Jimbo la Siha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jimbo la Siha

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Giddy Mangi, Apr 27, 2011.

 1. G

  Giddy Mangi JF-Expert Member

  #1
  Apr 27, 2011
  Joined: Feb 14, 2011
  Messages: 833
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Jimbo la Siha lina changamoto nyingi ikiwemo Miundombinu,Afya,Elimu na uwajibikaji wa watendaji wa Serikali.Mbunge wa Siha Mh.Agrey Mwandri amekuwa Mbunge kwa miaka Kumi sasa na japo kuwa kofia ya pili ndani ya serikali ya Ccm tena wizara nyeti ya TAMISEMI ameshindwa kufanya mambo ya msingi na pia ameshidwa kutatua kero za wana wa Siha kwani kero kubwa zikiwemo Elimu,Afya,Miundombinu ya barabara na Masoko bora bado ni kero zinazo wakabili watoto,baba,mama,bibi na babu zake Mh Mwandri ambaye anasikifa sana kwa majibu mazuri ndani ya Bunge hili hali akiwa amewasahau wapiga kura wake tena ambao uwakumbuka tuu wakiwa na misiba na pia wakati wa kampeni akiwafuata kwenye vilabu vya mbege na kuwanunulia ikiwa ni njia ya kuomba kura.NAOMBA MSAADA WA MAWAZO TUWASAIDIE VIPI WANA SIHA.
   
 2. Mlengo wa Kati

  Mlengo wa Kati JF-Expert Member

  #2
  Apr 28, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 2,733
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Siha kila kijiji kina maji,na sasa vimebaki vijiji nane tu ambavyo havina umeme,barabara za siha zimetanda vijiji vyote! Najua unataka Ubunge jenga hoja tu kwa wananchi ila mkoa wa kilimanjaro hakuna jimbo ambalo limefanikiwa kwa maendeleo kama Siha Mwanri amefanya kazi sana! Wewe wambie wananchi mabadiliko ya kupata mbunge mwingine ni mhimu kwenye barabara,maji,umeme usiguse watakushangaa na kukuona uko nyuma ya wakati!
   
 3. G

  Giddy Mangi JF-Expert Member

  #3
  Apr 28, 2011
  Joined: Feb 14, 2011
  Messages: 833
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hapana kwani ninajaribu kuona mbali ya hapo ulipo wewe,barabara ya Lawate Kashashi hadi Forest imechakachuliwa na serikali imetenga tema M.30 ambazo zimeanza kuliwa na ushahidi upo.,mkandarasi wa Halmashauri atakuwa anaelewa ninasema nini sasa,pia viwanja vya mji mpya kule Sanya wamegawiwa wenye uwezo huku mashaba makubwa maeneo ambayo watu wa hali ya chini wangeweza kulima na kujipa tia chakula yamegawanywa kwa wachache wenye nazo ambao wanaitwa matajiri wa Siha.Mifano ya barabara mbovu ninayo mingi,shule mbovu na hata maeneo yenye shida ya masoko na huduma za afya hakika Siha inahitaji Mbunge Mwanri afanye kazi ya ziada.
   
 4. measkron

  measkron JF-Expert Member

  #4
  Apr 28, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 3,713
  Likes Received: 365
  Trophy Points: 180
  umetaja maji hujagusia Afya ambapo katika mkoa wa Kilimanjaro ni Wilaya ya Siha hawana hospitali ya wilaya wala ya Shirika lisili la kiserekali inayoweza kufanya kazi kama hospitali teule ya Wilaya..... kikubwa hawana Ambulance, gari la kubeba wagonjwa nashindwa kuelewa mbunge wao kama Waziri TAMISEMI kashindwa kusaidia hapa... wanafikisha ngonjwa late hospitali za KCMC, Mawenzi. ukipata ndugu anahitaji rufaa toka Siha kwenda KCMC ama Mawenzi ndo utajua nazungumza nini hapa. U simtetee bado hajafanya kazi huyu mbunge.
   
 5. M

  Moelex23 JF-Expert Member

  #5
  Apr 28, 2011
  Joined: Oct 8, 2006
  Messages: 497
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ndugu Giddy mangi, naona umekuja na propaganda kali.

  Swali:: Ilikuwaje mpaka jimbo la Siha likawa Wilaya?? Unajua ilivyokuwa vigumu kuaccomplish hilo jambo??

  Sasa baada ya kuwa Wilaya, unataka ASAP kuwe na Hospitali ya Wilaya wakati KCMC ni karibu??

  Suala la Umeme vipi Siha?? Je maji salama vipi na huo mradi mkubwa wa Wajerumani?? Barabara za Lami mpaka huko Sanya Juu vipi?? Shule za Sekondari kila kona nazo vipi??

  Wilaya bado inachangamoto nyingi ambazo zinaendelea kushughulikiwa. The fact kuwa SIHA ni Wilaya imeleta benefits nyingi mno na zingine zitaendelea kuonekana jinsi siku zinavyokwenda.

  Kwa hiyo Mwanri kuwa Waziri Tamisemi ulitaka afanye ufisadi na kupendelea SIHA kwa gharama ya kutekeleza wilaya zingine nchini?? Huyu mtu sio wa dhuluma na anafanya kazi kwa manufaa ya nchi wakati huo huo akijaribu kuleta maendeleo Siha kwa juhudi bila kucompromise wilaya nyingine maskini ndani ya TAnzania.
   
 6. Mlengo wa Kati

  Mlengo wa Kati JF-Expert Member

  #6
  Apr 28, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 2,733
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Unachekesha sasa Hospitality ya Kibong'oto iko wapi? Tena ni hospital Bingwa ya Kifua Kikuu ipo SIHA na inatoa na huduma mbalimbali ukiacha Kifua kikuu! Siha inaenda kwa kasi sana ilinganishe na Hai utaona hai wapo palepale!
   
 7. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #7
  Apr 28, 2011
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,696
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  Mjadala mzuri sana huu. Ni wa maendeleo badala ya siasa na porojo. Tungekuwa na mingi ya namna hii ya kuwapa changamoto wabunge na viongozi wengine. Hongereni akina Mangi. Kama kawaida.
   
 8. measkron

  measkron JF-Expert Member

  #8
  Apr 28, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 3,713
  Likes Received: 365
  Trophy Points: 180
  we ndo umechekesha. tofautisha Hospitali ya kifua kikuu na hospital ya Wilaya....Nadhani huna data za kutosha.... unajua kwamba chumba cha upasuaji pale Kibon'goto kimefungwa na hakuna upasuaji wowote pale? hadi wajenge hospitali ya Wilaya..... naongea kama Daktari na mwanasiha pia..... nimefika kibon'goto mara nyingi..... kwa nini wasiombe jengo hilo la upasuaji likatumika wakati wanasubiri kujenga la hosp ya wilaya? wanaoteseka ni wananchi na wapiga kura wa Mwanri..... think rationally.
   
 9. D

  DoubleOSeven JF-Expert Member

  #9
  Apr 28, 2011
  Joined: Jul 5, 2008
  Messages: 661
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  ... wee! wee! barabara ile kuu imejengwa na mkoloni. Maji ni mradi wa Germans through KfK, umeme mradi wa Japanese. hata barabara za Mibasheni ni mradi wa wananchi wa huko tangu zama za Babu wa Mangi Giddy!(Mmachame for that) Mashule na infrastructure zake ni miradi ya wananch hao kwani tangu zamani, hata wakati Aggrey akiwa dogo, wananchi hao walikuwa na utamaduni wa kujitegemea katika yote hayo ikiwa ni pamoja na michango na makato from income ya mauzo ya kahawa, licha ya zile walotafuna kina TANU na wezi wao waliokuwa KNCU. Mpaka leo dola 160,000,000 mali ya KNCU by 1982 hazijulikani ziko wapi???
  Nirejee kwenye mada: Ukiachilia kelele zake na usanii aliojaliwa, hamna cha ajabu ndani ya miaka kumi ya UBUNGE wa Mwanri. Wanywa gongo, wazururaji, na aina hiyo wameongezeka mno sambamba na umasikini unaokua kila leo. Sustainable development efforts ndio kitu nataka sikia. Tell me about that!
   
 10. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #10
  Apr 28, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Holy crap.
   
 11. M

  Marytina JF-Expert Member

  #11
  Apr 28, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,034
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Be blessed
  Naifaham sana SIHA ingawa sio home.Hamna initiative yeyote ya MWANRI as mbunge.
  Kwa sasa SIHA INADORORA tena kwa kasi ya ajabu uwezi amini ukiipimia SIHA ya 1995 na hii ya leo.
  Mwari aondoke manake kazi imemshinda at all.(Nitajie chochote kile alichokianzisha au kikoleza kwa wanaobisha)
   
 12. Mchaga

  Mchaga JF-Expert Member

  #12
  Apr 28, 2011
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 1,371
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Mkuu kabidhi huo ushahidi PCCB kama kweli unapenda maendeleo ya Jimbo la Siha. Binafsi nampongeza sana Mwanri ni mtendaji hodari.
   
 13. G

  Giddy Mangi JF-Expert Member

  #13
  Apr 28, 2011
  Joined: Feb 14, 2011
  Messages: 833
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Siha na wanasiha kazi kwenu.Mwenye tender zote wilayani humo ni watu watatu tuu ufisadi ni mwingi sana,ukiona umepata uongozi kwa kuhonga sigara,mbege na gongo basi jua unao waongoza wote ni waathirika ambao urithi wa familia zao umeziweka kwenye mikono yako.BARAKA GIDEON huyu ni mtu maarufu sana Siha.Siyo kwamba tuu ni mtoto wa Mangi Gideon laa bali ndie aliyekuwa Mwenyekiti wa kijiji cha Kashashi na kufanya mambo makubwa ambayo yaliwasaidia sana wana wa Kashashi kwani alikomesha kutokuwajibika kwa wana familia R.I.P Baraka G.
   
 14. s

  salisalum JF-Expert Member

  #14
  Apr 28, 2011
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 379
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Mjadala mgumu, haya endeleeni.
   
 15. G

  Giddy Mangi JF-Expert Member

  #15
  Apr 28, 2011
  Joined: Feb 14, 2011
  Messages: 833
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kuna kila sababu kuwa wazalendo na kama 2takubaliana siyo kila mtu anaweza kuwa kiongozi bora.Sasa kama sisi tutaamua kuwa wakweli,wapenda maendeleo nivema kama tutapenda Haki itendeke kwani mrejesho wa Haki ni maendeleo,amani na umoja katika jamii.lakini pia 2elewe nini tunataka kwanza ndio mambo mengine yaendelee.CCM na mpango kazi wake wa miaka 50 ya uhuru wameingiza siasa kila mahali hautatufikisha popote.MWANRI anayo kazi kubwa kwani hata Gamba bado ajavua.
   
 16. m

  mangalawa New Member

  #16
  Apr 28, 2011
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jaman tusilete ushabiki wa kisiasa usiokuwa na tija katika jimbo letu la siha nani asiyejua aliyo yafanya Mwanri tangu atupiwe mzigo na Makidara???????
  Ni msiha gani asiyefahamu ilivyokuwa shughuli pevu wasiha kujikomboa mikononi mwa wamachame??kama hujui kaulizie hilo tu linatupa pa kuanzia kwa wasiha wote kwa ujumla!!!!1
  Mtu anasema wanasiha wamemchagua mwanri kwa kuwanywesha gongo au mbege ndani ya siha kuna wasomi wazuri tu unataka kuniambia wote hawa wamedanganywa na gongo au mbege!!!1
   
 17. m

  mangalawa New Member

  #17
  Apr 28, 2011
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jaman tusilete ushabiki wa kisiasa usiokuwa na tija katika jimbo letu la siha nani asiyejua aliyo yafanya Mwanri tangu atupiwe mzigo na Makidara???????
  Ni msiha gani asiyefahamu ilivyokuwa shughuli pevu wasiha kujikomboa mikononi mwa wamachame??kama hujui kaulizie hilo tu linatupa pa kuanzia kwa wasiha wote kwa ujumla!!!!1
  Mtu anasema wanasiha wamemchagua mwanri kwa kuwanywesha gongo au mbege ndani ya siha kuna wasomi wazuri tu unataka kuniambia wote hawa wamedanganywa na gongo au mbege?
   
 18. m

  mangalawa New Member

  #18
  Apr 29, 2011
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wanasiha wote kufaae!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 19. Fasta fasta

  Fasta fasta JF-Expert Member

  #19
  Apr 29, 2011
  Joined: Feb 15, 2011
  Messages: 620
  Likes Received: 114
  Trophy Points: 60
  Huu mjadala nimeupenda sana na unaweza kutoa picha halisi ya sehemu husika.
   
 20. Liz Senior

  Liz Senior JF-Expert Member

  #20
  Apr 29, 2011
  Joined: Apr 19, 2007
  Messages: 485
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mangalawa, usomi hausababishi watu kupiga kura kwa kuzingatia uadilifu! Kama hawakuhongwa wao gongo wamesaidia kuhonga gongo. Ni wasomi wangapi wa Siha walikuwepo siha wakati wa kupiga kura? Wale wa mijini na hasa Dar walikuwa wanachangishana na kupeleka mafungu yaliyotumika huko wakapigia kura zao Dar. Angalia wale vijana pale Siha waliovyochoka! wamepauka kwa gongo! Siha imebaki na ukiwa!
   
Loading...