Jinsi engine ya gari inavyofanya compesation iwapo nguvu ya gari inazalishwa kidogo

JituMirabaMinne

JF-Expert Member
May 4, 2020
1,321
2,000
images.pngGari ina namna moja tu ya kufidia endapo nguvu itazalishwa kidogo, ambayo ni kuongeza kiasi cha mafuta.

Engine ya gari ili iweze kuzalisha nguvu iliyokusudiwa ni lazima kuwe na mafuta, Cheche pamoja na hewa. Kila kimoja hapo kinatakiwa kuja katika hesabu ambayo kimepigiwa. Kukiwa na upungufu au ongezeko ni matatizo.

Mfano mafuta yakija mengi yanaweza kulowesha spark plug na kuzifanya zisichome vizuri wakati yakija machache mlipuko utakuwa mdogo na case zote mbili zitazalisha nguvu ndogo na gari yako inaweza kukosa nguvu.

Hewa ikija nyingi sababu ya kupasuka au kuchomoka kwa moja wapo ya pipe au MAF sensor kutoa hesabu mbaya basi gari inaweza ikagoma kuwaka kabisa au ikawaka na misi juu au ikawaka ikazima. Na hewa ikiwa kidogo kitakachotokea ni kama tu ambacho kinatokea mafuta yanapokuwa mengi. Nimeelezea hapo juu.

Cheche zikiwa hazina nguvu inaweza kupelekea mlipuko kuwa mdogo na engine kukosa nguvu wakati cheche zikiwa zikiwa na nguvu kubwa inaweza kupelekea pre ignition yaani mafuta yatakuwa yanaungua muda wote hata kama spark plug haijatoa cheche sababu ndani ya engine joto ni kali sana.

Kikawaida ratio ya hewa na mafuta kwa engine ya petrol huwa ni 14.7 kwa 1 wakati kwa engine ya diesel huwa ni 14.5 kwa 1. Hizo ratio huwa zinaweza kupanda juu kidogo yaani Lean au kushuka chini kidogo yaani Rich. Lakini ratio ikishaanza kufika 17 kwa 1 hapa kuna shida. Au ikishaanza kushuka na kufika 12 kwa moja hapa pia kuna shida kubwa.

Sasa kwa mfano nikizunguzmzia engine ya petrol ambayo air fuel ratio yake ambayo ni standard ni 14.7 kwa 1 kama ikitokea hii ratio ikapanda sana au kushuka sana, control unit huwa inafidia ili hiyo ratio irudi mahali pake. Na namna pekee ya kufidia huwa ni kuongeza mafuta au kupunguza mafuta. Na mara nyingi huwa ni kuongeza mafuta yanayokuja kwenye engine.

Yaani katika vitu vitatu pale ambavyo nmetaja kwamba vinaingia kwenye engine. Cheche na hewa huwa zinakuja kwa kiwango ambacho ni constant ila mafuta ndio huwa yanaongezwa au kupunguzwa kulingana na nguvu inayozalishwa.

Na mafuta hayaongezwi kwa kuongeza speed ya pump hapana. Mafuta huongezwa kwa kuziacha nozzle zikae wazi muda mrefu kabla ya kufunga. Hivyo kama nozzle zako unaona zinatema sana acha kuzihukumu moja kwa moja sababu muda mwingine kuna matatizo mengine ambayo yanaweza kupelekea zifanye hivyo lakini yakirekebishwa zinarudi kawaida.

Uzuri ni kwamba kama mafuta yanaenda mengi, ukipima huwa inaonesha. Oxygen sensor lazima zitoe taarifa.
 
Boeing 747

JF-Expert Member
Mar 30, 2018
3,139
2,000
View attachment 1807753

Gari ina namna moja tu ya kufidia endapo nguvu itazalishwa kidogo, ambayo ni kuongeza kiasi cha mafuta.

Asante kwa somo zuri

Sent from my itel P51 using JamiiForums mobile app
 
Msingida

JF-Expert Member
Dec 1, 2010
7,884
2,000
Huwa narudia mara nyingi kuisoma hii mada.
Nilikuwa na Pajero Jr ilikuwa na tatizo la mis sana,mara fundi aguse plugs,mara sensor,mara kwenye throto,wala hakuwa anaweza kutatua tatizo zaidi ya kubahatisha.
Japo niliiuza hakuna rangi niliacha kuiona.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom