Jinamizi ni nini? Kwanini hutokea wakati wa kulala tu?

i pad3

JF-Expert Member
Mar 16, 2012
1,518
378
Kwanini jinamizi linatokea ukiwa umelala na ni nini dawa yake?

===========

Nadharia:
Jinamizi kwa kiingereza Nightmare ama waweza sema ndoto zisizo za kawaida kama vile za kutisha na kadhaalika.. Jinamizi linaloulizwa hapa ni Sababu ya hizo ndoto mbaya mfano mtu anahisi kama vile anakabwa na kushindwa kupumua,,Hiyo inaitwa Sleep Paralysis na hutokea either anapolala akiwa ameshiba uchovu nk.. Hususan akilala chali..

Kinachotokea ni Misuli kuchoka au Muscle atonia hapo panakosa mawasiliano mazuri kwenye mfumo wa mjongeo(Movement) na Upumua(Breathing) ndo mana mtu anahisi tabu kupumua na hata kusogeza japo kidole..

Ndoto za kutisha (nightmare). Zinasababishwa na shibe (kushiba sana), na ulalaji mbaya (chali)...!

Hali hii usababishwa na kugusana kwa diaphragm na abdominal, na hii kupelekea uvutaji wa pumzi kuwa wa shida... Na meseji inayopokewa kwenye ubongo wako ni picha mbaya ya kutisha (kukabwa).

Unaweza kumuona mtu aliyelala akiangaika uku na kule, unachopaswa ni kumtikisa polepole na kumuita jina lake ili ahamke... Hupaswi kumshtua kwa sauti mtu aliye kwenye hali hii, unaweza kumsababishia madhara mengine makubwa, kama vile mshtuko wa moyo.

Jinamizi, ni neno linalotumika kwa wagonjwa au watu fulani kutaka kueleza jinsi anavyo "kabwa" wakati akilala usiku.

Neno la kiingereza huitwa Breathlessness na lile la kitaalamu huitwa "Paroxysmal Nocturnal Dyspnea" (PND).

Hii hutokea pale kunapokuwa hakuna uwiano sawa kati ya damu inayozunguka mwili hasa itokayo na kwenda katika mapafu (Pulmonary Circulation) na Upumuaji wa hewa ya Oxygen..

Mkandamizo/Shinikizo(Pressure/Tension) unapokuwa mkubwa katika uwiano huu hasa kwa watu wenye magonjwa mengine tayari mfano moyo, mapafu, ini, figo pia uzee, n.k husababisha damu kurudi katika mapafu badala ya kuendelea na mzunguko wake wa kawaida...

Na kwa vile mapafu hutumika kwa kupumulia(Breathing), maji au damu yanapokuwa yakijaa husababisha mtu kushindwa kupumua vizuri, na wagonjwa/watu wengi husema "NIMEKABWA NA JINI ila baada ya kufungua madirisha liliondoka"...

Watu wengi husema hivyo kwa sababu mtu ukisimama mkandamizo ni mkubwa na hivyo kulazimisha kutoka katika mapafu kwenda katika moyo, na ile damu kidogo inayobaki due to gravity haileti madhara..lakini pale mtu anapolala tena, mzunguko ule ule hutokea na hivyo kufanya mtu kushindwa kulala, ..kutumia mito(pillows) husaidia katika hali hii, lakini ikumbukwe kwamba the more the pillows the worse the condition.

MUHIMU: Hali hii PND, "Kukabwa na jinamizi" hutokea na dalili nyingine kama kuchoka haraka,(katika kupanda ngazi, kutembea mwendo mfupi), mapigo ya moyo kwenda kasi, kusikia kizunguzungu n.k ila watu wengi hupuuzia kwani huona ni jambo la kawaida hadi pale hali inapokuwa mbaya kwa kushindwa kulala na hivyo kwenda hospitali..

Ushauri: Ni vema kuwahi HOSPITALI hali hii inapojitokeza.

Wengi wamekuwa wakiongelea kitu hicho, lakini ukweli ni kwamba watu wengi walalapo chali hubana kwa kiasi fulani mishipa iendayo kichwani na kusababisha upungufu wa oxygen katika ubongo na hivyo kumfanya mtu awe anaweweseka katia usingizi.

Wengine ni kwamba wakilala chali sehemu ya nyuma ya ulimi huziba kiasi fulani koo na kusababisha upungufu wa hewa hivyo kuufanya ubongo kukosa hewa ja kutosha na mara nyi gi watu hawa pia hukoroma.

Hatari ni kwama mtu aweza kuwa na magonjwa ya moyo yaliyo jifincha, mfano, wakati wa usiku anapata bradycardia (mapigo ya moyo au moyo kufanya kazi taratibu) na hufanya damu pia isifike ktk ubongo kwa wingi na kupunguza kiasi cha oxgen na mtu kujikia kama kabanwa au kaishiwa nguvu.

Kama mtu anapata jinamizi mara kwa mara ni vizuri akafanye kipimo cha ECG, kuangalia kama ana matatizo ya moyo. Kwa watu hawa mara nyingi hufariki wakiwa usingizini.
 
Hebu ngoja wajibu wenye experience na hayo madude. I have never come across..
 
Last edited by a moderator:
Ndoto za kutisha (nightmare).
Zinasababishwa na shibe (kushiba sana), na ulalaji mbaya (chali)...!

Hali hii usababishwa na kugusana kwa diaphragm na abdominal, na hii kupelekea uvutaji wa pumzi kuwa wa shida... Na meseji inayopokewa kwenye ubongo wako ni picha mbaya ya kutisha (kukabwa).

Unaweza kumuona mtu aliyelala akiangaika uku na kule, unachopaswa ni kumtikisa polepole na kumuita jina lake ili ahamke... Upaswi kumshtua kwa sauti mtu aliye kwenye hali hii, unaweza kumsababishia madhara mengine makubwa, kama vile mshtuko wa moyo.
 
jinamizi ni nini,,, jinamizi linatokano unapolala na uko katika hali ya uchafu na hali ya uchafu sio majasho kakini ni umefanya hali ndogo au kubwa au umetokwa na manii na ukalala bila ya kuoga,,,
 
Wengi wamekuwa wakiongelea kitu hicho, lakini ukweli ni kwamab watu wengi walalapo chali hubana kwa kiasi fulani mishipa iendayo kichwani na kusababisha upungufu wa oxygen katika ubongo na hivyo kumfanya mtu awe anaweweseka katia usingizi, wengine ni kwamba wakilala chali sehemu ya nyuma ya ulimi huziba kiasi fulani koo, nakusababisha upungufu wa hewa hivyo kuufanya ubongo kukosa hewa ja kutosha na mara nyi gi watu hawa pia hukoroma.

Hatari ni kwama mtu aweza kuwa na magonjwa ya moyo yaliyo jifincha, mfano, wakati wa usiku anapata bradycardia (mapigo ya moyo au moyo kufanya kazi taratibu) na hufanya damu pia isifike ktk ubongo kwa wingi na kupunguza kiasi cha oxgen na mtu kujikia kama kabanwa au kaishiwa nguvu. kama mtu anapata jinamizi mara kwa mara ni vizuri akafanye kipimo cha ECG, kuangalia kama anmatatizo ya moyo. kwa watu hawa mara nyingi hufariki wakiwa usingizini.
 
Jinamizi ni uongo ulotungwa na baadhi ya watu ili wauze vipindi wapate hela ati wana imani kali kumbe fix... We unalala chali unabana misuli yako hyo inayopeleka na kutoa info kwenye kichwa afu unashindwa kujitikisa then kesho ati Jinamizi lilikaba, hahaha, wabongo tumedakwa sana na Conspiracy theories, kitu kikiwekwa kwenye net tu bac watu wanadhani ni ukweli wakisahau anaeweka nae ni mtu
 
Hapo hakuna ushetani kwa sababu hii hali inaweza kukutokea hata kabla ya kusinzia lakini mwili hauwezi kumove na kuongea kwa sauti huwezi bali unaweza kunong'ona huku macho yakiona vizuri na kuzunguka pande zote.

Pia wakati mwingine hii hali inawatokea watu mchana kweupe pee.
 
Aaa." Kwaufaham wangu mimi ni tabia ya KISHETWaNI." Chakuzingatia ni kujiepusha kulala chali hbaass!ndo dawa yake!
 
kwa nini jinamizi llinatokea ukiwa umelala na ni nini dawa yake?

Jinamizi, ni neno linalotumika kwa waginjwa au watu fulani kutaka kueleza jinsi anavyo "kabwa" wakati akilala usiku!!

Neno la kiingereza huitwa Breathlessness na lile la kitaalamu huitwa "Paroxysmal Nocturnal Dyspnea" (PND)

Hii hutokea pale kunapokuwa hakuna uwiano sawa kati ya damu inayozunguka mwili hasa itokayo na kwenda katika mapafu( Pulmonary Circulation) na Upumuaji wa hewa ya Oxygen..

Mkandamizo/Shinikizo(Pressure/Tension) unapokuwa mkubwa katika uwiano huu hasa kwa watu wenye magonjwa mengine tayari mfano moyo, mapafu, ini, figo pia uzee, n.k husababisha damu kurudi katika mapafu badala ya kuendelea na mzunguko wake wa kawaida...na kwa vile mapafu hutumika kwa kupumulia(Breathing), maji au damu yanapokuwa yakijaa husababisha mtu kushindwa kupumua vizuri, na wagonjwa/watu wengi husema "NIMEKABWA NA JINI ila baada ya kufungua madirisha liliondoka"...
Watu wengi husema hivyo kwa sababu mtu ukisimama mkandamizo ni mkubwa na hivyo kulazimisha kutoka katika mapafu kwenda katika moyo, na ile damu kidogo inayobaki due to gravity haileti madhara..lakini pale mtu anapolala tena, mzunguko ule ule hutokea na hivyo kufanya mtu kushindwa kulala, ..kutumia mito(pillows) husaidia katika hali hii, lakini ikumbukwe kwamba the more the pillows the worse the condition.

MUHIMU: Hali hii PND, "Kukabwa na jinamizi" hutokea na dalili nyingine kama kuchoka haraka,(katika kupanda ngazi, kutembea mwendo mfupi), mapigo ya moyo kwenda kasi, kusikia kizunguzungu n.k ila watu wengi hupuuzia kwani huona ni jambo la kawaida hadi pale hali inapokuwa mbaya kwa kushindwa kulala na hivyo kwenda hospitali..

Ushauri: Ni vema kuwahi HOSPITALI hali hii inapojitokeza.
 
wengi wamekuwa wakiongelea kitu hicho, lakini ukweli ni kwamab watu wengi walalapo chali hubana kwa kiasi fulani mishipa iendayo kichwani na kusababisha upungufu wa oxygen katika ubongo na hivyo kumfanya mtu awe anaweweseka katia usingizi, wengine ni kwamba wakilala chali sehemu ya nyuma ya ulimi huziba kiasi fulani koo, nakusababisha upungufu wa hewa hivyo kuufanya ubongo kukosa hewa ja kutosha na mara nyi gi watu hawa pia hukoroma. Hatari ni kwama mtu aweza kuwa na magonjwa ya moyo yaliyo jifincha, mfano, wakati wa usiku anapata bradycardia (mapigo ya moyo au moyo kufanya kazi taratibu) na hufanya damu pia isifike ktk ubongo kwa wingi na kupunguza kiasi cha oxgen na mtu kujikia kama kabanwa au kaishiwa nguvu. kama mtu anapata jinamizi mara kwa mara ni vizuri akafanye kipimo cha ECG, kuangalia kama anmatatizo ya moyo. kwa watu hawa mara nyingi hufariki wakiwa usingizini.

Mkuu nice description, ila nadhani utakuwa unaongelea Obstructive Sleep Apnea, (OSA)
 
kwa nini jinamizi llinatokea ukiwa umelala na ni nini dawa yake?

hebu ngoja wajibu wenye experience na hayo madude ,i ahve never come across

hakuna kitu kinachoitwa jinamizi,ni kulala vibaya na kuibana baadhi ya mishipa ya damu tu.

aaa." kwaufaham wangu mimi ni tabia ya kishetwani." chakuzingatia ni kujiepusha kulala chali hbaass!ndo dawa yake!

jinamizi has more to do with brain activities then sipirituality. As u know the brain is like a computer, that means gabage in gabage out. Also a computer can as well stuck sometimes. So when you experience jinamizi, dont be shoked, wake up, drink something hot....rest and relax a little bit, listen to soft music for few second and then go back to sleep. If you can pray before you sleep.

 
Nadharia:
Jinamizi kwa kiingereza Nightmare ama waweza sema ndoto zisizo za kawaida kama vile za kutisha na kadhaalika..Jinamizi linaloulizwa hapa ni Sababu ya hizo ndoto mbaya mfano mtu anahisi kama vile anakabwa na kushindwa kupumua,,Hiyo inaitwa Sleep Paralysis na hutokea either anapolala akiwa ameshiba uchovu nk..Hususan akilala chali..Kinachotokea ni Misuli kuchoka au Muscle atonia hapo panakosa mawasiliano mazuri kwenye mfumo wa mjongeo(Movement) na Upumua(Breathing) ndo mana mtu anahisi tabu kupumua na hata kusogeza japo kidole..
 
Jamani nauliza hii kitu ni kweli na ikikutokea ufanye nini?........kuna vitu vinafana sana na simulizi za hii kitu huwa vinanitokea sana ..................nisaidieni bandughu
 
Lala vizuri,kama ni mto wa kulalia uwe wa wastani na usile chakula kingi kabla ya kulala.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom