kidaganda
JF-Expert Member
- Aug 26, 2013
- 2,999
- 2,582
Miaka mingi watu wamelia sana Kwa kuumizwa na watu wao wa karibu(marafiki).
Sio mbaya tukashare yalitukuta Mtu uliyedhani ni rafiki yako siri yako yake, siri yake yako,shida yake yako ya kwake yako.
Binafsi nakumbuka miaka kama mitatu minne imepita nilikuwa na kidada kimoja cha chuo Fulani maarufu tu hapo DAR,nilikipenda hiki kidada maana nilitamani kukioa nikamua kumtambulisha Kwa rafiki yangu mpendwa.
Siku ya utambulisho tulikaa kwenye moja ya hotel maarufu tu Mwanza,nilivyomwagia sifa rafiki yangu sikujua kama angegeuka nyoka.Baada ya utambulisho tulikuwa tukikutana sehemu mbalimbali Mimi nikiwa na mtarajiwa wangu na jamaa yangu wakati mwingi akiwa peke yake.
Baada ya miezi michache kupita na binti kurudi chuo mawasiliano yalipungua sana Mimi na binti,ikabidi nimweke kitako na ndipo alipoanza kuniambia Ohh mliniona Mimi Malaya sana baada ya kunitumia ukachoka ukamtuma na rafiki yako Fulani.
Kiukweli niliumia Sana maana niliona hadi text alizokuwa anamtumia na nyingi za kunipondea.
Hadi muda huu naandika Uzi huu Yule mdada sijui hata yuko wapi alikata mawasiliano na Mimi.
Kuhusu huyu rafiki sikuwahi mwambia chochote nilishampuuza tu na unafiki wake.