Jinsi CCM Ilivyowaingiza wafanyakazi kizani (SSRA)- Yaibuka Bungeni

Mpaka Kieleweke

JF-Expert Member
Feb 27, 2007
4,132
1,571
Hii ni sehemu ya hotuba ya kambi hya upinzani leo , wafanyakazi someni muielewe serikali yenu.

3.0 MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII
Mheshimiwa Spika,
Ayaya 81 ya Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduziya 2010 – 2015 iliahidi kwamba ili kuimarisha na kuendeleza hifadhi yajamii CCM itazielekeza Serikali zake “… kufanyatathimini ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na kurekebisha viwango vya mafao vinayotoaili visipishane mno; kuanzisha na kuimarisha Mamlaka ya Uthibiti na Usimamiziwa Sekta ya Hifadhi ya Jamii; na kuchukua hatua za makusudi za kupanua wigo wa kingaya Hifadhi ya Jamii, ili Watanzania walio wengi waweze kufaidika na huduma zamifuko ya jamii.” Vile vile, kwa mujibu wa Ilani hiyo, Serikali za CCMzitapaswa “kuelimisha jamii yawafanyakazi na waajiri juu ya umuhimu wa hifadhi ya jamii kwa maendeleo yawafanyakazi na ya nchi kwa ujumla”; na “kuendeleakutumia uwezo wa kifedha uliopo katika kila Shirika la Hifadhi ya Jamii, kwakuwekeza katika miradi mbali mbali ya maendeleo nchini.”
Mheshimiwa Spika,
Ahadiya kwanza iliyotajwa katika Ilani ya CCM, yaani kurekebisha viwango vya mafaoili visipishane mno haijatekelezwa hadi sasa kwani viwango vya mafao vinavyotolewana Mifuko mbali mbali ya Hifadhi ya Jamii ni vile vile vya kabla ya UchaguziMkuu wa 2010. Aidha, hakukuwa na sababu yoyote ya msingi ya kuingiza ahadi yapili katika Ilani hiyo kwani Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Mifuko yaHifadhi ya Jamii (SSRA) imekuwepo kisheria tangu mwaka 2008 wakati Bunge lako tukufulilipotunga Sheria ya Mamlaka ya Udhibitina Usimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, Sura ya 135 ya Sheria za Tanzania.Kuhusiana na utekelezaji wa ahadi ya tatu ya CCM kwa Watanzania, Taarifa yaWaziri wa Kazi na Ajira iliyotolewa kwa Kamati ya Huduma za Jamii mwezi Juni,2012 inaeleza kuwa “asilimia 6 tu yanguvu kazi ya Tanzania ndio wanaopata huduma za Hifadhi ya Jamii.” Kwamaana hiyo, ahadi ya kupanua wigo wa kinga ya hifadhi ya jamii ili Watanzaniawengi zaidi wafaidike na huduma hiyo nayo haijatekelezwa!
Mheshimiwa Spika,
Ahadiya nne kwenye Ilani ya CCM kuhusiana na hifadhi ya jamii nayo haijatekelezwakwani, kwa mujibu wa Taarifa ya Wazirikwa Kamati ya Huduma za Jamii, takwimu za Watanzania wanaopata huduma yahifadhi ya jamii “… zinadhihirisha kuwabado kuna uelewa mdogo wa masuala ya hifadhi ya jamii kwa watunga sera,waajiri, waajiriwa, wanachama na wananchi kwa ujumla.” Kama watunga sera,yaani Wizara na Serikali yenyewe, bado wana ‘uelewa mdogo wa masuala ya hifadhiya jamii’ – kama anavyokiri Waziri katika Taarifa yake - maana yake ni kwambaWatanzania wasitegemee kwamba Serikali hii ya CCM ina uwezo wa kutekeleza ahadizake za uchaguzi kuhusu kupanua wigo wa wapata huduma za hifadhi ya jamii!
Mheshimiwa Spika,
Ahadipekee kuhusu hifadhi ya jamii iliyotekelezwa na Serikali ya CCM ni kuendeleakutumia fedha za wafanyakazi zilizomo katika Mifuko mbali mbali ya Hifadhi yaJamii kuwekeza katika miradi ambayo haina manufaa yoyote kwa wafanyakaziwenyewe. Hii ni kwa sababu, Serikali imechota mabilioni ya fedha za Mifuko hiyona kuziingiza katika miradi ambayo haina manufaa yoyote kwa Mifuko yenyewe nahasa kwa wafanyakazi ambao ndio wenye fedha hizo. Ushahidi wa jambo hili, Mheshimiwa Spika, unapatikana katika Taarifa Kuu ya Mwaka ya Mdhibiti na MkaguziMkuu wa Hesabu za Serikali Kuhusu Hesabu za Mashirika ya Umma na TaasisiZingine kwa Mwaka 2010/2011 iliyowasilishwa kwa Rais Kikwete tarehe 28Machi, 2012.
Kwamujibu wa Taarifa hiyo, kuna udhaifu mkubwa katika vitega uchumi vinavyosimamiwana Mifuko ya Hifadhi ya Jamii. Kwa mfano, ukaguzi wa vitega uchumi vya NSSFulionyesha kwamba licha ya Mfuko huo kuwekeza shilingi bilioni 234.054 zawafanyakazi katika ujenzi wa Awamu ya Pili ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM),Mfuko ulikuwa haujasaini mkataba na Serikali juu ya fedha za mradi huo. Vilevile, kwa mujibu wa Taarifa hiyo, licha ya NSSF kusaini mkataba na Serikali ilikuwekeza shilingi bilioni 35.218 kwa ajili ya ujenzi wa Awamu ya Kwanza wa Chuohicho na licha ya majengo yaliyojengwa katika Awamu hiyo kuanza kutumika tanguSeptemba 2008, “Mfuko haujapokea fedha yapango, au malipo ya mkopo kutoka Serikalini ambao tayari umelimbikiza riba yashilingi bilioni 14.157.”
Aidha,Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu anaituhumu Serikali hii ya CCM kwa kukiuka masharti yamkataba kwa kugeuza riba ya mkopo wa NSSF kuwa sehemu ya mtaji wakati NSSFilitakiwa kupokea kodi ya pango ambayo ni gharama ya uwekezaji na riba yaasilimia 15 kwa mwaka kwa kipindi cha miaka kumi.
Mheshimiwa Spika,
Siofedha za NSSF tu ambazo zimetumiwa na Serikali hii ya CCM kwenye UDOM. Taarifaya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu inaonyesha kwamba Mifuko mingine nayo imepotezamabilioni ya fedha za wafanyakazi kwenye ujenzi wa Chuo hicho. Hivyo, kwamfano, PPF imekwishazamisha jumla ya shilingi bilioni 39.987; PSPFimechakachuliwa shilingi bilioni 105.921; LAPF imepoteza shilingi bilioni 22.030;wakati ambapo NHIF imekwishaunguza shilingi bilioni 13.403 za wanachama wake.Jumla ya fedha za wafanyakazi wanachama wa Mifuko hii mitano ambazo zimeunguzwakatika ujenzi wa UDOM ni shilingi bilioni 450.615. Kwa mujibu wa Taarifa ya Mdhibitina Mkaguzi Mkuu wa Fedha za Serikali, vitega uchumi vyote hivi katika UDOMvilikuwa ‘non-perfoming’, ikimaanishakwamba havirudishi fedha za mikopo yaMifukohusika.
Mheshimiwa Spika,
UDOMsio White Elephant pekee anayeteketezafedha za wafanyakazi. Kwa mujibu wa Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu, NSSF‘ilikubali’ kutoa mkopo wa shilingi bilioni 5.33 kwa riba ya asilimia 15 kwamwaka kwa ajili ya ujenzi wa Jengo la Idara ya Usalama wa Taifa. Mkopo huo nariba yake ulitakiwa kulipwa kwa njia ya kodi ya pango katika kipindi cha miakakumi kuanzia 2007. Hata hivyo, “taasisihusika ya Serikali bado haijaanza kulipa mkopo huo na hakuna malipo yoyoteyaliyofanywa hadi sasa. Vile vile, riba inayotokana na mkopo huo nayo badohaijalipwa. Taasisi husika ya Serikali ilitakiwa ianze kufanya malipo tangutarehe 31 Desemba, 2010.” Kwa mujibu wa Taarifa ya Mdhibiti na MkaguziMkuu, hadi kufikia tarehe 30 Juni, 2011, Jengo hilo la Usalama wa Taifa pialilikwishatafuna shilingi bilioni 6.5 za PSPF.
Mheshimiwa Spika,
Ujenziwa Ukumbi huu wa Bunge lako tukufu pia umefanywa na mikopo inayotokana na fedhaza makato ya wafanyakazi ambazo pia hazijalipwa hadi sasa. Kwa mujibu waTaarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu, hadi kufikia tarehe 31 Desemba, 2011, NSSFilikuwa haijalipwa shilingi bilioni 8.96, na PPF ilikuwa inadai malipo yashilingi bilioni 7.9 zilizotumika katika ujenzi wa Ukumbi huu wa Bunge. Aidha,hadi tarehe 30 Juni, 2011, LAPF ilikuwa imechangia shilingi bilioni 2.91 kwaajili ya ujenzi huo.
Mheshimiwa Spika,
Taarifaya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu inaonyesha fedha nyingine nyingi za Mifuko yaHifadhi ya Jamii zimetumika katika miradi ya ujenzi yenye manufaa yenye mashakakwa wafanyakazi na kwa Mifuko yenyewe. Hivyo, kwa mfano, mwaka 2007 NSSF ilitoa mkopo wa shilingi bilioni 20wenye riba ya asilimia 15 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za Jeshi la Polisi.Mkopo huo na riba yake ulitakiwa ulipwe katika kipindi cha miaka kumi baada yamwaka mmoja wa ‘huruma.’ Kwa mujibu wa Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu, “Mfuko haujaanza kukusanya kodi ya nyumbahizo kwani Mkataba wa Upangaji bado haujasainiwa licha ya kwamba nyumba zenyewezimekuwa zinakaliwa.”
Mabilionimengine ya wafanyakazi yameteketezwa katika ujenzi wa Machinga Complex ambayoni mali ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Kwa mujibu wa Taarifa yaMdhibiti na Mkaguzi Mkuu, mwaka 2007 NSSF ilitoa mkopo wa shilingi bilioni 12.9kwa riba ya asilimia 14.9 kwa mwaka kwa ajili ya ujenzi wa Machinga Complexjijini Dar es Salaam. “Mkopo haujaanzakulipwa bado na hakuna malipo yoyote yaliyofanywa. Hadi tarehe 30 Juni, 2011,mkopo huo ulikuwa umefikia shilingi bilioni 15.4.”
Mikopomingine ambayo Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu inaitaja kama ‘notperforming’ ni pamoja na Continental Venture Tanzania Ltd. inayodaiwa dola zaMarekani milioni 3.5, Meditech Industrial Co. Ltd. (dola za Marekani milioni1.45), General Tyre yenye kudaiwa dola za Marekani milioni 18.8 na Dar esSalaam Cement Co. Ltd. inayodaiwa dola za Marekani milioni 4.7. Wadaiwa wenginewa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ni pamoja na Kagera Sugar yenye kudaiwa shilingibilioni 12, Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) shilingibilioni 78.6 na Kiwira Power Ltd. shilingi bilioni 13.5.
