Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 43,037
- 34,741
Kwa yule mwenye jini mahaba ni kweli ana dalili asilimia 80 au zaidi ya zilizotajwa. Nimewahi kuwa mke mwenye jini mahaba, yaani ni shida na matatizo. Unahitaji kuwa na uvumilivu wa hali ya juu sana ili muendelee kuwa pamoja. Hatukuweza kuendelea kuishi pamoja pamoja na kuwa tuliishi kwa miaka 8 lakini ilikuwa ngumu sana kuvumilia. Hakika majini mahaba yanatesa sana watu.
Mimi nakubaliana 100% na mzizi mkavu.
Jini Mahaba kwa jina anaitwa Succubus
Majini yapo ya aina mbali mbali na koo zao ziko mbali mbali kutokana na maumbile yaliyoelezewa katika vitabu vya dini kuwa yametokana na moto, majini yana sifa za moto au joto katika usafiri wake wa aina tatu yaani conduction,convection na radiation.
Majini yanatuona na sisi hatuyaoni ila yanaishi ulimwemgu huu tuliyomo, kuna viumbe vingi duniani ambavyo mwanadamu hawezi kuviona ila kwa darubini lakini vile vile kuna viumbe hawezi kuviona hata kwa darubini ila kuhisi na kutambua kwa dalili tu.
Majini tunapishana nayo sehemu mbali mbali mida fulani na kiasi kwamba hata kurusha takataka kwenye majalala waweza kuyarushia kwani mara nyingi yapenda kukaa sehemu chafu baadhi yao, hivyo basi ikitokea ukarusha takataka likayapiga yanadhani umefanya makusudi nayo yanalipiza kisasi na kukutesa sana, ushauri weka takataka kwenye dust bin au jalala bila kurusha endapo yapo usije yapiga na kalipiza kisasi kwani ni machungu sana ukiyaumiza au kuyatupia kitu bila kuyaona.
Majini yana tabia kama ya wanadamu mfano kuna majizi(chuma ulete), mazinifu(majini mahaba), mafitini yenye kuchonganishi familia na wanajamii bila kuelewa kwa kuingilia mifumo yao ya fahamu na kuwatia wasi wasi na husuda kubwa yenye chanzo cha majini wa aina hiyo.
Majini mahaba yakimtamani mwanamke yanajitahidi kumuingilia usiku kama mke wa hayo majini na yakiisha muhodhi yanammiliki na hayataki mtu mwingine amguse au kumuoa kama hajaolewa kiasi kwamba posa zitaharibika kila mara, kama ni mke wa mtu yatamfanya amchukie mume wake bila sababu na akisafiri mke huyu anakuwa na furaha na akirudi anahuzunika na kuona yuko kama kifungoni vile, sehemu za siri zinakuwa na mgogoro kama kukauka, kubana sana, kuumia, kutoka damu ghafla ili mradi wasifanye tendo la ndoa na mume kwa amani.
Pia kuna majini mahaba ya kike yakitamani mwanaume usiku ataota mwananmke mzuri na atazini naye kila mara kiasi kwamba atamchukia mke wake bila sababu na kumuona mbaya wa sura na kumjibu majibu ya chuki hata kwa jambo la kawaida sana.Jini mahaba likiwa na wivu mwingi mpaka nguvu za kiume kumuingilia mke wake zinakosa na kuhisi moyo kwenda mbiu. Si hii tu mpaka mipango na afya yake vyaweza kuvurugika kila mara.Haiifai binadamu kuowa au kuolewa na Jini.
Ukiwa na Shida yoyote ile
Usipo pona kwa Dawa za Hospitali nitafute mimi nipate kukutibia upate kupona ukihitaji matibabu yangu
Unaweza kunitafuta kwa Mawasiliano Herbalist Dr. MziziMkavu Email barua ya pepe.fewgoodman@hotmail.com What's App na Viber +905344508169 Au Ni add Kwa Facebook tumia jina hili mzizimkavu.