Jinsi CCM inavyowachezesha Wapinzani kwa rimoti

mkuu Evarist Chahali hawa wapinzani wa nchi hii ni sikio la kufa...Tuliwaambia kuhusu EL hawakusikia.
Hapa ni kuwa ccm itatawala miaka yote nami namsapoti Jpm na serikali yake.
chADEma ni wahuni flulani
uko na verified ID ukidhani utakumbukwa cheo cha ufagizi ofisi za lumumba kwa kuutukana upinzani!!!
linganisha kura za slaa 2010 na lowassa 2015
 
Sema hivyo tuu Kwa sababu unaona ni sawa. Hivi mnataka watu wabadilishwe kwa style ile ya Gaddafi?
Lakini mkuu kuwa wakweli tu ;

Ni hoja ipi ambayo mpaka sasa hatujaisikia toka upinzani?

Tumesikia zote, hakuna kipya;
 
They are done; hamna kitu tena
Mi nadhani haujafa, isipokuwa serikali ndio inatamani hilo litokee.
Ingekuwa ni kwamba vyama vyote ni kama TLP,TADEA,DP,UDP,TPP,CHAUMA,CCJ,ADC, ningekubaliana na hiyo hoja. Lakini CHADEMA na CUF bado vinainyima serikali yetu usingizi. Zanzibar kule CCM bado haiwezi kujisimamia bila mkono wa dola. Huku bara CCM inaweza ikajaribu yenyewe lakini pia bila dola kuingilia inaweza na yenyewe ikashuka daraja.
Unajua siasa zetu bado ni za vyama sio sera na mahitaji. Bado watu wanadhani nijukumu la serikali kuweka chakula mezani kwao. Ndio maana licha ya serikali kusimamia utekelezaji na uwekaji udhibiti mzuri wa mazingira wezeshi, wananchi wao husema hatuna pesa, mara hali ngumu. Hawajui jukumu lao ni lipi na la serikali ni lipi. Kwa mantiki hiyo upinzani bado utaendelea kuwepo, hata maji yakitoka kila nyumba masaa 24, hata umeme ukiwaka masaa 24. Kuna watu wanataka serikali iwaingizie maji bure, umeme bure na chakula wapewe bure, matibabu bure na elimu bure.
 
Ni kweli kabisa sasa hivi kuna #2020 twende na Membe badala ya #FreeMboweMatiko.

Ndio maana sisi wengine tulimpa Magufuli kura sio kwa sababu ni bora, ila alikuwa na unafuu kuliko mpinzani wake...

Mpaka sasa tunamchukia Magufuli ila ukiangalia upande wa pili hakuna mbadala... ndio maana hata wao wamekuwa wakidandia yanayoendelea ndani ccm kuliko yanayowahusu.

Ukiangalia kwa jicho la tatu, kisa cha Mbowe kupuuza masharti ya dhamana ni ili akae ndani ni kuendelea kushikilia kiti kwa namna fulani.....kifupi anatafuta huruma ya wafusi kuendelea kukalia kiti.

Ni mtazamo tu.!
 
Yale yale ya kuendelea kucheza ngoma ya CCM.!
Mission ni moja tu, ni kumtoa Jiwe magogoni.

Awe CCM awe upinzani ila jiwe hatakiwi tena baada ya 2020.

Wapinzani wanajua dhahiri hawana chao kwenye urais kwasababu hawana tume huru ya uchaguzi na dola yote ipo CCM.

Cha kwanza jiwe atoke 2020. Mengine Wapinzani watahangaikia baada ya 2020.
 
Faida ya competetion ni kwenye choice ya mlaji. Kama hadi kwenye upinzani system ipo, shida yao nini sasa kukimbizana nao. Kama upinzani umekuwa tishio kwa usalama kwanini muundo mpya usiandaliwe kudhibiti hayo. Tunachoona tunapoteza utaifa kwa tamaa ya wachache. Wananchi hawana muda na siasa ila mnawalazimisha kwa matendo yenu. Mmewaweka jujuu muda wote wasililize siasa. Nadhani we are remotely controlled.
Lakini mkuu kuwa wakweli tu ;

Ni hoja ipi ambayo mpaka sasa hatujaisikia toka upinzani?

Tumesikia zote, hakuna kipya;
An
 
CHAHALI ACHA KUOKOTEZA STORI ZA VIJIWENI, KWA KIFUPI HUNA MPYA, SISI HATUMTAKI JIWE FULLSTOP, WEWE ENDELEA KUJIPENDEKEZA ILI AKUSAMEHE MAJUNGU YAKO.
 
aisee kwa hapa tulipofikia nashauri wanachama wa vyama vyote waungane wafanye maamuzi ya pamoja tz ni moja jamani
 
Hivi huyo mbunge full agent na sio informer ni nani? Tunaweza kuwataja na kuwachambua hapa kwa jinsi wanavyobehave ? Tunatamani tumfahamu kwa mustakabali wa watanzania na sio wachache wa tabaka tawala.......................FUNGUKENI PLEASE 1. NI ZITO KABWE 2.NI JOHN MNYIKA 3.NI JOSHUA NASARI 4.NI ESTER BULAYA 5.NI HALIMA MDEE AU NI NANI?
 
Moja ya mapungufu makubwa ya Wapinzani wetu ni suala lile lile wanaloilalamikia CCM kila kukicha, kwamba ukiikosoa CCM unaonekana mhaini. As if wao ni wazuri katika kukubali kukosolewa.

Katika hili la kumuona kila anayekosoa ni mhaini au anataka u-DC, tofauti kati ya CCM na Upinzani ni jina tu. Na utakuwa na bahati kama utawakosoa na wakakuita mhaini au mtaka u-DC bila matusi, another janga la kitaifa katika political conversations zetu.

Lakini kwa vile si kuitwa mhaini wala mtaka u-DC kunakoweza kumdhuru mtoa hoja, basi hakuna sababu ya kuchelea kuzungumzia masuala mbalimbali kuhusu Tanzania yetu.

Na ni katika mantiki hiyo, naamsha tafakuri kuhusu jinsi Wapinzani wetu wanavyoendeshwa kwa rimoti na CCM.

Mfano hai: ishu ya Membe. Kwa sie tunaokwenda mbali zaidi ya kusoma mabandiko mtandaoni (au/na ku-like/reply/comment) trend moja imejitokeza bayana tangu Bashiru atoe tamko kuhusu Membe.

Na trend hiyo ipo katika sura mbili. Kwanza, suala hilo linaongelewa zaidi na wapinzani kuliko CCM. Labda ni wishful thinking ya wapinzani kudhani suala hilo litaivuruga CCM. But they are wrong. It won't.

Membe is damaged goods. Mtu aliyefeli mchakato uliokuwa in his favour (he's one of the forces behind Lowassa's downfall kwenye kinyang'anyiro cha urais 2015) hawezi kufanikiwa thru "vita ya msituni."

Linalohusiana na sura hii ya kwanza ni ukweli kwamba japo upinzani wa kisiasa si uadui, kila mwenye akili timamu anafahamu kuwa CCM sio tu inawaona wapinzani kuwa ni maadui bali pia kama watu hatari zaidi ya wahalifu/wahaini/magaidi (you name it).

Na hilo halijaanza na Jiwe. Chuki ya CCM dhidi ya upinzani ilikuwapo from word go in 1992. Tofauti kati ya Jiwe na watangulizi wake ni kwamba yeye hahangiki kuficha chuki yake/ya chama chake vs Wapinzani.

Wakati CCM ya Jiwe inanunua wapinzani waziwazi, ya JK ilipandikiza watu kibao ndani ya upinzani walionawiri na kugeuka kansa inayoutafuna upinzani leo hii. Je wafahamu kuwa mbunge mmoja wa upinzani ni afisa kamili (sio source) wa Idara ya Usalama wa Taifa? Huo ni ndio "ununuzi wa wapinzani" uliofanyika kabla ya Jiwe, na ni wa hatari zaidi kuliko huu wa "nunua nunua" aka "hama hama."

Pointi yangu hapa ni kwamba japo upinzani wa kisiasa haupaswi kuwa uadui, "adui" wa kwanza wa Upinzani ni CCM...as chama cha siasa kilichopo madarakani, na ambacho wapinzani wanapaswa kujibidiisha kuking'oa. Kwahiyo iwe Membe, au Mwandosya, au Mwigulu au aendelee Jiwe madarakani, CCM itaendelea kuwa "CCM adui wa wapinzani."

Na la ziada hapo ni ukweli kwamba "vita ya jirani haimaanishi amani kwako." Kwamba kweli kuna vita inayoendelea chini chini huko CCM kuhusu urais 2020, kama ilivyokuwa 1995, 2005, 2015 na sasa 2020 (ilipaswa kuwa 2025 lakini sote twajua sababu za mabadiliko haya).

So, vita hizi zimekuwepo kila baada ya miaka 10. In fact huanza kila baada ya uchaguzi mkuu. JK na Lowassa walianza mkakati wa Ikulu mara baada ya kuwekewa zengwe na baba wa Taifa 1995 na wakaunda mtandao uliofanikiwa kuwaingiza madarakani miaka 10 baadaye yaani 2005.

Sawa, "adui yako mwombee njaa" but only if njaa hiyo itakuwa na faida kwako. Hakuna ushahidi wowote kuwa misukosuko ndani ya CCM huwanufaisha wapinzani. Kwa sababu kama ilivyo kwenye boxing, udhaifu wa opponent wako haumaanishi ubora wako. Ili kumtwanga bondia dhaifu shurti uwe bora zaidi yake na sio dhaifu kama yeye au zaidi yake.

Sura ya pili ya trend hii ni jinsi suala la Membe lilivyopelekea kwa kiasi kikubwa tu kusahaulika kwa masahibu yanayomkabili Mbowe na Esther Matiko, ambao wapo jela kwa siku kadhaa sasa, huku danadana ya kimahakama ikiendelea.

Lengo la danadana hiyo ni wanasiasa hao wawili wawe jela hadi baadaye mwakani. Why? Partly ni mkakati dhidi ya upinzani tarajiwa kwenye mjadala ujao bungeni kuhusu muswada ya vyama vya siasa.

Partly kuwakumbusha wapinzani kwamba "kama tunaweza kumfanyia hivi huyu kiongozi wenu mkuu, ninyi wengine ni akina nani haswa?" It's all wrong lakini it really doesn't matter kwa CCM, wazoefu wa kila mbinu chafu za kisiasa.

Samahani kwa andiko refu, lakini nihitimishe kwa kuwakumbusha ndugu zangu wa upinzani kuwa hizi sideshows za CCM zisiwafanye mjisahau.

Ni haki yenu kujadili kuhusu mustakabali wa siasa za Tanzania including kinachoendelea ndani ya CCM, lakini la muhimu msitolewe kwenye reli kirahisi hivyo.

Whether Membe anatendewa haki au la, haijalishi kwani mwajua fika kuwa Mbowe na Matiko wananyimwa haki zao. Epukeni kuendeshwa na matukio.

I stand to be corrected.
Nashukuru umekubali kukosolewa,kuna kitu umekosea ktk kuwa judge wapinzani,kwanza utambue kuwa ishu ya Mbowe kuwekwa gerezani na kunyimwa dhamana si jambo la kuwapa wapinzani tension as if huo ni unyama mpya kati ya unyama mwingi ambao Serikali ovu ya CCM imekuwa ikiwafanyia wapinzani.
Watu hawajatoka kwenye reli eti kwa sababu ya Membe,kuna jambo umeshindwa kujifunza hapo,kwa sasa adui mkubwa wa upinzani ni Magufuli,sasa adui yoyote wa Magufuli ni rafiki mkubwa wa wapinzani... no matter what!
Membe anaweza kuwa mbaya kwa wapinzani pia,lakini ni mzuri nyakati hizi ambazo wapinzani wana tabu kuu...
Ni ule msemo wa ndugu zangu waislamu,Nguruwe ni haramu,lakini ukizidiwa na njaa na hakuna chakula popote basi unaruhusiwa kumla Nguruwe,baada ya kushiba Nguruwe ataendelea kuwa haramu.
Nadhani hadi hapo umenisoma,jambo lingine umekosea kumtuhumu Membe kuwa ni mtu anaye fail mipango yake mingi kama alivyo fail kuupata urais 2015.
Hapo umechemka sana,2015 halikuwa kosa la Membe,sote tunajua kilichotokea,Tanzania ipo mikononi mwa mtu ambaye hata anajua fika kuwa hakupaswa kuwa rais.
Dhambi ya kikwete kumchafua Lowassa tangu akiwa waziri mkuu,kumtengenezea kashfa feki ya Richmond ili kumwondelea nguvu aliyokuwa nayo CCM,kwa lengo tu la kumwandaa Membe ili aje kuwa rais,kisha Membe ampe uwaziri wa mambo ya nje Ridhwani ili aandaliwe naye kuwa rais.
Mambo hayakuwa kama alivyotaka kikwete,nashangaa wewe mtu ulitumikia kitengo nyeti unashindwa kutambua hili,au unapuuza na kumdharau Membe kwa Sababu zako binafsi.
Halafu you should think beyond,mkuu niishie hapa kwa Leo,not everything that you plan will be successful... And nobody knows tomorrow, usipuuze mambo usiyoyajua kesho take,we're all blindfolded about our tomorrows.
Jiwe anaweza kutoka 2020 na huyu huyu Membe unayemdharau leo akashika nchi.
Soma mapinduzi ya Romania,uone kilichomtokea Nicolae Ceasecue .
 
Mange alikuita kichaa ila kila nikisoma thread zako nakuona wewe ni mtu makini unaeona mbali sana , yule mwanamke sitakaa nimuamini tena
 
Moja ya mapungufu makubwa ya Wapinzani wetu ni suala lile lile wanaloilalamikia CCM kila kukicha, kwamba ukiikosoa CCM unaonekana mhaini. As if wao ni wazuri katika kukubali kukosolewa.

Katika hili la kumuona kila anayekosoa ni mhaini au anataka u-DC, tofauti kati ya CCM na Upinzani ni jina tu. Na utakuwa na bahati kama utawakosoa na wakakuita mhaini au mtaka u-DC bila matusi, another janga la kitaifa katika political conversations zetu.

Lakini kwa vile si kuitwa mhaini wala mtaka u-DC kunakoweza kumdhuru mtoa hoja, basi hakuna sababu ya kuchelea kuzungumzia masuala mbalimbali kuhusu Tanzania yetu.

Na ni katika mantiki hiyo, naamsha tafakuri kuhusu jinsi Wapinzani wetu wanavyoendeshwa kwa rimoti na CCM.

Mfano hai: ishu ya Membe. Kwa sie tunaokwenda mbali zaidi ya kusoma mabandiko mtandaoni (au/na ku-like/reply/comment) trend moja imejitokeza bayana tangu Bashiru atoe tamko kuhusu Membe.

Na trend hiyo ipo katika sura mbili. Kwanza, suala hilo linaongelewa zaidi na wapinzani kuliko CCM. Labda ni wishful thinking ya wapinzani kudhani suala hilo litaivuruga CCM. But they are wrong. It won't.

Membe is damaged goods. Mtu aliyefeli mchakato uliokuwa in his favour (he's one of the forces behind Lowassa's downfall kwenye kinyang'anyiro cha urais 2015) hawezi kufanikiwa thru "vita ya msituni."

Linalohusiana na sura hii ya kwanza ni ukweli kwamba japo upinzani wa kisiasa si uadui, kila mwenye akili timamu anafahamu kuwa CCM sio tu inawaona wapinzani kuwa ni maadui bali pia kama watu hatari zaidi ya wahalifu/wahaini/magaidi (you name it).

Na hilo halijaanza na Jiwe. Chuki ya CCM dhidi ya upinzani ilikuwapo from word go in 1992. Tofauti kati ya Jiwe na watangulizi wake ni kwamba yeye hahangiki kuficha chuki yake/ya chama chake vs Wapinzani.

