Jina la Mfugale flyover lirekebishwe

Jina la Mfugale flyover lirekebishwe

Napendekeza jina la Mfugale Flyover lirekebishwe kuwa Patrick Mfugale Flyover. Sababu ni moja tu kuwa Mfugale wako wengi. Hivyo kutoa nafasi kwa Mfugale asiyehusika kunufaika na jina hilo. Mifano ni mingi kuhusu majina kuwa kamili au kuanza na herufi za kwanza.
Jiwe la msingi hili hapa. Sijui umefanya utafiti au umekurupuka?
20180927_195740.png
 
Kama Mfugale wa ukoo wetu amefanya makubwa kwa nini na sisi tusifaidike na jina la ukoo wetu.
 
Wewe sio mtu wa mjini (Dar es salaam) kile kibao kiliwekwa siku ya kwanza kabisa mwanzo wa daraja kushoto ukitokea airport kinasomeka "Eng. Patrick Mfugale Flyover' watu wana akili zaidi yako.
La. Nimekumbuka. Kweli. Lakini mie nimeona kubao kilichobandika juu ya daraja. Hata hivyo nimekupata. Uko sawa.
 
Daraja linaitwa eng Patrick mfugale fly over na si mfugale kama unavyotaka kuaminisha watu, kasome pale kwenye jina la daraja ndo utaelewa
 
Hela atoe mjapan jina lipewe mhehe.
Mlipakodi wa Japan ndie angeitwa lile daraja. Mitsui Miyosoka bridge. Ile siyo flyover jamani...
 
Hivi Mfugale alizaliwa mwaka gani? Mbona wakati Prof. Lema anasoma Wasifu wake hakusema alizaliwa lini zaidi ya kusema alizaliwa Mafinga na maeneo alikosoma tu
 
Labda haijulikani lakini amekaa serikalini miaka 41.

Patrick Aron Nipilima Mfugale Alizaliwa katika eneo la Ifunda huko Iringa.

-Alipata elimu yake ya msingi katika shule ya Consalata Fathers Primary School mjini Iringa

-1975 Alimaliza elimu yake ya shule ya upili katika shule ya upili ya Moshi.

-1977-Mfugale aliajiriwa katika wizara ya ujenzi

-1983 alijipatia shahada yake ya kwanza katika chuo kikuu cha Rocky nchini India

-1991 Mfugale alisajiliwa kama muhandisi mtaalam.

-1992- Aliteuliwa kuwa mkurugenzi wa barabara za mikoa.

-1994-1995-Alipokea shahada yake ya pili katika chuo kikuu cha Loughborough, Braunshweig nchini Uingereza

-2003-Alipokea tuzo ya Distinguished Engineering Accomplishment.

-Aliteuliwa kuwa muhandisi mkuu wa madaraja nchini Tanzania wakati huohuo na akiwa masomoni nchini Uingereza mwaka 1995 alitafiti na kutengeneza mfumo wa madaraja nchini.

-Alitengeza mfumo wa usimamizi wa madaraja kwa jina Tanzania Bridge Management System

-2014- Alisajiliwa kuwa muhandisi mshauri na kuwa mwanachama wa chama cha wahandisi Tanzania.

-Ametumia muda wake mwingi kama mtaalamu wa madaraja .

Alibuni daraja la Magarasi lenye mita 178 kwa shilingi za Tanzania milioni 300.

-Baadhi ya madaraja alioweza kujenga ni:

  • Daraja la Mkapa Rufiji
  • Daraja la Umoja linalounganisha tanzania na Moxzambique huko Ruvuma.
  • Daraja la Rusumo huko Mara
  • Daraja la Kikwete huko Magarasi.
  • Daraja la Nyerere huko Kigamboni
- Mfugale ambaye kwa sasa ni mtendaji mkuu wa Tanroads amesaidia ujenzi wa madaraja 1400 nchini Tanzania.

Amebuni na kusimamia barabara za kitaifa zenye urefu wa takriban kilomita 36,258.

- Ni Mwenyekiti wa kikosi cha ujenzi wa Reli ya kisasa SGR inayoendelea kujengwa.

- Ni mjumbe wa timu ya majadiliano ya miradi mikubwa ya umeme.

-2018 Alituzwa tuzo ya uhandisi ya Engineering Execellency
 
Jalada/file lake linaonesha alizaliwa lini?? Kama inajulikana alizaliwa Ifunda na maeneo yote alikosomea inakuwaje vigumu kujua mwaka alozaliwa?
 
Napendekeza jina la Mfugale Flyover lirekebishwe kuwa Patrick Mfugale Flyover. Sababu ni moja tu kuwa Mfugale wako wengi. Hivyo kutoa nafasi kwa Mfugale asiyehusika kunufaika na jina hilo. Mifano ni mingi kuhusu majina kuwa kamili au kuanza na herufi za kwanza.
Hata Patrick Mfugale hawezi kuwa peke yake.
Ungeshauri ziwekwe initials za majina yake mawili ya mwanzo, kama ilivyo kwa mji mkuu wa USA. Washington DC nk nk.
 
Jalada/file lake linaonesha alizaliwa lini?? Kama inajulikana alizaliwa Ifunda na maeneo yote alikosomea inakuwaje vigumu kujua mwaka alozaliwa?
Ni ajabu mkuu.
Labda hawataki astaafu kama kweli hajastaafu 😛😛
 
Back
Top Bottom