Mheshimiwa Spika,
Hukumuya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu juu ya uendeshaji, udhibiti na usimamizi wa Mifukoya Hifadhi ya Jamii katika nchi yetu inajieleza yenyewe: “Kushindwa kwa makampuni haya (baadhi yao yakiwa yamedhaminiwa naSerikali) kuheshimu majukumu yao ya mikopo kunatia shaka kama uchambuzimadhubuti ulifanywa na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii juu ya uwezo wa wakopajikulipa mikopo hiyo. Zaidi ya hayo, ukubwa wa biashara inayofanywa baina yaMifuko ya Hifadhi ya Jamii na taasisi za Serikali na malipo yasiyokuwa nauhakika ya mikopo hiyo yanatia shaka juu ya uendelevu wa Mifuko husika katikasiku chache zijazo.”
Mheshimiwa Spika,
Taarifaya Waziri kwa Kamati ya Huduma za Jamii inaeleza kwamba NSSF imeanza kutekelezamradi wa uzalishaji umeme wa megawati 300 katika eneo la Mkuranga. Zaidi yahayo, Taarifa ya Waziri inasema kwamba NSSF imeanza ujenzi wa Daraja laKigamboni “… ambapo mkandarasiamepatikana na kukabidhiwa eneo la kazi, na yuko katika hatua ya ukusanyajivifaa kwa ajili ya kuanza ujenzi.” Aidha, katika mwaka wa fedha 2012/2013,NSSF itaendelea na ujenzi wa Daraja la Kigamboni na mradi wa uzalishaji umemewa Mkuranga. Vile vile, NSSF itawekeza katika ujenzi wa nyumba za Jeshi laWananchi (TPDF), kushiriki ujenzi wa Hospitali ya Apollo jijini Dar es Salaam,ujenzi wa ofisi za RITA, Chuo cha Sayansi na Hisabati katika UDOM na miradimingine mingi ya ujenzi kwa kutumia fedha za akiba ya wafanyakazi.
Kwakuzingatia yote ambayo yametokea kutokana na uwekezaji wa fedha za wafanyakazikatika miradi iliyokaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu, Kambi Rasmi yaUpinzani Bungeni inaitaka Serikali kusitisha mara moja matumizi haya makubwa yafedha za wafanyakazi katika miradi ambayo inaelekea kuifilisi Mifuko ya Hifadhiya Jamii na hivyo kuhatarisha maslahi ya moja kwa moja ya wafanyakazi waTanzania. Aidha, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka Serikali ieleze Bungehili tukufu kwa nini inatumia mabilioni ya fedha za akiba ya wafanyakazi kwa majengoyasiyokuwa na umuhimu wowote kiuchumi kama ofisi za Idara ya Usalama wa Taifa. Vilevile, Serikali ilieleze Bunge hili tukufu kwa nini hadi sasa haijalipa mikopona riba iliyotolewa na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kwa ujenzi wa miradiiliyotajwa na lini inatazamia kufanya hivyo.
Mheshimiwa Spika,
Kwaushahidi wa Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu, ni wazi kwamba Mifuko yaHifadhi ya Jamii ya Tanzania inaongozwa, kuendeshwa na kusimamiwa na watu ambaohawana uwezo wa kutekeleza majukumu yao kwa ujuzi na uadilifu unaohitajika kwamaslahi ya wafanyakazi wanachama wa Mifuko hiyo. Ni wazi, kwa ushahidi huu,kwamba mabadiliko makubwa ya kimfumo na kiutendaji katika Mifuko hiiyanahitajika na kwa haraka kabla mifuko hii haijafilisika kabisa. Kwa sababuhiyo, na ili kuinusuru Mifuko hiyo na kunusuru maslahi ya maelfu ya wafanyakaziwanachama wake, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inamtaka Rais Kikwetekuwawajibisha watendaji wakuu wote wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ambao wameachamabilioni ya fedha za wafanyakazi yazamishwe kwenye miradi mikubwa ya uwekezajiambayo, kwa ushahidi wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu, imefanywa bila uchambuzimadhubuti wa uwezo wa wamiliki wa miradi hiyo kurudisha fedha za wafanyakazi.
4.0 MAREKEBISHO YA SHERIA YAMIFUKO YA HIFADHI YA JAMII
MheshimiwaSpika,
Baadaya kutapanya fedha za wafanyakazi kwa kuwekeza katika grandiose projects isiyokuwa na manufaa ya kiuchumi kwa wafanyakaziwanachama na hata kwa Mifuko yenyewe, sasa Serikali hii ya CCM imeamua kuwadhulumuwafanyakazi fedha zinazotokana na makato ya mishahara yao. Vile vile, inaelekeaSerikali hii ya CCM inataka kuficha uchafu ilioufanya katika Mifuko ya Hifadhiya Jamii kwa kutunga Sheria inayowazuia wafanyakazi kupata fedha zao wakatiwanapozihitaji zaidi, yaani wanapokuwa hawana ajira. Hii imefanyika kwaSerikali kupenyeza kinyemela, na kinyume cha Kanuni za Kudumu, mashartiyanayowazuia wafanyakazi wote wanachama wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Tanzaniakuchukua mafao ya kujitoa uanachama wa Mfuko husika kabla ya kufikisha umri wamiaka hamsini na tano au sitini. Kisheria, umri wa kustaafu kwa hiari ni miakahamsini na tano wakati umri wa kustaafu kwa lazima ni miaka sitini. Kwamasharti haya, mfanyakazi hana haki au namna nyingine yoyote ya kupata fedha zamakato yake ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii hata akiachishwa kazi na mwajiri wakebila kosa lolote, hadi atakapofikisha umri huo wa kustaafu kwa hiari au kwalazima.
Mheshimiwa Spika,
Muswada wa Marekebisho yaSheria za Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, 2012 ulichapishwakatika Gazeti la Serikali la tarehe12 Januari, 2012. Hakukuwa na masharti ya kuzuia mafao ya kujitoa uanachama waMfuko. Tarehe 1 Februari, 2012, Muswada huu uliletwa Bungeni kwa ajili yaKusomwa kwa Mara ya Kwanza chini ya kanuni ya 83(1) ya Kanuni za Kudumu. Hapapia hakukuwa na masharti ya kuzuia mafao ya kujitoa. Baada ya hapo, Muswadaulipelekwa kwenye Kamati ya Huduma za Jamii kwa ajili ya kuujadili kwa mujibuwa kanuni ya 84(1) ya Kanuni za Kudumu. Masharti hayo hayakujadiliwa walakupendekezwa na Kamati ya Huduma za Jamii. Ingekuwa hivyo, kwa mujibu wa kanuniya 84(3) na (4)ya Kanuni za Kudumu, masharti hayo yangeletwa Bungeni wakati waMuswada kusomwa kwa Mara ya Pili. Hilo halikufanyika.
Kutokakwenye Kamati, Muswada huu ulirudishwa Bungeni tarehe 13 Aprili, 2012 kwa ajiliya Kusomwa kwa Mara ya Pili na kujadiliwa na Bunge lako tukufu chini ya kanuniya 86 ya Kanuni. Hotuba yote ya Waziri haina mstari hata mmoja unaoonyesha niaya Serikali ya kufuta mafao ya kujitoa kwa wanachama ambao hawajafikisha umriwa kustaafu kwa hiari au kwa lazima. Aidha, hotuba za Mwenyekiti wa Kamati yaHuduma za Jamii na Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni nazo ziko kimyajuu ya kufutwa kwa mafao ya kujitoa uanachama. Ukimya huu unatokana na ukwelikwamba hadi kufikia hatua hiyo hakukuwa na jambo lolote la kuashiria nia yaSerikali kufuta mafao ya kujitoa.
Aidha,sio Mwenyekiti wa Kamati au Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani pekee waliokuwakimya kuhusu masharti haya. Kwa mujibu wa TaarifaRasmi ya Majadiliano ya Bunge ya Mkutano wa Saba, Kikao cha Nne cha tarehe 13Aprili, 2012, hakuna hata mmoja wa Wabunge wote thelathini na nanewaliochangia mjadala wa Muswada aliyezungumzia suala la kufuta mafao ya kujitoauanachama wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii. Suala hilo halikuzungumziwa katikamichango ya Wabunge kwa sababu halikuwepo kwenye mjadala. Na wala halikuingizwakwenye mjadala na Wabunge wengine watano waliowasilisha Majedwali yaMarekebisho ya vifungu mbali mbali vya Muswada.
Mheshimiwa Spika,
Kwakutumia udhaifu wa uongozi wa Bunge katika kusimamia Kanuni za Kudumu, naupungufu wa muda wa mjadala Bungeni ambao ni matokeo ya kuvurugwa kwa Kanuni zaKudumu zinazohusu muda wa Wabunge kujadili hoja za Serikali, Waziri aliwasilishaJedwali la Marekebisho lililopendekeza marekebisho ya vifungu vipatavyo 45 navifungu vidogo karibu 70 vya Muswada. Ni katika msitu huo wa Jedwali laMarekebisho ndiko Serikali ilikochomeka masharti ya kufuta mafao ya kujitoa kwawafanyakazi wasiofikisha umri wa kustaafu kwa hiari au kwa lazima. Kwa sababu yaurefu wa Jedwali na uchache wa muda wa kulichunguza na kujadili, inaelekeahakuna Mbunge hata mmoja aliyeona mapendekezo hayo ya kufuta mafao ya kujitoa.Hansard inaonyesha kwamba ibara za 9, 10 na 11 “… zilipitishwa na Kamati ya Bungeni Zima pamoja na marekebisho yake.”Ibara ya 11 ndio iliyobadilishwa na Jedwali la Marekebisho la Waziri kwa kuwekamasharti kwamba mfanyakazi atapata mafao ya kujitoa pale tu atakapofikisha umriwa miaka 55 au miaka 60.
Mheshimiwa Spika,
Maranyingi Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imelalamikia ukiukwaji wa kanunizinazohusu muda wa mjadala Bungeni. Tumelalamika kwamba uongozi wa Bungeumeshiriki katika kupunguza muda wa mjadala kinyume cha Kanuni za Kudumu.Hatukusikilizwa. Tumepigia kelele kupunguzwa kwa muda wa mjadala wakati wakupitisha vifungu vya Miswada ya Sheria na mafungu ya bajeti. Hakuna aliyetakakuelewa kelele zetu. Tumepaza sauti zetu kwamba Bunge lako tukufu linageuzwakuwa muhuri wa kuhalalisha maamuzi ya Serikali tunayotakiwa kuisimamia nakuishauri. Tumepuuzwa. Haya ndio matokeo ya kuruhusu kanuni za mjadalakukanyagwa jinsi zilivyokanyagwa. Sheria hii inayodhulumu wafanyakazi kwakuzuia mafao yao ya kujitoa katika Mifuko ya Hifadhi ya Jamii sio tu ni matokeoya hila za Serikali, bali pia ni uthibitisho wa ulegevu wa uongozi wa Bunge naudhaifu wa Bunge lenyewe katika kusimamia Kanuni za Kudumu za Bunge lakotukufu.
Mheshimiwa Spika,
Kwamujibu wa Kumbu Kumbu Rasmi, kifungu pekee kilichofanyiwa marekebisho ya kuzuiafao la kujitoa ni kifungu cha 21 cha Sheria ya Mfuko wa Pensheni wa Mashirikaya Umma. Hata hivyo, SSRA imedai kwamba Sheria ya Marekebisho ya Sheria zaMifuko ya Hifadhi ya Jamii yanahusu Mifuko yote na wafanyakazi wote. KambiRasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka Serikali kulieleza Bunge lako tukufu kamaSheria hii mpya imerekebisha vifungu vya Sheria nyingine by implication, kama inavyoelekea kuwa tafsiri ya SSRA. Kama Sheriampya haijabadilisha vifungu vya Sheria za Mifuko mingine, ni kwa nini SSRA inang’ang’aniakwamba marekebisho ya Sheria ya PPF “…yanawahusu wafanyakazi wote nchini mwetu bila kubagua sekta yoyote ile.”
MheshimiwaSpika,
Aidha tunaelewa kuwa Pensheni ni suala lamsingi sana na hatuwezi kuwaacha wazee wetu waishi bila Pensheni. Vile viletunatambua kuwa kuna mahitaji ya sasa ambayo hayasubiri mpaka mtu azeeke ndipoaweze kuyatatua ndio maana tunaunga mkono wafanyakazi katika kupata fao lakujitoa na tunapendekeza sheria irekebishwe na kuzingatia yafuatayo;
i. Uanzishweutaratibu wa kuwa na mafao kwa wanachama ambao ama wamekosa kazi kutokana nasababu mbalimbali (Unemployment benefits)kama vile kumalizika kwa mkataba , kuachishwa kazi,kufukuzwa kazi nk kwakipindi cha miezi sita mwanachama wa mfuko husika aweze kulipwa kiasi cha mshahara kamili na miezi sita minginekama hajapata kazi alipwe nusu mshahara namfuko na baada ya mwaka mmoja kama atakuwa hajapata kazi basi mfuko uachekuendelea kumlipa mwanachama huyo. Mifuko itenge fungu maalum kwa ajili yakulipia mafao hayo.
ii. Mifukoitenge fedha kwa ajili ya masomo (Educationfund) kwa ajili ya wanachama wake pindi watakapokuwa wanaenda masomoniwakiwa ni wanachama wa mfuko ,hii itawafanya wanachama kuweza kujiendelezakielimu na hivyo itapunguza idadi yawanachama ambao wanajitoa kwa ajili ya kupata fedha za kusoma.
Mheshimiwa Spika,
Aidha Kambi Rasmiya Upinzani Bungeni inaitaka Serikali kurejea pendekezo letu tuliloishaurikatika bajeti ya Wizara hii ya mwaka 2011/2012 katika kuona umuhimu wakuiunganisha mifuko yote ya hifadhi za jamii na kubaki katika wizara mojaambayo ni ya Kazi na Ajira. Kambi rasmi ya Upinzani inasisitiza kuwa lengo kuula kuunganisha mifuko hii ya hifadhi za jamii ni katika kuirahisishia Mamlakaya Usimamizi na Udhibiti wa Hifadhi za Jamii (SSRA) katika kutekeleza Sheriamoja na kuunda vifungu sawa vya kisheria vitakavyosimamia utekelezaji nauendeshaji wa mifuko hii ambapo kwa sasa mifuko hii imekuwa chini ya wizaratofauti na hivyo hata utekelezaji wake unakua mgumu na kuleta ukinzani kwaMamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Hifadhi za Jamii. Tunasisitiza kuwapendekezo letu ni kuifanya PPF na NSSF iunganishwe na kuwa mfuko mmoja kwaajiliya Sekta Binafsi vilevile LAPF, PSPF na GEPF iunganishwe na kuwa mfuko mmojakwaajili ya Sekta ya Umma. Pia, kambi ya Upinzani inapendekeza mifuko yote isimamiwechini ya Wizara ya Kazi na Ajira.
 
Nimependa mapendekezo ya waziri kivuli kama SSRA wakichukua haya mapendekezo hapo ndipo tungesema hawa wana vichwa vya kufikiri si kusuka nywele!!!watumieni haya mapendekezo jamani maana .......
 
Back
Top Bottom