Jina linalofaa kwa wanandoa

Sisi tunaitana majina yetu ya kwanza, na watoto siku wakitaka "kukata kiu" utasikia wanakuita jina lako...... huwa tunacheka tu.
Ila sasa wazazi huwa hawajisikii vizuri tunapoitana majina yetu mbele yao. nakumbuka kuna siku mama yangu aliwahi kuniuliza kwa nini namwita mume wangu kwa jina la kwanza, nikamjibu ndo nimezoea hivyo, akasema sio vizuri. mama mkwe wangu pia aliwahi kumwambia mume wangu kuwa mimi nina watoto, kwa hiyo aniite mama fulani, akamjibu hawezi. kwa hiyo inabidi watuvumilie tu
 
aisee, mie wa kwangu namwita jina lake la kwanza

Karibu niulize hapa jukwaani...Jamani fulani mbona haonekani siku hizi kaishia wapi? Bahati nzuri wakati napitia pitia mijadala hapa ukumbini nikamsoma mchangiaji mmoja aliyeandika De Novo alikuwa nani huko siku za nyuma :)
 
Sidhani kama ni vyema kumuita mwenzi wako kwa jina la kwanza tena mbele ya watoto maana kuna uwezekano mkubwa wa watoto ku-adopt utaratibu huo na kujikuta akimuita mzazi wake kwa jina lake la kwanza kitu ambacho si kizuri saaana kwa tamaduni zetu watanzania.,lakini mwisho wa siku hakuna sheria inayombana mtu kuchagua aitweje, nadhani mwisho wa siku ni busara za wazazi tu ndizo zinazohitajika katika hili.
 
Kwani tulipokutana tuliitanaje? Nadhani majina yenu ya kwanza ndiyo halisi na genuine kwani hata penzi likichuja bado mtaitana majina yenu tu. Lakini unapomwita mtu majina kama sweetie, sugar potato, my love, my darling, my...., je siku mkikoromeana mtaitanaje? Si watoto pia watawashangaa kuwa hawa leo imekuwaje? Ni vizuri kutumia majina halisi wakati wote!
 
Back
Top Bottom