Unataka ushahidi gani Mkuu wakati kila kitu kipo wazi? kaka kuwa targeted si lazima bastola iwe sikioni - ni matendo tu anayofanyiwa huyu kamanda kweli yanaashiria mwisho wa Sitta CCM. na hata akin'gan'gania kubakia humo bado atakuwa na misukosuko mingi sana kuelekea uchaguzi mkuu.
Kitendo cha UVCCM kukabidhiwa majimbo yote ya hawa wapiganaji kuhakikisha yanachukuliwa na wao ni kitendo tosha kwamba wameshawachoka.
Mtera - Jimbo limekabidhiwa wa UVCCM
Urambo - Jimbo limekabidhiwa wa UVCCM
Nzega - Jimbo limekabidhiwa wa UVCCM
Simanjiro - Jimbo limekabidhiwa kwa UVCCM nk
UVCCM watapata kila support kutoka makao makuu kuhakikisha list hii hapa chini hairudi bungeni kwa tiketi ya CCM
Kwa hiyo, Sintashangaa kutowaona Malecela, Selelii, Sitta, Sendeka, Mwakyembe, Sherukindo, Shibuda kwenye bunge lijalo - ni vizuri tu waanze kujipanga mapema kukabiliana na vita hii ndani ya CCM.