Jinsi dunia inavyoweza kukutana na mwisho wake

vivaforever

Senior Member
May 30, 2016
113
162
1) Vita ya Nyuklia (Nuclear Armagedon)

Bomu moja la Nyuklia lina uwezo wa kusababisha kifo kwa asilimia 80 hadi 95 kutoka eneo lililoripuliwa kuelekea umbali wa kipenyo cha Km 4 ingawa uharibifu mkubwa unaweza fika mbali zaidi.

Ingawa watu wanahofia sana kifo kutokana na mlipuko wa mabomu haya lakini tunachotakiwa kuhofia zaidi ni Msimu wa Baridi wa Nyuklia ( Nuclear winter ). Hii ni pale wingu la vumbi zito na moshi unaotokana na hii milipuko kufunika anga la Dunia hivyo kuzuia miale ya jua kufika Duniani. Mimea itakufa, wanyama watakufa... baridi litakuwa kali sana maana joto litadondoka chini ya 0°C, vurugu zitasambaa kwa wale wachache watakaobakia wakigombania mahitaji machache yatakayokuwa yamebakia. Wengine watakufa kutokana na kudhuriwa (watapata Kansa za ajabu) na mionzi yenye sumu ya Nyuklia kutoka kwenye hayo mabomu au vinu vya Nyuklia vitakavyo ripuka.

Marekani na Urusi pekee wana zaidi ya vichwa 7000 vya nyuklia.. ikitokea vichwa 4000 tuu vimetumika kwenye hii vita basi Dunia ndo kwisha habari yake. Nchi nyinginezo zenye mabomu ya nyuklia ni kama vile India, Pakistan, Korea Kaskazini, Uingereza, Ufaransa n.k.

2) Silaha za Kibaiolojia & Kikemikali ( Biological and chemical warfare ).

Tofauti na siraha za Nyuklia ambazo ni ghali sana na ngumu kuzitengeneza pia huaribu majengo, kuua mimea, wanyama kiufupi huaribu chochote kilicho mbele yake... siraha za kibaiolojia & kikemikali huweza kutengenezwa kwa gharama ndogo sana ndani ya Maabara kwa kutumia malighafi ambazo ni rahisi sana kuzipata.

Ndani ya miongo michache tumeshuhudia matumizi ya vimelea hatari kama vile Kimeta vikitumiwa kufanya mashambulizi ya kibaiolojia pia gesi na kemikali zenye sumu kama vile Sarin ambazo hutumika sana vitani.

Jee! Hatari iko wapi..??
Ukitaka kujua hatari ilipo basi fikiria kuhusu Virusi vya Corona vya mwaka 2019 (SARS - nCOV - 2019) ambavyo vimeitesa na Dunia kwa mwaka mmoja uliopita. Kama virusi hatari vikibadirishwa maabara kuvifanya viwe hatari zaidi (Mfano: Ebola Virus, Measles Virus) halafu visambae kama vya Corona... vifo vingekuwa vingi sana na Dunia ingesimama kwa miongo kadhaa.
Kuhusu hizi gesi za Sumu & Kemikali kama zikiwa zimeachiwa kwenye Vyanzo vya maji (Mfano; Bahari) au Hewa... basi ingesambaa haraka sana mwishowe Dunia isingekalika na viumbe hai vingekufa ovyo.

3) Mabadiriko ya Tabia ya Nchi. (Climate change)

Mnalionaje jua la Bongo huko..?? liendelee kuteremka au tupunzike kidogo..??

Umoja wa mataifa kupitia Jopo la wanasayansi wake wametoa tahadhari kuwa tuna miaka 12 tuu ili kurudisha Joto la Dunia katika kiwango sahihi (Optimum levels).

Mwendelezo wa mabadiriko ya tabia ya Nchi hutegemeana na jinsi Dunia inavyozidi kuchemka (warming) kutokana na kuongezeka kwa Joto.