Wakati CCM ya Jiwe inanunua wapinzani waziwazi, ya JK ilipandikiza watu kibao ndani ya upinzani walionawiri na kugeuka kansa inayoutafuna upinzani leo hii. Je wafahamu kuwa mbunge mmoja wa upinzani ni afisa kamili (sio source) wa Idara ya Usalama wa Taifa? Huo ni ndio "ununuzi wa wapinzani" uliofanyika kabla ya Jiwe, na ni wa hatari zaidi kuliko huu wa "nunua nunua" aka "hama hama."

Pointi yangu hapa ni kwamba japo upinzani wa kisiasa haupaswi kuwa uadui, "adui" wa kwanza wa Upinzani ni CCM...as chama cha siasa kilichopo madarakani, na ambacho wapinzani wanapaswa kujibidiisha kuking'oa. Kwahiyo iwe Membe, au Mwandosya, au Mwigulu au aendelee Jiwe madarakani, CCM itaendelea kuwa "CCM adui wa wapinzani."

Na la ziada hapo ni ukweli kwamba "vita ya jirani haimaanishi amani kwako." Kwamba kweli kuna vita inayoendelea chini chini huko CCM kuhusu urais 2020, kama ilivyokuwa 1995, 2005, 2015 na sasa 2020 (ilipaswa kuwa 2025 lakini sote twajua sababu za mabadiliko haya).

So, vita hizi zimekuwepo kila baada ya miaka 10. In fact huanza kila baada ya uchaguzi mkuu. JK na Lowassa walianza mkakati wa Ikulu mara baada ya kuwekewa zengwe na baba wa Taifa 1995 na wakaunda mtandao uliofanikiwa kuwaingiza madarakani miaka 10 baadaye yaani 2005.

Sawa, "adui yako mwombee njaa" but only if njaa hiyo itakuwa na faida kwako. Hakuna ushahidi wowote kuwa misukosuko ndani ya CCM huwanufaisha wapinzani. Kwa sababu kama ilivyo kwenye boxing, udhaifu wa opponent wako haumaanishi ubora wako. Ili kumtwanga bondia dhaifu shurti uwe bora zaidi yake na sio dhaifu kama yeye au zaidi yake.

Sura ya pili ya trend hii ni jinsi suala la Membe lilivyopelekea kwa kiasi kikubwa tu kusahaulika kwa masahibu yanayomkabili Mbowe na Esther Matiko, ambao wapo jela kwa siku kadhaa sasa, huku danadana ya kimahakama ikiendelea.

Lengo la danadana hiyo ni wanasiasa hao wawili wawe jela hadi baadaye mwakani. Why? Partly ni mkakati dhidi ya upinzani tarajiwa kwenye mjadala ujao bungeni kuhusu muswada ya vyama vya siasa.

Partly kuwakumbusha wapinzani kwamba "kama tunaweza kumfanyia hivi huyu kiongozi wenu mkuu, ninyi wengine ni akina nani haswa?" It's all wrong lakini it really doesn't matter kwa CCM, wazoefu wa kila mbinu chafu za kisiasa.

Samahani kwa andiko refu, lakini nihitimishe kwa kuwakumbusha ndugu zangu wa upinzani kuwa hizi sideshows za CCM zisiwafanye mjisahau.

Ni haki yenu kujadili kuhusu mustakabali wa siasa za Tanzania including kinachoendelea ndani ya CCM, lakini la muhimu msitolewe kwenye reli kirahisi hivyo.

Whether Membe anatendewa haki au la, haijalishi kwani mwajua fika kuwa Mbowe na Matiko wananyimwa haki zao. Epukeni kuendeshwa na matukio.

I stand to be corrected.
Hivi wewe pia una amini Tweet ni za Membe??? maana Account original ya Membe aijapostiwa toka 2015!!! Wenyewe kwa Wenyewe mtafute mchawi acheni usaniii! au kweli Mweshimiwa Mbowe ana simu ya Mbunge Lema???? mpaka sasa Membe (ukipitia acc yake original AJAJIBU NA WALA AJAMWELEZA BASHIRU CHOCHOTE sasa nashangaaa wewe TISS nguli pia umeingia choo cha mabasha bora ingekuwa cha kike)
 
Back
Top Bottom