Jinsi hacking ilivyonipa 250,000 tshs leo!!!!!!!!!

Jinsi hacking ilivyonipa 250,000 tshs leo!!!!!!!!!

Singida ndio home

JF-Expert Member
Joined
Feb 23, 2012
Posts
3,188
Reaction score
3,377
Ni majuzi juzi tu nlianzisha thread kwamba inabidi tanzania tujiupgade kwenye techs kwa njia ya kuhack, well nkapost topic inayohusu site ndogo tu nliyohack hata sekunde kumi hazijapita thread ikafutwa , nkakaa mezani nkafikiria hivi nikipata loopholes kwenye site za tz na nkienda kuziripoti itakua dili , mzee mzima nkaingia mzigoni na brand new kali linux nkaanza kusearch loopholes na kujaribu kuziexploit nikazinotedown fasta fast nkang'oka mbio kwenda ofisi husika ya shirika nliloweza kupata matundu, mwanzoni nmefika pale secretary ndo kwanza hata hajui maana ya kuhack bahat nzuri mkubwa flan akasikia then akanifata nlienda na laptop yangu na nkamwonyesha jinsi itavyokuwa wasipoziba sio siri alikua surprised akapiga simu kwa kijana wake wa i.t akaja mbio kuhakiki maana alikua ni mbishi mno kafika pale nae anatoa macho tu ndo kwanza hata kali haijui well tukafix mambo palepale nkapelekwa ofisi zao za uhasibu chap chap nkapewa kitita cha laki 2 nae jamaa wa i.t akaniita palepale akanipa 50 jumla ikawa 250 k na kiukweli nilifurahi sana maana nimefumbuliwa macho kuwa kipaji changu cha kuhack kinaweza kuwa bonge la dili
 
Kwenye heading ibadilishe 250,oo tshs iwe 250,000 tshs
 
Safi sana. Tumieni akili zenu kujipatia ajira. Itasaidia taasisi nyingi hasa za serikali.
 
...naomba nikupe account yangu yoyote then ui hack, na tukubaliane, ukishindwa u must me, na ukishinda i will pay u, muda nao utahusika
 
...naomba nikupe account yangu yoyote then ui hack, na tukubaliane, ukishindwa u must me, na ukishinda i will pay u, muda nao utahusika

namruhusu pia a hack site yangu
www.joenyandigira.com aweke chochote anachotaka ili niamini. nampa mwezi iyo homework. akiweza anidai laki
 
Na siku zote script kiddie ndo hutoka kifua mbele na kujisifia, hacker hana mda huo

Tofauti kati ya hacker na huyo script kiddie ni nini mdau...??
Afu nilishawai sikia kitu inaitwa black hacker na white hacker...vipi kuhusu hawa watu..??
 
Tofauti kati ya hacker na huyo script kiddie ni nini mdau...??
Afu nilishawai sikia kitu inaitwa black hacker na white hacker...vipi kuhusu hawa watu..??
Script kiddie ni watu ambao kiuwezo hawajawa ma-programmer wa kuweza kutengeneza software zao wenyewe kwa ajili ya hacking, ila wao hutegemea sana software kutoka kwa proffesional programmer wanaotengeneza software kwa ajili ya hacking, mfano wanaweza wakatengeneza software fulani kwa ajili ya kupiga simu pasipo malipo, wewe ambaye hujahusika kutengeneza unaweza ukaitumia kukwepa kulipia gharama za simu, kumbuka hapa wewe utakuwa hacker lakini utaitwa script kiddie hacker kwa sababu huelewi hiyo software imetengenezwaje (program codes) zaidi ya kuitumia
Mkuu ukiachana na hawa wanaojiita black hacker na white hacker, wapo wanaojiita kwa majina yao mengi tu na kila mmoja ana lengo lake, hawa wanaojiita back hacker (black hat) wao kazi yao kubwa ni kuharibu security system kwa manufaa yao wanayoyajua wao pindi wanapotaka kufanya hacking i.e wanapofanya hacking kwako mwisho wanataka wafaidike na nini!?. Na mara nyingi hawa ndio crackers
Kuhusu white hacker (white hat) hawa wao huwa wanafanya hacking ya security system kwa ajili ya kupima uwezo wa hiyo security system, mfano unaweza kutengeneza software yako yenye security system ili kuilinda watu fulani wasiweze ku-access vitu fulani pasipo na ruhusa yako, sasa ili kupima uwezo wa hiyo security yako unawaita hao jamaa ili waweze kuifanyia hacking ili uweze kujua mapungufu ya security system yako, hii mara nyingi huwa inaitwa ethical hacking
Niishie hapa ila kama kutakuwa na wadau wengine wataongezea wanachojua wao
 
