Jinsi gani ya kuzuia fungus na weusi kwenye pavement?

abudist

JF-Expert Member
Oct 25, 2009
850
780
Wadau naomba kujua tatizo linalofanya weusi kama fungus kwenye patio na jinsi ya kutatua tatizo hilo kwenye hizo pavement. Tafadhalini naomba ushauri kama kuna fundi pia wa kazi hiyo.

WhatsApp Image 2020-07-10 at 18.04.34.jpeg
 
fumua hizo paving, weka mchanga, fanya levelling hakikisha maji yapate uelekeo, (weka kapeti juu ya mchanga Kama utaweza) panga pavement hakikisha huachi uwazi mkubwa kwenye joint, tia mchanga juu the Re-compact halafu safisha mchanga juu ya pavement!

Miongoni mwa sababu zinazosababisha fangasi, nikutoweka mchanga wa kutosha chini kabla ya pavement kupangwa, pia ni kutoyapa uelekeo maji yatokanayo ardhini! Pia zingatia usafi wa Mara kwa Mara usirundike uchafu au kitu chochote kinachotoa umande juu ya pavement !
Mwisho! Funga gata kwenye bati lako ili kupunguza kiwango Cha maji yanavyotoka kwenye bati kutuama juu ya pavement ambapo chini kumbuka Kuna kapeti Jambo ambalo hupelekea unyevu unyevu fangas
 
Hapo inaonyesha kabisa weusi unasababishwa na kutuama kwa maji....Je angalia source ya maji ni chini au kutoka juu unyevu wa bati unaodondoka? Kama ni Juu weka gata au kama chini fumua peving uweke nylon.
 
Back
Top Bottom