JINSI JINIALIVYOLITESA PENZI LANGU; Eposide.13
Mzee John na mkewe waliingia ndani kisha kumfuata mtoto wao Lulu, mzee John hakuweza kujizuia chozi lilimdondoka hasa kutokana na mapenzi ya kweli kwa mwanae,alimpakata kisha kumbusu.Mzee John alianza kwa kuulizia kama
wavuvi wenzake walikuwa hai na ndipo alipopata habari za kuhuzunisha kwamba walikwisha fariki na matanga yao yamekwisha fanyanywa,kwa kweli ilimuuma sana akabaki kuwa ombea Mungu.Ule wasaha wa mzee John kuelezea nini
kilimpata ukafika ambapo alieleza yote aliyofanyiwa na kumshukuru mkewe kwa maombi yake kwa kipindi chote alipokuwa hatari.Kisha mongezi hayo mzee John alichomoa kibunda cha hela alichokuwa amepewa na mkewe na kamanda kisha kuanza kuzihesabu pamoja na mkewe,iliwachukua takribani saa moja kumaliza kuhesabu pesa ambazo
zilikuwa shilingi millioni mbili na nusu,loo! ilikuwa ni pesa kubwa kwao hivyo wakaamua kukarabati nyumba yao na kununua toyo(pikipiki).Naam zile risasi mbili zilimwingia mkewe na kamanda barabara na kumpeleka chini,alianza kulia na kuhangaika kwa mauvivu makali akijaribu kujiokoa pasipo matumaini Lakini ghafla alisikia milio ya king'ora nje ya nyumba
akajaribu kujikongoja mpaka dirishani na kuchungulia njeLo!walikuwa ni pollisi ambao walianza kuizingira nyumba huku wengine wakianza kuingia ndani,mkewe na kamanda akajivutavuta toka pale dirishani mpaka chumbani kwake.Akiwa ndani alisikia tangazo"yeyote aliyomo ndani ya nyumba hii ajisalimishe" kusikia vile mkewe na kamanda alichukua rundo la nguo na kujifunika ili kujificha.Polisi nao hawakuchelewa waliingia ndani na kukuta maiti ya kamanda na wale walinzi lakini baada ya kuangalia vizuri wakaona michirizi ya damu ikienda mbele wakaamua kuifuatilia
JINSI JINIALIVYOLITESA PENZI LANGU; Eposide.14
Walielekea kule damu ilikokuwa inatokea mpaka walipofika mbele ya mlango wa chumba cha mkewe na kamanda.Polisi walipeana ishara za kijeshi wakiwa na lengo la kujipa tahadhari hasa kwa kutojua ninini kilichopo ndani na ninani
aliyopo huku,polisi wawili waliingia kwa tahadhari huku bastola zao zikiwa mbele.Mkewe na kamanda aliendelea kutokwa na damu nyingi zilizotokana na majeraha ya risasi,akiwa bado chini ya nguo aliweza kuona polisi wakiingia na bastola zao,akajaribu kujipapasa na kuangalia kama anabastola lakini alikua ameisahau pale sebuleni,akaamua kusubiri
kitakacho tokea na kitokee,kisha polisi kuingia waliangalia kila kona kisha kuzirudia zile damu na kukuta zimeishia kwenye lundo kubwa la nguo,wakazipangua zile nguo haraka haraka na kukutana uso kwa uso na mke wa kamanda,wakamchukua mkukumkuku na kumpeleka kwenye gari la polisi hukuakiwa ndani ya pingu na kuambia kuwa
yeye ni muuaji,maneno yaliyoenda sanjari na kipigo.Polisi wengine walianza kuipekua nyumba nzima ya kamanda na kufanikiwa kukuta kilogram mia mbili za madawa ya kulevya,wakayachukua na kwenda nayo kituoni.Jalada la kesi lilifunguliwa kama kesi ya mauaji na ya kukitwa na madawa ya kulevya.Mawakili wa pande zote mbili waliendelea
kubishana kisheria.Kwa ujumla kesi ilikuwa imebalansi kiasi kwamba hukumu ilikuwa haitabiri .Hatimaye siku ya hukumu iliwadia mkewe na kamanda alipandishwa kizimbani chini ya ulinzi mkali wa askari polisi hukuwakizongwazongwa na waandishi wa habari waliotaka kupamba vyombo vyao vya habari.Punde si punde hakimu aliingia mahakamani ,watu
wote wakasimama kama ilivyo ada ya mahakamani,kisha hakimu kukalia kiti cha akaanza kutoa maelezo mafupi kuhusu ile kesi huku vifungu vya sheria vikitumika na sasa akaanza kutoa hukumu,watu ndani ya mahakama walitulia tuli kusubiri hiyo hukumu huku mawakili wa pande zote mbili wakionekana kutokuwa na wasiwasi huku kila mmoja akiamini upande wake utashinda*****
JINSI JINIALIVYOLITESA PENZI LANGU; Eposide.15
:Hazikupita dakika tano hakimu akasema"kwa mujibu wa sheria na kanuni zilizo wekwa mtuhumiwa anahukumiwa kifungo cha maisha na kazi ngumu" kisha kumaliza halpo askari liita "court!!!!"""" watu wakasimama hakimu akatoka nje .Mkewe na kamanda alitokwa na chozi mara baada ya hukumu hasa pale alipokumbuka kwamba maisha aliyokuwa
akiishi yalisababishwa na mumewe kamanda ambaye kamwe hakuwa chaguo lake la moyoni kwani wazazi wake ndio waliomlazimisha kuolewa nae hasa kutokana na tamaa ya pesa.Alikuwa ameshindwa kutoroka hasa kwa sababu
alitishwa kuuwawa endapo angejaribu kutoroka,aliwaza pia ni namna gani ataenda kuishi gerezani kwani hali ya maisha hayo alikuwa akiiona kwenye television.Polisi wakamchukua na kumuingiza garini tayari kuelekea gerezani kutumikia adhabu yake.Njiani mkewe kamanda alionena kuweka kichwa dirishani ili awezekuiona dunia kwa mara ya mwisho.Ni
miaka miwili sasa tangu mkewe na kamanda aanze kutumikia adhabu yake,umbo lake lilionekana kupungua na kuzoofu pia alikuwa mtu mwenye msongo wa mawazo.Mfungwa mmoja aliyekuwa rafiki yake alijaribu kumshauri kwamba ayakubali tu maisha hayo kwani ndio yaliyobaki na kuachana na mawazo,lakini ushauri huo ulikuwa kama upepo haya kupata hata chembe ya nafasi katika kichwa cha mkewe na kamanda chazaidi ni kwamba aliiendelea kujitenga na
wenzake.Mwaka mmoja baadae hali ya mkewe na kamanda ilizidi kuwa mbaya kwani sasa ikuwa hali tena chakula hivyo mkuu wa gereza akaagiza apelekwe hospitali.Alichukuliwa haraka haraka mpaka hospitali na mara baada ya kuwasili walipokelewa na daktari kisha mgonjwa kulazwa chini ya uangalizi mkali wa askari na ilipofika mjira ya saa nane usiku hali ya mgonjwa ili badilika *****
JINSI JINIALIVYOLITESA PENZI LANGU; Eposide.16
Daktari aliitwa haraka na kwenda,alipofika alimkuta mkewe na kamanda akikata roho,akamfunika shuka kisha kuwaambia wale askari waliokuwa karibu kisha akatoka kwenda kuandaa cheti cha kifo,baada ya kumaliza askari waliutwaa mwili wa marehemu na kwenda kuuzika.Miaka mitano ilikuwa imepitaa ambapo Lulu alikuwa mkubwa
kidogo,siku moja jioni mkewe na mzee John alimwita mwanae na kumuuliza"mwanangu ungependa kuja kuwa nani ukiwa mkubwa?","kuwa mwanasheria "Lulu aliendelea kwani ninapenda sana kuja kuwa mtetezi wa kinamama na watoto kwani mwalimu alitufundisha kuwa katika jamii zetu watoto na wanawake ndio watu wanaoonewa sana."sasa kazana sana na
masomo".Maneno hayo yalimfurahisha sana mkewe na mzee John kwa furaha alimkumbatia mwanae.Maisha yaliendelea kwa amani na furaha lakini kwa upande mwingine maisha ya pale kimara yakizidi kuwa magumu,hali iliyomfanya mzee John awe anachelewa kurudi nyumbani sababu ya kusubili wateja katika toyo yake.Jioni ilipofika mzee John alimwita mkewe na mwanae na kuwaambia kuna jambo anataka wazungumze******
JINSI JINIALIVYOLITESA PENZI LANGU
; Eposide.17
Kwakweli nimeamua kuwaiteni hapa ili kuwa fahamisheni kwamba "hali yangu ya kiafya inazorota''.kauli hiyo ilitoka kwasababu alikuwa amepatwa na uvimbe sehemu yake ya kulia ya tumbo lake,mkewe na mzee John alionekana
mnyonge na mwenye simanzi kubwa,na akajikuta akitamka"pole baba lulu tumwombe Mungu atatusaidia,maana sisi sote ni watoto wake na ipo siku utapona" kisha kusema hayo Mzee John aliiendelea na wewe mwanangu kipenzi cha
roho yangu kazana sana kusoma na hakikisha unaongoza darasani"sawaee""ndio baba" Lulu alijibu,mzee aliendelea, maana hiyo elimu ndio ukombozi wako,mimi na mama yako unavyotuona hapa hatukufanikiwa kusoma enzi zetu na ni
kwasababu wazazi wetu hawakuwa na uwezo wa kutulipia ada,ila wewe mwanetu umebahatika kusoma tumia nafasi hiyo ili uje uwe na maisha mazuri na ya raha, si umenielewa,"ndio baba" Lulu alijibu kwa ujasiri mkubwa kisha kumalizia"baba na mama kamwe sitawaangusha".Kadiri siku zilivyozidi kwenda ndivyo Lulu alivyozidi kukua na wakati
hali ya afya ya mzee John ilikuwa bado haieleweki yaani haijatengamaa na hivyo kupelekea yeye kulazwa katika hospitali ya Lugalo.Madaktari walimpokea na kumfanyia vipimo,vipimo vilipo kamilika familia ya mzee John ilitwa na daktari,baada ya mkewe na mzee John kuketi daktari aliwapa pole kisha kufungua karatasi ya majibu*******
Je nini kitatokea??? JINSI JINIALIVYOLITESA PENZI LANGU; Eposide18
Karatasi ya majibu ilionyesha kwamba mzee John alikuwa anaugua kansa ya tumbo ambayo ni ngumu sana kwa yeye kupona.Taarifa hii ya daktari ili wasononesha sana na kuwastua sana akina Lulu na mama yake,ambao macho yao
haya kusita kuonyesha hisia kwa kutoka machozi mithili ya mvua nyikani.Siku ile mkewe na mzee John pamoja na mwanae hawakuondoka pale hospitalini.Ilipofika majira ya saa moja usiku hali ya afya ya mzee John ilianza kutia matumaini walau kidogo kwani aliweza kuongea japo kwa shida shida,mzee John akamwita mkewe sanjari na mwanae
Lulu kisha kuwaambia"mke wangu nakuomba jitahidi sana umsomeshe mwanetu mpendwa,tunza zile mali zetu,wakati haya yote yakiendelea mkewe na mzee John alikuwa amejiinamia pembeni ya mumewe huku akibugujikwa na machozi, mzee John aliendelea "nawe mwanangu Lulu kazana kusoma na ushike sana elimu na usimwache aendezake maana huo
ndio ufunguo wako wa maisha" kisha kusema hayo aliomba apatiwe maji maana alijihisi kubanwa na kiu,mkewe aliinuka haraka haraka na kuchukua maji na kuanza kumnywesha,akiwa bado anaendelea kumnywesha maji akaona mzee John akishua pumzi kwa haraka na mara akaona maji aliyokuwa akimnywesha yakitoka mdomoni mithili ya udenda,akajiribu kumtikisa huku akiita "mzee John!!"mzee John!!!,hakuna sauti iliyotoa jibu,mkewe alianza kulia kwa sauti huku akimwita
daktari aje kumpa msaada.Mara baada ya daktari kuchukua vipimo kwa mzee John aliwageukia mkewe na John na mwanae,"kwakweli mzee hatunaye tena" kauli hiyo ilipokelewa kwa vilio vikali.Mwili wa marehu ulifunikwa na kuchukuliwa mpaka mochwari ambako ulihifadhiwa kusubiri taratibu za mazishi.Tarattibu za mazishi zilifanyika na mwili wa marehemu ulipata nyumba ya milele katika makaburi ya kinondoni.Wakati mzee John anafariki dunia Lulu alikuwa na umri upatao miaka saba.Kifo cha mzee John kilimpa majonzi mengi na simanzi kubwa mama lulu hali iliyopelekea afya
yake kudhoofu kutokana na msongo wa mawazo hali hiyo ilimpelekea kukosa nguvu na kumshawishi ajione mwenye mikosi na balaa tupu hapa duniani kisha kumlilia Mungu wake "kwanini mimi tu".Miaka ilizidi kusonga na hali ya mkewe na mzee John ilirejea katika hali yake ya kawaida hasa baada ya mawazo na kumbukumbu za kifo cha mumewe kuanza kupotea.Siku moja mkewe na mzee John alikuwa akitoka katika kazi yake ya kuuza mboga mboga za majani alijihisi kuumwa na kichwa lakini alifikiri kuwa hali hiyo ilisababishwa na jua kwani siku hiyo alishinda juani.Siku zilisogea hali ya
mkewe na mzee John ilizidi kubadilika na kuwa mbaya,hali ya iliyomlazimu Lulu kumwendea jirani yao ,bwana Masele na kuomba msaada.Taarifa ziliwafikia pia majirani wengine ambao walimchukua na kumpeleka hospitali.walipokuwa njiani mmoja wa majirani aligungua kitu****
JINSI JINIALIVYOLITESA PENZI LANGU; Eposide.19
Mwili wa mama Lulu ulikuwa umekauka na hakukuwa na dalili yeyote ya yeye kupumua,akawataarifu wenzake na mara baada ya kumwangalia vizuri waligundua kwamba alikuwa amekwisha fariki dunia.Lulu alishuhudia kifo hicho cha mama yake kipenzi,Lulu alilia sana tena kwa uchungu na majonzi mengi kwani tayari alikuwa ameuanza ukurasa mpya wa
kukosa mapenzi na malezi ya baba na mama yaani ukurasa wa uyatima,alikumbuka maisha aliyoishi na mama yake huku akibugujikwa na machozi tele.Taratibu za mazishi zilifanyika na ndugu wa Lulu waliwasili pale kimara na hatimaye mazishi yalifanyika katika makaburi ya kinondoni,mahali pale pale alipozikwa mzee John .Baada ya mazishi kumalizika
wanandugu wa Lulu walikaa kikao na kuamua kwa pamoja kwamba mjomba ake na Lulu ndiye atakae mlea Lulu mpaka atakapofikisha umri wa kujitegemea.Wakati mama yake na Lulu anafariki dunia Lulu alikuwa akisubiri matokeo yake hasa mara baada ya kuhitimu darasa la saba.Hivyo Lulu alilazimika kuhamia Mbagala kwa mjomba ake,ambako alienda
kujiunga na kidato cha kwanza katika shule ya sekondari ya jitegemee.Lulu alipokelewa vizuri katika familia ile ya mjombaake na maisha yalikuwa mazuri kwani alipewa mahitaji yote aliyoyahitaji.Alipendwa sana na shangazi yake na kila siku alimsisitizia kusoma kwa bidii.Lulu alionyesha kusikia na kushika vizuri yaleyote aliyoambiwa kwani kila mtihani alikuwa anakuwa wa kwanza darasani hali iliyompelekea kupendwa na kila mtu si wanafunzi wenzake tu bali hata
walimu wake.Lulu aliendelea kujituma zaidi ili aweze kufaulu mitihani yake,pamoja na hayo yote alikutana na Seleman ambaye alikuwa classment wake katika shule ya sekondari jitegemee,walishirikiana vizuri sana katika masomo yao hivyo kuweka ushindani mkubwa sana katika nafasi ya kwanza na ya pili darasani mwao.Siku moja Lulu na Seleman walichaguliwa kwenda kuiwakilisha shule yao katika mashindano ya 'debate' ambapo shule zote za Tanzania zilihudhuria kupitia wawakilishi wao,ambapo katika mashindano hayo kulitokea kitu cha kushangaza**********
JINSI JINIALIVYOLITESA PENZI LANGU; Eposide.20
Wanafunzi wa shule moja waliongoza katika mashindano yale ya debate na hawa si wengine bali ni Lulu na Seleman kutoka shule ya sekondari Jitegemee.Katika mashindano hayo Lulu na Seleman waliweza kuelezea vizuri sana namna
ukosefu wa demokrasia katika nchi unavyoweza kuchangia kudidimiza maendeleo ya nchi.,kutokana na maelezo yao bora walizawadiwa computer moja kila mmoja.Jambo hilo lilikuwa la furaha sana kwao hivyo walipongezwa na wote waliohudhuria ile debate na wao pia walipongezana.Haya yote yaliendelea kuwatia moyo na kuwapa ari na hamasa
kubwa ya kufanya vizuri zaidi katika masomo yao.Maisha yao ya shule yalikuwa ya kuigwa kwani kila mwanafunzi darasani mwao alipenda kwenda kuuliza maswali pamoja na kuomba ushauri wa kimasomo kwa Seleman na Lulu na hii ilikuwa kwasababu tu walikuwa na uwezo mzurri wa kimasomo.Hali haikuishia hapo waliendelea kupendwa na walimu
wao kwani siku moja wakiwa darasani wanafunzi wenzao walipanga kumpiga mawe mwalimu wao wa kiingereza sambamba na kuchoma moto nyumba yake kisa alikuwa haingii darasani kufundisha na ifikapo mwisho wa muhula huingia na kutoa mtihani ,wakiwa katikati ya mazungumzo yao Lulu na Seleman walishauriana namna ya kutuliza jazba
ile na hatimaye kutoa wazo la kumuita mwalimu husika na kumweleza shida yao na kumtaka awe anahudhuria vipindi.Uamuzi huo ulipokelewa na wanafunzi wote ambao walimwita mwalimu na kumweleza yote ,naye mwalimu alikiri akisema "nisameheni wanafunzi nitabadilika" na hii ilisababisha amani kutawala tena pale shuleni kwao.Miaka nayo ilizidi
kwenda kadhalika pia siku nazo zilikuwa hazigandi Lulu na Seleman walimatiza kidato cha nne.Muda wa matokeo kutoka uliwadia ambapo shule ya sekondari Jitegemee ili faulisha wanafunzi wote kwa kiwango cha daraja la kwanza na la pili,kwa upande wao Lulu na Seleman walipata daraja la kwwanza yaani "division one" na ilikuwa ni bahati sana kwao
kwani walichaguliwa kujiunga kidato cha tano katika shule moja.Maisha ya "high level" yalikwenda salama na hatimaye siku iliyokuwa ikingojewa iliwadia ambapo Lulu na Seleman walifika ukingoni mwa elimu yao ya sekondari yaani kidato cha sita.Siku ya mahafali yao iliwadia huku kila mmoja akiipokea kwa hamu kubwa na katika hali isiyotegemewa Selemani aliona kitu******
JINSI JINIALIVYOLITESA PENZI LANGU; Eposide.21
Alikuwa ni Lulu ambaye alionekana kutokuwa na furaha yoyote ile na hii ilijidhihirisha wazi moja kwa moja toka usoni kwake hali iliyomfanya Sele kumkaribia na kumuuliza "kulikoni rafiki yangu?""niko sawa tu,kwani unaonaje,aliuliza Lulu."niambie ukweli kwani unaonyesha wazi kwamba hauko sawa, tafadhali niambie,Sele alisisitiza.Akiwa anajiweka
sawa kwa kuelezea yote yanayo msibu alijikuta akitokwa na machozi mengi ,Sele alijaribu kumtuliza.Lulu aliongea kwa kwikwi "nawakumbu.......ka......wa.....za.....zi,alishindwa kuendelea kuzungumza huku kilio cha kwiki nacho kilimbana.Baada ya kutulia kidogo aliendelea"unajua Sele natamani sana kama wazazi wangu wangekuwepo katika
mahafali haya,ningefurahi sana tena mno""usijali sahau hayo maana hiyo ni kazi ya Mungu na haina makosa ,acha basi kuwa mnyonge tusherekee vizuri,alisema Sele.Kwa shingo upande Lulu alikubali kuendelea na maandalizi ya mahafali yao.Muda wa mahafali uliwadia ,wageni nao walikuwa wamesha wasili,kwa bwembwe nyingi na shamra shamra sana
wahitumu waliingia ndani ya ukumbi ulio pambwa vizuri na ukapambika haswa,punde si punde kelele zililindima ukumbini «««happy day,happy day»»»».Wazazi wa Selemani waliwasili ukumbini huku wakiwa wamekumbatia zawadi nyingi bila
shaka zilikuwa kwa ajili ya mwanao , naye mjomba ake na Lulu sanjari na mkewe walikuwepo ukumbini.Burudani ziliendelea huku watu wakiserebuka na kula na kunywa.Wakati hayo yote yakiendelea Lulu alimwita Sele na kumnong'oneza kitu********* (Mwisho)******************************