Jina la Mfugale flyover lirekebishwe

Jina la Mfugale flyover lirekebishwe

Labda haijulikani lakini amekaa serikalini miaka 41.

Patrick Aron Nipilima Mfugale Alizaliwa katika eneo la Ifunda huko Iringa.

-Alipata elimu yake ya msingi katika shule ya Consalata Fathers Primary School mjini Iringa

-1975 Alimaliza elimu yake ya shule ya upili katika shule ya upili ya Moshi.

-1977-Mfugale aliajiriwa katika wizara ya ujenzi

-1983 alijipatia shahada yake ya kwanza katika chuo kikuu cha Rocky nchini India

-1991 Mfugale alisajiliwa kama muhandisi mtaalam.

-1992- Aliteuliwa kuwa mkurugenzi wa barabara za mikoa.

-1994-1995-Alipokea shahada yake ya pili katika chuo kikuu cha Loughborough, Braunshweig nchini Uingereza

-2003-Alipokea tuzo ya Distinguished Engineering Accomplishment.

-Aliteuliwa kuwa muhandisi mkuu wa madaraja nchini Tanzania wakati huohuo na akiwa masomoni nchini Uingereza mwaka 1995 alitafiti na kutengeneza mfumo wa madaraja nchini.

-Alitengeza mfumo wa usimamizi wa madaraja kwa jina Tanzania Bridge Management System

-2014- Alisajiliwa kuwa muhandisi mshauri na kuwa mwanachama wa chama cha wahandisi Tanzania.

-Ametumia muda wake mwingi kama mtaalamu wa madaraja .

Alibuni daraja la Magarasi lenye mita 178 kwa shilingi za Tanzania milioni 300.

-Baadhi ya madaraja alioweza kujenga ni:

  • Daraja la Mkapa Rufiji
  • Daraja la Umoja linalounganisha tanzania na Moxzambique huko Ruvuma.
  • Daraja la Rusumo huko Mara
  • Daraja la Kikwete huko Magarasi.
  • Daraja la Nyerere huko Kigamboni
- Mfugale ambaye kwa sasa ni mtendaji mkuu wa Tanroads amesaidia ujenzi wa madaraja 1400 nchini Tanzania.

Amebuni na kusimamia barabara za kitaifa zenye urefu wa takriban kilomita 36,258.

- Ni Mwenyekiti wa kikosi cha ujenzi wa Reli ya kisasa SGR inayoendelea kujengwa.

- Ni mjumbe wa timu ya majadiliano ya miradi mikubwa ya umeme.

-2018 Alituzwa tuzo ya uhandisi ya Engineering Execellency
Kwa haraka haraka na kwa kuzingatia umri wa watoto kuanza shule kwa miaka hiyo (miaka 7 hivi na mara nyingi zaidi ya hapo) kama alimaliza form four mwaka 1975 kwa sasa hivi alitakiwa kuwa alishastaafu. Labda ndiyo sababu ya kutotaja mwaka wake wa kuzaliwa. Yaani mwaka 1975 ni 7+7+4=18 yrs + 43 yrs=61 yrs. Tena hapo ni kama alibahatika kuanza darasa la kwanza akiwa na miaka 7.
 
Kwa haraka haraka na kwa kuzingatia umri wa watoto kuanza shule kwa miaka hiyo (miaka 8 hivi au zaidi) kama alimaliza form four mwaka 1975 kwa sasa hivi alitakiwa kuwa alishastaafu. Labda ndiyo sababu ya kutotaja mwaka wake wa kuzaliwa.
Hapo kuna "hidden agenda" Wasifu wa MTU so ndiyo CV bwana!! Na content za CV date of birth is inevitable!!!
 
Napendekeza jina la Mfugale Flyover lirekebishwe kuwa Patrick Mfugale Flyover. Sababu ni moja tu kuwa Mfugale wako wengi. Hivyo kutoa nafasi kwa Mfugale asiyehusika kunufaika na jina hilo. Mifano ni mingi kuhusu majina kuwa kamili au kuanza na herufi za kwanza.

Hoja zingine bhana wala hazifai kuwekwa hapa kwa ' Great Thinkers ' kabisa. Vipi kuhusu jina la Nyerere kutumika mahala mbalimbali? Ina maana linawahusu pia na akina Yericko na Steve ambao nao majina yao ya mwisho yanaishia na Nyerere? Sijaona tatizo lolote kwani ' Logically ' tu hata likiitwa hivyo hivyo Mfugale Flyover tayari Sisi wa Kizazi hiki ' automatically ' tu tunamjua ni ' Engineer ' Mfugale na siyo hao akina Mfugale wengine japo pia hata kama litawagusa hao ' Wafugale ' wengine bado hakuna ubaya wowote tena sana sana ndiyo itasaidia hilo jina Kukumbukwa mara kwa mara kiumuhimu wake na kuzidi kuwa jina Kubwa na lenye Heshima ya aina yake hapa Tanzania. Kwani majina ya Patrick nayo anamiliki Yeye tu? Mbona Congo DR zamani ( Zaire ) kulikuwepo Patrck Lumumba ( Mwanamapinduzi na Baba wa Taifa hilo ) lakini leo hii pia huko nchini Kenya kuna ' Mtaalam ' na ' Fundi ' wa masuala ya Kisheria na Siasa anaitwa Patrick Lumumba na bado haifuti ukweli kwamba Kizazi na Kizazi aliyenza kutangalia kuitwa hivyo ndiye atabaki kuwa ' Nguli ' na wengine watakuwa wanasafiria tu nyota yake.

Kila la kheri!
 
Sasa mbona una nongwa sana mzee?? Hata jina unakosoa kweli?
 
Napendekeza jina la Mfugale Flyover lirekebishwe kuwa Patrick Mfugale Flyover. Sababu ni moja tu kuwa Mfugale wako wengi. Hivyo kutoa nafasi kwa Mfugale asiyehusika kunufaika na jina hilo. Mifano ni mingi kuhusu majina kuwa kamili au kuanza na herufi za kwanza.
Jina linapwaya vilevile.He is not a monumental figure to deserve everlasting remembrance.Sifa zilizotolewa ni za kishkaji zaidi na siyo kitaifa.Turudishieni jina letu la Tazara Flyover kama hamna jina la maana.
 
Napendekeza jina la Mfugale Flyover lirekebishwe kuwa Patrick Mfugale Flyover. Sababu ni moja tu kuwa Mfugale wako wengi. Hivyo kutoa nafasi kwa Mfugale asiyehusika kunufaika na jina hilo. Mifano ni mingi kuhusu majina kuwa kamili au kuanza na herufi za kwanza.
Point taken.. Tatizo ni kukurupuka
 
akimaliza utawala wake hukombeleni akija kiongojimashuhuri nchinilitabadilishwa kama ilivyokuwa barabara ya Barak obama
 
Nadhani wahusika wamekusikia
Kapaisha ukoo wake libaki hilo hilo la Mfugale,Barabara ,majengo nk hayatakiwi kuwa na majina marefu sana ndio maana unakuta barabara inaitwa SOKOINE,KAWAWA,NYERERE,MANDELA ROAD NK MFUGALE LINATOSHA
 
Back
Top Bottom