Jee! Hatari iko wapi..?
○ Vimbunga vya Kitropiki vinavyoangamiza. Hivi mara nyingi hutokana na mabadiriko ya mgandamizo wa hewa na joto huchangia kwa kiasi kikubwa katika kuleta mvurugiko huo.
○ Kuzama kwa Majiji makuu. Mfano; Florida, Bangladesh, Dar-Es-Salaam hii ni kutokana na kuongezeka kwa Maji ndani ya Bahari (kumbuka: Kama bara lote la Antarctica ambalo limefunikwa na theluji tupu likiyeyuka basi sehemu kubwa sana ya Ardhi ya Dunia itazama chini ya Maji).
○ Kutanuka kwa Majangwa.

Hali hii itasababisha uhaba mkubwa wa chakula, watu kukosa makazi na magonjwa ya mlipuko yasiyoelezeka.

4) Kuanguka kwa mfumo wa Ikolojia (Ecological collapse).

Mfumo wa ikolojia ni mwepesi sana na hujumuisha jamii ya viumbe hai mbalimbali wanaoingiliana na mazingira yao ya asili (yasiyo hai) kama vile Maji, Hewa na Ardhi. Mfumo wa ikolojia huweza kupona kutoka kwenye uharibifu unaofanywa na Binadamu kama vile kuongezeka kwa Joto, uharibifu wa makazi ya viumbe hai n.k (angalia jinsi misitu inavyochipuka tena baada ya kukatwa) lakini kuna hatua flani ikifika haiwezi kupona tena na kutokana na ripoti mbalimbali za kisayansi ni kuwa tumefikia hatua hiyo.

Mfano mzuri ni Ziwa Chad lililopo Afrika Magharibi. Miaka 60 ya ukame na matumizi holela ya maji ya ziwa hilo imesababisha ziwa lipungue maji yake kwa Lake Chad in West Africa is an 90% kiasi kwamba viumbe hai na watu takribani milioni 40 kutoka Nchi za Chad, Nigeria, Niger na Cameroom wanaotegemea hilo ziwa wakiwa hatarini.

Wanasayansi wanaamini kwamba hiki kipindi katika Historia kinaunda wakati maalumu unaojulikana kama Anthropocene Era (Zama za Anthropocene). Katika zama hizi, Binadamu ndio waharibifu wakuu huku wakiwa wanaharibu kile kinachoifabya hii sayari iwe ya kukalika.

Jee! Hatari iko wapi..??
○Mimea na Wanyama mbalimbali wataendelea kuadimika na mwishowe kutoweka (from Endangered to Extinct). Lakini miongoni mwa viumbe hao ndio tunawategemea sana ili tuweze kuishi, Mfano: Nyuki, kama wakitoweka basi Dunia itaanza kufa taratibu.

5) Magonjwa ya kusambaa Dunia nzima. (Pandemics).

Wakati tukiwa tunalia na Corona, hebu tujikumbushe kuhusu Tauni (Plague), mara mbili katika Historia tauni ilienea Duniani huku ikiua kadirio la 15% ya watu wote Duniani miongo michache iliyopita. Ilitokea katika karne ya 14 na 15.

Kwa bahati sana ni kuwa haya magonjwa yenye uwezo wa kusambaa Dunia nzima ni adimu sana, lakini yanatokea. Karne moja iliyopita Mafua ya Uhispania (Spanish Flu) yaliua zaidi ya watu milioni 50 huku mlipuko wa Ebola na mafua ya SARS hivi karibuni ikiwa kama ukumbusho kwetu.

Jee! Hatari iko wapi..??
○ Usugu wa vimelea. Vimelea vingi vimekuwa sugu kiasi zile dawa zinazotumiwaga kuwaangamiza (Mfano; Antibiotics) hazina uwezo wa kufanya hivyo tena.
○ Kukosekana kwa Kinga na tiba dhidi ya Vimelea sugu. Baadhi ya magonjwa hayana tiba wala kinga, mfano; Ebola. Kama yatasambaa Dunia nzima basi vifo vitakuwa vingi sana.

6) Dunia kupigwa na Kimondo (Asteroid impact).

Vimondo ni mawe makubwa yanayoelea angani huku yakiwa yanalizunguka Jua. Ni mara chache sana haya mawe hugongana na Dunia kama vile ilivyotokea miaka mingi iliyopita na kusababisha kutoweka kwa viumbe aina ya Dinosaurs. Kama kimondo chenye ukubwa wa 1/10 ya ukubwa wa kimondo kilichoipiga Dunia na kusababisha kuangamia kwa Dinosaurs kikiipiga Dunia leo hii basi matokeo yake yatakuwa ni ya kuogofya.

Inaaminika kuwa kitatoa shock kubwa sana kiasi majengo yote yataporomoka, milipuko itaikumba Dunia nzima na Moshi mzito utatanda anga la Dunia kuzuia miale ya Jua kufika ardhini., Dunia itakuwa kama imepigwa na Vita ya Nyuklia.

7) (Mlipuko wa Volkano kuu) Supervolcanic eruption

Volkano kuu iliyoripuka miaka 74,000 iliyopita ilitoa kifusi kikubwa kilichoifunika Dunia kiasi kwamba wanasayansi wanaamini kilisababisha Dunia ipoe na kuwa na baridi kali kutokana na kukosa miale ya Jua. Hali hii ilipelekea kupotea kwa mimea na wanyama wa aina mbalimbali (great Mass extinction).

Jee! Hilo linaweza kutokea leo..?? Ni ngumu sana kusema kwa sababu hatuna data za kutosha lakini kwa kiasi flani zinaonyesha kuwa hii hali hutokea kila baada ya miaka 17,000... na kama ni hivyo basi tumepitiliza maana mara ya mwisho Volkano kuu kuripuka ni miaka 26,500 iliyopita huko New Zealand.

Hatuna njia za kugundua kuwa mripuko unakuja isipokuwa baada ya wiki au miezi kadhaa, na pia hatuna njia yoyote ya kuzuia hilo lisitokee, wanasayansi wanayachunguza kwa ukaribu maeneo machache ambayo ni hatarishi na huwenda Volkano kuu ikaanza kuripukia hapo.. mfano: eneo la Yellowstone huko Marekani.

8) Solar geoengineering

Kuna njia nyingi za kuzuia joto la Dunia lisipande lakini huja na hatari zake.

Solar geoengineering hii njia huakisi mwanga na joto la jua lisifikie Duniani na lipotelee kwenye Anga, hii hufanyika kwa kuweka "Aerosols" katika Stratosphere (tabaka la Pili la angahewa kutoka Ardhini). Kwa sasa hii Teknolojia ipo kwenye Models tuu (bado haijafanyika) lakini Wanasayansi wa Havard wana mpango wa kuanza kuifanyia majaribio.

Jee! Hatari yake ni ipi..??
Solar geoengineering ni moja kati ya Teknolojia mbili zinazochipuka ambazo zinaweza rekebisha anga hewa na kupunguza wingi wa hewa ya Ukaa (Carbondioxide), Teknolojia nyingine ni ile ya kuondoa hewa ya Ukaa moja kwa moja kutoka kwenye angahewa ingawa hii Teknolojia haiwezi ondoa hiyo hewa kwa uwingi. Sasa hii teknolojia ya Solar Geoengineering hatujui madhara yake yatakuwa ni yapi, huenda itavuruga mfumo wa ikolojia katika eneo maalumu au Dunia nzima na hapo ndipo tatizo lilipo... hii itaathiri Binadamu kwa kiwango kikubwa kwa kuanguka kwa mfumo wa Ikolojia.

9) Akili ya kubuni (Artificial intelligence).

Akili ya kubuni "Artificial intelligence (AI)" inaendelea kukua kwa haraka kila uchwao ambapo tunaona maroboti yenye uwezo wa kutenda kazi na kubuni vitu kwa ufanisi mkubwa kuliko Binadamu yakivumbuliwa kila siku. Wanasayansi wanakadiria kuwa ifikapo 2050 hawa Maroboti (au A.I) watakuwa na uwezo wa kutenda kwa ufanisi kwa 50% kuliko Binadamu wa kawaida... na miaka michache mbeleni watakuwa wamewapita Binadamu katika ufanisi wa kutenda kazi.

