Jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro hali tete

Jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro hali tete

Emma M.

JF-Expert Member
Joined
May 15, 2009
Posts
204
Reaction score
6
Kuna tetesi kuwa Hali Vunjo ni Tete.
1. Huenda jimbo likagawanywa (Vunjo Mashariki na Vunjo Magharibi).

2. Chama chenye nguvu ya watu wengi ni CHADEMA hivyo itategemea hesabu za UKAWA kama zitakuwa za kusoma alama za nyakati.

3. CCM imechukua uongozi mji mdogo wa Himo.Hizi ni salamu za wazi kwa UKAWA na TLP.

4. NCCR inatumia mgongo wa CHADEMA kujipatia uhalali UKAWA kwa kuwa Mbatia ni mwenyekiti mwenza UKAWA.

5. Kuna tuhuma kuwa NCCR ilinunua viongozi wa CHADEMA kwenye chaguzi za serikali za mitaa ndipo ikapata ushindi mkubwa zaidi ya vyama vingine.Hujuma zilitembea UKAWA kwa UKAWA.

6. Watangaza nia ya Ubunge CHADEMA wana nguvu kubwa NYUMA ya wapiga kura wanao subiri maamuzi ya UKAWA.Watangaza nia wa CHADEMA wako kadhaa hadi sasa.

7. Endapo Mbatia atagawiwa hilo jimbo ki-urafiki wa UKAWA kuna uwezekano mkubwa wa CCM kuchukua jimbo kirahisi bila jasho kubwa.Hadi sasa aliyetangaza nia kugombea kupitia CCM ni mmoja yaani Inocent Shirima.

8. TLP bado haitabiriki kwani Agustino Mrema ana mbinu nyingi za ushawishi kwa wapiga kura dakika za mwisho, hasa kwa akina mama.

9. Inasemekana kuwa ACT ya ZITTO KABWE inasubiria kuona maamuzi ya UKAWA ili ACT ipenyeze kwa kasi kupitia makosa ya maamuzi ya UKAWA. ACT sasa inajijenga mkoani kilimanjaro.

10. Wapiga kura wa Vunjo wanatabia ya kuwavuna wagombea pesa ila humpa kura mgombea anayeelekea kuishi jimboni baada ya kuchaguliwa.

Karibuni kwa mawazo na uchambuzi,

NAOMBA kutoa HOJA.
 
Mkuu unakaa vunjo au umepitia tu kama alivyo huyo dogo Shirima na pia huyo dogo alikua na beef na wazee wa huko limeisha au mnalazimisha tu apite. Na yule aliegombea kipindi ile yupo wapi je unajua kajipangaje
 
Wewe umetumwa...sasa hapo hoja ni nini? Ukawa ndo mpango mzima....mgombea wa NCCR NDIYE huyo huyo wa chadema au Cuf na kinyume chake...
 
Ishu ya kugawa majimbo naiona ni upande wa yanayoongozwa na upinzani tu! Vyovyote itakavyokua kuna possibility kubwa kuwapa ukawa more chance of winning. All in all Mbatia atapita Vunjo! Mrema hana chake CCM kwishney. Really fact hakuna jimbo linalojitambua kama Vunjo katika Majimbo yote Tanzania ...... October si mbali
 
Watagawa wapi hilo Jimbo ambalo ukipanda mtini unaona mwisho Kirua pale Mwika pale Kahe pale makuyuni ile
 
Vunjo bado ni jimbo dogo sana kuligawa,, angalau wangezungumzia jimbo la Rombo, maana ni kubwa sana sana.

Kuhusu ubunge, huo ni mtazamo wako tu. Ila jimbo lile hata kama kura hazijapigwa bado Mbatia atalichukua. Hayo mengine ni fitina na majungu tu unajaribu kupiga kwa malengo ya kuteteresha ukawa, ila jamaa wamejipanga hata CCM wanalijua hilo. Hawafuati majungu!!
 
jimbo la vunjo wangekuwa wanajitambua wasingemchagua mrema aliyekuwa anajipigia debe yeye huku akiwaambia wana vunjo wamchague JK wakt TLP ilikuwa na mgombea urais
 
tangu lini Mbatia akawa Mbunge wa Vunjo? Mbunge wa Vunjo ni Mrema.
 
Huo ni uoga usio na msingi wowote, Najua bandiko hili linahusiana moja kwa moja na John Mrema (Mtanisahihisha jina) wa Cdm...!!!!

Lakini tujenge mazoea ya kuheshimu maamuzi ya viongozi wakuu. Umoja wa UKAWA ni njia nyepesi isiyo na mabonde wala Milima kuelekea Ukombozi hatimaye tulifikie jumba lenye thamani kuliko yote hapa Nchini (Magogoni)

Katika njia ya kuelekea huko, moja ya gharama ni kama hizi, Unasalimisha lilicho chako kwaajili ya nduguyo..!!! Kwa Mrema nadhani kuna kazi nyingine zaidi ya Ubunge kichama, Waweza kugombea Udiwani tukilenga kupata Umeya wa Mji huo. Tusitengeneza fitna zisizo na msingi kwa mustakabali wa UKAWA

Ni hayo tu.

BACK TANGANYIKA
 
kaka unanifurahisha sana
natamani kukufahamu na kukutana na ww kwa sababu we unaonesha uhalisia bila uoga
 
kaka unanifurahisha sana
natamani kukufahamu na kukutana na ww kwa sababu we unaonesha uhalisia bila uoga

Pamoja sana mkuu,

Panapomajaliwa na ikimpendeza Mungu, one day tutafahamina na kuonana kabisa.!

BACK TANGANYIKA
 
Huo ni uoga usio na msingi wowote, Najua bandiko hili linahusiana moja kwa moja na John Mrema (Mtanisahihisha jina) wa Cdm...!!!!

Lakini tujenge mazoea ya kuheshimu maamuzi ya viongozi wakuu. Umoja wa UKAWA ni njia nyepesi isiyo na mabonde wala Milima kuelekea Ukombozi hatimaye tulifikie jumba lenye thamani kuliko yote hapa Nchini (Magogoni)

Katika njia ya kuelekea huko, moja ya gharama ni kama hizi, Unasalimisha lilicho chako kwaajili ya nduguyo..!!! Kwa Mrema nadhani kuna kazi nyingine zaidi ya Ubunge kichama, Waweza kugombea Udiwani tukilenga kupata Umeya wa Mji huo. Tusitengeneza fitna zisizo na msingi kwa mustakabali wa UKAWA

Ni hayo tu.

BACK TANGANYIKA
Suala si John Mrema tu.
Pamoja na kwamba :
1. kweli john Mrema bado ni maarufu Vunjo, lakini nasikia kuwa tayari kuna wana-CHADEMA wengine wameshatangaza nia Vunjo na wanakubalika na wananchi kuliko hata John Mrema na Mbatia..
2. Pia si vema kufikiri kuwa Agostino Mrema hana wafuasi wengi Vunjo.
3. CCM imechukua uongozi wa mji mdogo Himo. Hili mbona mnadhani sii kiashiria cha kulichukua jimbo pia?
 
Wadau;
Kwa 'hisia' na 'Ukweli' kwa sisi wafuatiliaji wa siasa za 'ukombozi', 'hisia' ni kwamba, itakuwa mchuano mkali, lakini 'Ukweli' kwa jinsi tunaoujua ni kuwa watakapokosea kuligawa jimbo la Vunjo ili kuleta Majimbo Mawili, ya Vunjo Mashariki na Vunjo Magharibi,

hayo yote yatakwenda kwa UKAWA maana kwa taarifa tu ni kuwa Vunjo Magharibi [Nyumbani kwa Mbatia] huko hata CCM wasipoteze muda kupeleka mgombea [Ofisi za Watendaji wa CCM - Nduoni, zilishafungwa zamani, hakuna CCM - (by Taarifa ITV news)], na kwa Vunjo la Mashariki, [ambalo ndiko Mrema wa TLP na Mrema wa Chadema wanatokea],
Mrema wa TLP anajua kuwa hali mbaya mno! hata Madiwani wake kadhaa walishaasi na amebakia na Mkiti za Kijiji kimoja au viwili tu. Kimojawapo ni kijiji alikozaliwa ca 'Kiraracha'!

Kwa CCM wanajua ukweli kuwa kwao kushinda ktk vijiji na mji wa Himo, hakuna kitu kwa Vunjo Mashariki nzima, maana mji wa himo wakazi wake wanaeleweka, na asili ya wengi wanatokea upareni [Mwanga, Kahe na Ugweno], na endapo UKAWA watamsimamisha tena Mh John Mrema [Chadema] kwa ajili ya Vunjo Mashariki, CCM na TLP vitafutika ktk historia ya Kilimanjaro ifikapo Oktoba 2015.

NOTE: TUME wakilogwa kakiligawa Jimbo la Vunjo, wameizidishia Ushindi na idadi ya wabunge Serikali ya UKAWA!
Picha chini zinajieleza zenyewe!

8d696__mrema.JPG John-Mrema.jpg John Mrema.jpg

Mbatia & Mrema TLP.jpg
 
Mwaka huu Mrema asipovaa siketi ili Rais ampe ubunge wa viti maalumu atakuwa na Bahati sana.
 
Mkuu wagawe wasigawe Mbatia tosha, hamna kosa litakalofanyika UKAWA ndo mpango mzima
 
Bunge limetenga boonge la budget kwa MAKABURI ya viongozi huko Dodoma...sijui itakuwaje.Hivi walifikiria kuhusu mila na tamaduni za watu kuhusu maziko....kwani wakizwa peke yao ndio hawatajipanga foleni kwenda mbinguni.Kama mila yako hairuhusu kuzikwa nje ya home USIGOMBEE tena
 
............ ktk mgawanyo wa majimbo ukawa mkoa wa kilmanjaro majimbo ya NCCR ni mawili ambayo ni Vunjo na Mwanga,namshangaa akisema vunjo kuna mgombea wa cdm.

Hili wazo linashangaza,
Eti Vunjo na Mwanga kagawiwa NCCR.
Kama kweli itakuwa hivyo ujue kuwa CDM itakuwa inajizika taratibu kwenye majimbo hayo mawili.
Kuna makamanda wa CDM wanakubalika sana Vunjo na Mwanga.
Iweje NCCR ipewe kama zawadi?
Nadhani wewe hufuatilii vizuri siasa za VUNJO na MWANGA.
Nakushauri uwajue watangaza nia wa majimbo haya mawili (MWANGA na VUNJO) kwanza kabla hujazungumzia ETI kapewa NCCR.
 
Back
Top Bottom