Wateja wanapojiunga kwenye vifurushi mbalimabli huletewa taarifa immediately via SMS kwamba wamefanikiwa kujiunga lakini kifurushi kikiisha ama wateja huchelewa kutumiwa meseji ya taarifa au hawatumiwi kabisa. Hili tatizo huwakumba zaidi wale wateja wanaopenda kubaki na salio kubwa kwenye simu zao. Kwa mfano, mtu unanunua vocha ya Tsh 2000 kisha unanunua kifurushi cha Tsh 500 na kubakiwa na Tsh 1500 kwenye simu. Pindi kifurushi cha 500 kikiisha hutatumiwa ujumbe wowote hadi utapokuwa umekausha 1500 zilizosalia kwenye simu. Huu pia ni wizi wa mchana na unaofanywa kwa makusudi na kampuni za simu hapa nchini. Ninao ushahidi usiokuwa na mashaka katika huu wizi wa makusudi