kaka maybe huelewi maana ya root.
unaposema root kiswahili ni mzizi na kwenye simu root ni mahali mafolder yanapoanzia.
kwenye android huwa mtu unaruhusiwa kufungua folder moja tu linaitwa sdcard mafolder mengine hayaonekani kama vile folder la system na data. hivyo mtu anaroot ili apate access ya hayo mafolder na kuweza kumodify kadri anavyotaka mwenyewe.
simu za zamani kama blackberry na symbian unaweza ku access folder zote hadi za system kwa kuinstall file manager tu kama xplore ukayaona hayo mafolder. hivyo hazihitaji kuroot. sasa wewe ukisema unataka kuroot bb wakati tayari ipo open ni kama mlango upo wazi halafu unatafuta jiwe uvunje mlango ili uingie ndani.