Tatizo liko wapi...??
Shida ni kuwa Wanasayansi wanaamini uwezo huo mkubwa wa kutenda kazi na kubuni vitu vipya kwa hawa Maroboti utamuweka Binadamu katika hatari ya kutawaliwa na hawa viumbe (Cheki movie ya I - ROBOT kama mfano) kwani wanaweza buni siraha hatarishi (A.I Weapons), kutenda kwa kufuata matakwa yao (kujiamulia) au kama wakiwa chini ya mtu mwenye malengo maovu wanaweza tenda kinyume na malengo ya kuundwa kwao (Cheki movie ya CHAPPIE kama mfano).

10) Hatari ambazo hatuzijui. (Unknown risks)

Ingawa miongo na karne kadhaa zilizopita stori za kuogofya kuhusu mwisho wa Dunia zilikuwa ni kuhusu Vita kuu ya Tatu ya Dunia na sababu nyinginezo ila hadi sasa kuna hatari nyingi sana zilizotuzunguka na hatujui itakuwaje hadi zitaleta Maangmizi Duniani.

SABABU ZA ZIADA:

01. Majaribio ya Kisayansi hatarishi.
MFANO;
● CERN's Large Hadron Collider.
● SETI experiments.
● Kola Superdeep Borehole.
● Nuclear Detonation Test (Majaribio ya mabomu ya Nyuklia).

02. Vitu hatarishi vya Angani.
MFANO;
● Mashimo meusi (Black holes) haya humeza chochote kilichopo ndani ya njia yake na kukifinyanga kuwa kama Tambi.. yana nguvu kiasi kwamba hata Mwanga hauwezi kuyahepuka. Galaxy letu lina mashimo meusi mengi sana na ni vigumu kujua pale linapokaribia.
● Gamma Rays Burst.
● Solar Flares.
● Supernovae.

03. Tabiri za kidini.
MFANO;
● Ujio wa pili wa Yesu / Nabii issa.
● Vita za kidini (Armageddon & Jihads).

* K A R I B U N I *
IMG_20211113_091855_235.jpg
View attachment 2008841View attachment 2008842View attachment 2008843View attachment 2008844View attachment 2008845View attachment 2008846View attachment 2008849View attachment 2008848
IMG_20211113_093055_352.jpg
IMG_20211113_093149_517.jpg
 
* K A R I B U N I *View attachment 2008840View attachment 2008841View attachment 2008842View attachment 2008843View attachment 2008844View attachment 2008845View attachment 2008846View attachment 2008849View attachment 2008848View attachment 2008847View attachment 2008850
Tafadhali unawez kuelzea kwa ufup Sana kivp CERN's LHC ikawa very risky?

Sent from my itel W6004 using JamiiForums mobile app
 
LHC ni mtambo unaozizungusha chembechembe za maada (particles) katika speed kubwa sana (yaani karibia 99% ya speed ya mwanga) halafu baadae unazigonganisha hizo chembechembe. Sasa kwa style hii nishati kubwa hutumika na kuna baadhi ya Wanasayansi wanaamini kuwa hali hii inaweza kuunda mashimo meusi madogo madogo (microscopic blackholes).

Ila haya mashimo meusi huwa na sifa ya kuvuta chochote kinachokatiza karibu yake (hata kama ni mwanga) maana yana uzito mkubwa sana kuliko hata jua letu pia yana nguvu kubwa sana ya Gravity..., na kadri yanavyozidi kula zile maada nayo yanazidi kukua na mwisho wa siku yanaimeza Dunia mzima.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Najaribu kuimagine hizo LHC pindi zitakapowashwa na tukajikuta inaanza meza Kila kitu Kwa Kasi ya tsunami na walioiwashwa wakashindwa izima na Ndio inakua forever together kaburini!

Majaribio mengine ni ya kutishana Kwa kweli
😁😁😁😁😁😁🔥
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom