Jini langu lina tamaa za mapenzi

Jini langu lina tamaa za mapenzi

Applicant

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2020
Posts
1,962
Reaction score
1,757
Kiukweli niwe wazi, mimi ninafuga jini qmbalo nalitumia kunipatia mali na kupata ninachotaka, lakini sasa cha ajabu linakua linataka kuplay role ya jini mahaba kwa kila msichana nitakaekua nae, yani kwamba nalo linataka mwanamke nitakaekua nae kimapenzi...!

Hii kitu inanipa stress sana, nakumbuka mwaka 2007 nililinunua lubumbashi kwa shilingi milioni 20, japo linaniingizia si chini ya milioni 2.5 kwa siku lakini tamaa zake ndio naona kero, natamani hata nilirudishe kwao.

Mnanishaurije?? Jini linalonipa utajiri linavunja kila mahusiano yangu nitakayokua nayo kwa tamaa
 
Naona katibu Pompeo umeamua kutangaza rasmi biashara yako ya ulozi.
 
goja jini lianze kupenda kuingiliwa lenyewe, ndo utajua hujui[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hilo jini Linakuingizia Mil 2.5 per day?,how? Na kwa kazi gani? Afu endelea kuchekelea lina tamaa na hao wanawake wako subiri likianza kutamani na marinda yako mkuu Pomp🤔
 
Ukishalinunua kulirudisha ni ngumu,Kuna mzee mmoja alinunua jini la kupata utajiri huko kaskazini alikua akifanya biashara za ng'ombe ..sasa lile jini likabadili gia angani likawa linamlazimisha kuoga mtoni mahali ambapo watu huamini kuna mizimu hela hakupata mwaka jana kapotea tu yaani hakuna anaejua ameelekea wapi, uongozi wa kijiji uliomba msaada kwa shule za karibu wanafunzi wakaruhusiwa kumtafuta lakini hajaonekana mpaka leo, hivyo kama unalo kweli ni bora utafute viongozi wa imani yako wakusaidie maana ni kisanga.
 
Naona katibu Pompeo umeamua kutangaza rasmi biashara yako ya ulozi.

[emoji23][emoji23]
 
Kiukweli niwe wazi, mimi ninafuga jini qmbalo nalitumia kunipatia mali na kupata ninachotaka, lakini sasa cha ajabu linakua linataka kuplay role ya jini mahaba kwa kila msichana nitakaekua nae, yani kwamba nalo linataka mwanamke nitakaekua nae kimapenzi...!

Hii kitu inanipa stress sana, nakumbuka mwaka 2007 nililinunua lubumbashi kwa shilingi milioni 20, japo linaniingizia si chini ya milioni 2.5 kwa siku lakini tamaa zake ndio naona kero, natamani hata nilirudishe kwao.

Mnanishaurije?? Jini linalonipa utajiri linavunja kila mahusiano yangu nitakayokua nayo kwa tamaa


Ni wajinga tu ndio Utawatapeli pesa.
 
Sasa wewe, lenyewe linakupa unachotaka,ila wewe hautaki kulipa linacho taka hauoni kuwa hautendi haki?Kila mla Cha mwenzake .........nadhani jawabu unalo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom