Mshana,
Umechambua vizuri,
Labda niongezee kidogo, Kibiblia, maandiko yako wazi kwamba unapozaliwa tu, unapewa mambo mawili uchague ama Uzima na Mema au Mauti na Mabaya, Kumb.30:15, Na hii chanzo chake ilianzia pale mwanzo baada ya Adamu na Hawa kukaidi maagizo, Tangu wakati huo, dunia ilitekwa na shetani akawa anaimiliki dunia kila kitu Kiroho na Kimwili na ili kuhakiki kuwa shetani (ibilisi) alikuwa anaitawala dunia angalia Luka 4:3-13, Ibilisi anamuonyesha Yesu Kristo milki yake na fahari ya dunia kuwa ni yake....Hii haikumpa Mungu Ukuu wake akatoa tahadhali kwa kila mtu awe na uchaguzi ama Mungu (Uzima na Mema) au shetani (Mauti na Mabaya), Kwahiyo kama Mshana alivyosema, unapozaliwa tu unakuwa na uchaguzi wa aidha umwelekee Mungu au shetani, Na ujue shetani njia zake ni za uongo, udhalimu, mabaya yote, yatendekayo duniani yeye ndiye mwanzilishi akijipanga kwenda Jehanamu. Wema, ukweli, uwazi, furaha, amani, upendo, kuvumiliana, kuchukuliana, afya na uzima tele ndo mfumo halisi wa Mungu anavyotaka tuishi