Jinamizi ni nini? Kwanini hutokea wakati wa kulala tu?

Nimekua nikisikia na hata mara moja moja kukutwa na hali hii ya kukumbwa na hiki kitu kinachoitwa jinamizi,aghalabu hua ni nyakati za usiku ambapo unakua kama unakabwa na kushindwa kupumua huku ukipiga kelele ambazo hakuna anaezisikia!mwenye uelewa wa hili jinamizi jina ninalolifahamu mimi hebu tufunuliane nipate mwangaza hasa hiki nikitu gani!
 
”Jinamizi, au nightmare ni ndoto ambazo hututokea watu wote isipokuwa watoto wa umri mdogo sana mpaka miaka 5
Hizi ndoto mbaya zinakuja kwa njia nyingi kubwa zaidi ni kulala vibaya labda umejigeuza na kuwa umelala vibaya, au msongamano wa mawazo stress,anxiety. Pia ndoto mbaya zinakuja pia unapokula tu na kwenda kulala. Nafikiri umenielewa pia tusubiri wataalam zaidi
 
picchu uko sahihi kabisa hiyo inaitwa sleeping paralysis ila sababu ndio kama hizo ulizotoa hakuna cha majini wala mashetani
 
”Jinamizi, au nightmare ni ndoto ambazo hututokea watu wote isipokuwa watoto wa umri mdogo sana mpaka miaka 5
Hizi ndoto mbaya zinakuja kwa njia nyingi kubwa zaidi ni kulala vibaya labda umejigeuza na kuwa umelala vibaya, au msongamano wa mawazo stress,anxiety. Pia ndoto mbaya zinakuja pia unapokula tu na kwenda kulala. Nafikiri umenielewa pia tusubiri wataalam zaidi

mkuu nashukuru kwa maelezo yako
 
Jinamizi inaweza kuwa na maana mbili

1. Ndoto mbaya
2. Ni aina ya ugonjwa ambao bado unafanyiwa uchunguzi kwa sababu bado kuna utata kwa kiingereza wanaita sleep paralysis yani ni kuparalaizi ndani ya usingizi lakini hii hali huwa inamtokea mtu kama anakuwa yuko macho na anaona kinachoendelea (yani anakuwa kati ya kulala na kuwa macho) lakini hawezi kuongea wala kutikisika na akiishtuka huwa mapigo ya moyo yanakuwa juu sana. Kuna imani mbali mbali juu ya hili jambo kuna wengi wanao amini kuwa inatokana na majini au mashetani lakini pia wanasayansi wanasema inatokana na kulala vibaya mara nyingi chali na pia inaweza kuwa inatokana na matumizi ya madawa ya kulevya yaani ukiwa unatumia sana halafu ukakosa pia inatokana na uchovu sana yani ukilala ukiwa uchovu sana.
 
Tumezoea mara nyingi ukiwa usingizini hasa ukiwa umelala style ya kuangalia paa la nyumba(chali) kuna kitu kinatokea na kukukaba kwa nguvu zote na unakuwa unajitahidi sana kutoa sauti Ya kuomba msaada lakini bila mafanikio. Mara nyingi linapokukaba huwezi hata kugeuka, ukibahatika kuamka unajikuta umelala chali hivyo hivyo ndipo unapokumbuka na kuamua kubadilisha ulalaji,
Mara nyingi tumekuwa tukiambiwa kuwa hilo ni JINAMIZI. na linapenda watu wanaolala hiyo staili na kuwachezea,
Binafsi nimekuwa siamini hiki kitu, naamini kuwa kuna sababu ya kisayansi kabisa inayosababisha hilo tukio,ndio maana nimekuja hapa kwa wataalamu wetu watuambie hasa ni nn kinatokea hasa katika mwili kipindi hiki?
Tafadhari kama unajua chochote basi ni vyema ukakiweka hapa wengine pia tufaidike
 
hata mimi huwa inanitokea sana lakini kama hiyo siku nikisoma mda mrefu usiku,,badae niliizoea nikajua ni jambo la kisayansi tu kuhusiana na mwili wa binadamu,,niliamini hivi baada ya kumshirikisha rafiki yangu naye akaniambia humtokea akisoma sana...enzi hizo ilikuwa ni advance PCM,,lakini kwa sas sio mara kwa mara la ndoto za kupaa nazo zinajirudia
 
hata mimi huwa inanitokea sana lakini kama hiyo siku nikisoma mda mrefu usiku,,badae niliizoea nikajua ni jambo la kisayansi tu kuhusiana na mwili wa binadamu,,niliamini hivi baada ya kumshirikisha rafiki yangu naye akaniambia humtokea akisoma sana...enzi hizo ilikuwa ni advance PCM,,lakini kwa sas sio mara kwa mara la ndoto za kupaa nazo zinajirudia
Lakini kwa nini itokee wakati umelala chali? Inahusiana nn na kuota ndoto hizo mbaya mkuu?
 
Habari zenu wakuu,

Kuna vitu ambavyo naviwaza sivipati majibu mwenye uelewa kuhusu hili anisaidie.

Ni kwanini mtu unapolala kwa kuangalia juu yani bati anakuwa anaota ndoto mbaya za kutisha na kama vile kuna kukabwa flani hivi na hii sio kwangu tu nimewasikia watu wengi pia wakilalamika.

Je, jambo hili linahusiana na mambo ya kichawi kama wengi wanavyozani? Au kuna namna kisayansi lazima itokee endapo mtu akilala hivyo labla kuna vitu vinaforce ubongo kuhisi hivyo?

Wataalam naombeni msaada wenu
 
Dah hapa mkubwa cna cha kuchangia huwa hata mm inanitokea na cjapata jibu labda tusikie wadau humu
 
Habari zenu wakuu..
Kuna vitu ambavyo naviwaza sivipatii majibu mwenye uelewa kuhusu hili anisaidie..
Ni kwanini mtu unapolala kwa kuangalia juu yaan bati anakuwa anaota ndoto mbaya za kutisha na kama vile kuna kukabwa flani hivi... na hii sio kwangu tuu nimewasikia watu wengi pia wakilalamika.
Je jambo hili linahusiana na mambo ya kichawi kama wengi wanavyozani? Au kuna namna kisayans lazma itokee endapo mtu akilala hivyo labla kuna vitu vinaforce ubongo kuhisi hivyo?
Wataalam naomben msaada wenu.
Sidhani kama ina ukweli/uthibitisho/ushahidi wowote wa kidini au kitaalam; nadhani ni mtazamo wa mtu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom