuacha fedha kwenye akaunti, zitatafunwa na hawa mafisadi.
mkuu hizi michezo za bahati nasibu....washind wanakuwa n wa kweli au n waku tengenezwa....?
Mkuu usidanganyike kuna jamaa namfahamu anademu wake anapiga kazi voda tena anakitengo kikubwa tu,sasa basi jamaa kila droo za washindi jamaa lazima achukue jamaa ameshawai kupata Hyundai,pesa na droo kama za simu.tena demu wake ndiyo anamuambia "nimekuingiza kwenye droo watakupigia simu" hapo ndiyo nikagundua haa kumbe.
mkuu, ujajanja uliopo ni kwamba usiweke salio kubwa kwenye akaunti yako. nunua vocha nyingi za 500 ukae nazo mfukoni...recharge tu pale unapotaka kununua bundle. ukijipendekeza kuacha fedha kwenye akaunti, zitatafunwa na hawa mafisadi.
Mwezi wa nane nilimtumia mke wangu muda wa maongezi shilingi 11,000/ tigo. Ile pesa kwangu ilikata ila kwa mke wangu haikufika hadi leo. Niliwapigia tigo, walichonijibu ni kuwa mke wangu kapata salio ila ananidanganya. Kwa kweli ni bahati kwamba mke wangu tulikuwa wote pamoja hivyo simu yake nilikuwa nayo na hakuna salio liloingia. Niliwaza sana kwamba hivi ingekuwa mke wangu yuko mbali si ningesema ananidanganya na pengine tungegombana. Hadi leo hiyo pesa haijafika kwa wife wala kwangu haijafika.