SIKILIZA KWA MAKINI KABLA HUJAKUTWA YA KUKUKUTA;....

kwanza scanning a site without owner consent is illegal.... kwa sababu inafall under unathorized access (The access without right to a computer system or network by infringing security measures).... nadhani ipo kwenye sheria zetu YA ELECTRONIC kama cjakosea na pia kwenye international convention on cyber crime ambayo tanzania imeridhia..... unaweza jiuliza si natafuta vulnerabilities/exploit kwa nia njema lakini nataka nikwambie sometimes scanning a site using automated tools inaweza ikasababisha site kucrash au kuanza unexpected behaviour hivyo kumsababishia hasara mwenye site...,

kwa jinsi ulivyosema inaonyesha unatumia automated way of looking for exploits which is sometime unfriendly to the site and leaves massive of prints which can incriminate you kama hujamask properly your i.p, hivyo kitaalamu ungetumia manual ways of looking for exploits because even though its time consuming but its effective and reliable......

Nakushauri next tym ukifanya hiko kitu, jaribu zungumza na wahusika kwanza otherwise ukiwakuta waelewa unaweza jikuta in trouble.... ndo maana nchi nyingi zilizoendelea, its a criminal offence scanning a site without owner consent.....

hali kadhalika nakushauri utumie msemo unaotumiwa na wadau wa backtrack kuwa THE QUIETER YOU BECOME, THE MORE YOU CAN HEAR.... Usipende sana hii habari ya kusanua kila kitu....

YANI JITAHIDI USIWE KAMA baadhi ya MAPRODUCER WETU WA MUZIKI WA BONGO AMBAO WANAWEZA PIGA KINANDA NA GITAA ZA FRUITY LOOPS, UKIMPA APIGE VYOMBO LIVE ANAANZA OOOH SIJAMASTER OOOH SIKUJIAANDAA....
WE ULIWEKA KALI LINUX IKUFANYIE KILA KITU, LAKINI U HAVE NO IDEA WHATS HAPPENING ON THE OTHER SIDE....

PIA HACKING SIYO KIPAJI....
 
Ni majuzi juzi tu nlianzisha thread kwamba inabidi tanzania tujiupgade kwenye techs kwa njia ya kuhack, well nkapost topic inayohusu site ndogo tu nliyohack hata sekunde kumi hazijapita thread ikafutwa , nkakaa mezani nkafikiria hivi nikipata loopholes kwenye site za tz na nkienda kuziripoti itakua dili , mzee mzima nkaingia mzigoni na brand new kali linux nkaanza kusearch loopholes na kujaribu kuziexploit nikazinotedown fasta fast nkang'oka mbio kwenda ofisi husika ya shirika nliloweza kupata matundu, mwanzoni nmefika pale secretary ndo kwanza hata hajui maana ya kuhack bahat nzuri mkubwa flan akasikia then akanifata nlienda na laptop yangu na nkamwonyesha jinsi itavyokuwa wasipoziba sio siri alikua surprised akapiga simu kwa kijana wake wa i.t akaja mbio kuhakiki maana alikua ni mbishi mno kafika pale nae anatoa macho tu ndo kwanza hata kali haijui well tukafix mambo palepale nkapelekwa ofisi zao za uhasibu chap chap nkapewa kitita cha laki 2 nae jamaa wa i.t akaniita palepale akanipa 50 jumla ikawa 250 k na kiukweli nilifurahi sana maana nimefumbuliwa macho kuwa kipaji changu cha kuhack kinaweza kuwa bonge la dili

This is how it should work. Alert the owners of the website with vulnerabilities so they could fix it.
 
shiny c, kwanza hongera kwa kuwa bonge la Exaggerator! jana ulikuwa unajidai kwamba ohh, nimepost saa nane za usiku website niliyo hack, ukaweka na link yake, the cricket archive... i checked the site and yes ilikuwa vulnerable to injections through forms, uliendelea kujinadi tena kwnye thread yako tz tuanze hacking jamaan kuhusu hyo website uliohack, nikakuuliza swali, ambalo naona umelikimbia, na nitaliuliza tena, just because hyo site iko vulnerable to injections ndo umeihack? maana nafahamu kuwa kwenye google ukisearch inurl:search.cgi, nyingi huwa ni vulnerable, ss hii site umeihack vp?

6cbd.png
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom