Elections 2010 Jimbo la Karagwe kwenda CHADEMA

Baija Bolobi

JF-Expert Member
Feb 25, 2009
1,093
1,726
Jimbo la Karagwe mkoani Kagera linaenda kiulaini mikononi mwa CHADEMA kutokana na NEC ya CCM kurudisha jina la BLANDES GOZIBERT. Viongozi wa CCM hapa Karagwe wanasema BLANDES hawezi kushinda na hata akishinda hawezi kuongoza akiwa gerezani. Wanatoa sababu zifuatazo:

-Amekuwa anakabiliwa na kesi ya rushwa tangu uchaguzi wa ndani ya chama, na tarehe 4/8/2010 hakimu alitamka kuwa ana kesi ya kujibu baada ya kuhitimisha mchakato wa awali.

-Tarehe 30/8/2010 Blandes alikamatwa na TAKUKURU tena na wapambe wake na kulala ndani kwa mahojiano. Hivi sasa wanakamilisha taratibu za kumfungulia kesi nyingine ya rushwa.

-Kamati ya siasa ya wilaya na Mkoa walitoa alama ya chini kwa jina lake kwa kuhofia kuwa likirudi atashindwa kirahisi.

Wakati huo huo, CHADEMA wamemsimamisha kijana DEUSDEDIT JOVIN kwa jimbo la Karagwe. Kijana huyu, miaka 38 anauzika vizuri kwa watu, ana ujasiri na uwezo mkubwa wa kuchambua masuala mbalimbali. Licha ya kubobea katika kufundisha IT lakini ni mwandishi mchambuzi katika magazeti ya Raia Mwema, Mwana Halisi na Tanzania Daima. Zamani aliandika sana katika Rai, lakini lilipouzwa kwa Rostam aliacha.

Habari ndiyo hiyo.
 
Good analysis; ila mzee angalia kama huyo kijana ana resources watu wa kutosha na how are the ccm guys serious; labda wanakudanganya
 
Hata jimbo la Mbulu linaweza kwenda chadema kwani Filip Marmo ametumia uwizi wa kura kushinda katika kura za maoni. wanaccm mbulu wameapizana kukipigia Chadema kura tarehe 31 OCTOBER mwaka huu.
 
good analysis; ila mzee angalia kama huyo kijana ana resources watu wa kutosha na how are the ccm guys serious; labda wanakudananya
=========

hata wakidanganya haiwasaidii maana blandes atakuwa kifungoni ndani ya mwezi mmoja kuanzia sasa. Kijana sijamwona zaidi ya kusoma makala zake mara kwa mara katika raia mwema.
 
Huyo hakimu ataamrishwa kumuona hana hatia. Nani kasema mahakama zetu ni huru? Ikiwa Appeals Court iliagizwa kutupilia mbali kesi ya mgombea binafsi, itakuwa hakimu huyu wa lower court?
 
Are you sure? au ni ushabiki tu? nahisi hata huko Karagwe hujawahi tia mguu, acha masihara mkuu
 
Huyo hakimu ataamrishwa kumuona hana hatia. Nani kasema mahakama zetu ni huru? Ikiwa Appeals Court iliagizwa kutupilia mbali kesi ya mgombea binafsi, itakuwa hakimu huyu wa lower court?
=====

Well, uko sahihi Zak Malang kwa sababu unaongea kutokana na uzoefu.

Argument yangu ya awali ilikuwa na mashiko kwenye contradictions za maamuzi ya NEC. Wanamwondoa Mwakalebela, lakini wanamwacha Blandes aliye mahakamani tayari, wanawaacha akina Mramba, Chenge, et al.
 
Hata jimbo la Mbulu linaweza kwenda chadema kwani Filip Marmo ametumia uwizi wa kura kushinda katika kura za maoni. wanaccm mbulu wameapizana kukipigia Chadema kura tarehe 31 OCTOBER mwaka huu.

Nilikuwa huko juzi, yule aliyeshindwa nasikia kapandishwa cheo wilayani hukohuko mbulu!
 
Could any honourable member update me on the election situation in NGARA

Wamempitisha yule Mnyarwanda Ntukamazina. Jimbo hilo likipata mgombea serious wa upinzani linakwenda kwao maana mgombea wa CCM pamoja na kuwa na uraia wa nchi mbili, ameisha choka na wala hakuwahi kufanya kitu chochote alipokuwa Katbu mkuu wa utumishi. yeye aliwasaidia Wanyarwanda wengi kuingia ktk utumishi wa umma na kuwasaidia RPF kwenye harakati zao za kukomboa Rwamda
 
Tegemeo pekee la wana sisiem ni chakachua mengine mbele kwa mbele lakini jimbo
watapigana walipate tu
 
CCM wao kwao ushindi si kushawishi bali kulazimishiaa..kwa sasa wameshika pabayaa...NGARA, KARAGWE kote CCM itaangukiaa puaa..
 
Wamempitisha yule Mnyarwanda Ntukamazina. Jimbo hilo likipata mgombea serious wa upinzani linakwenda kwao maana mgombea wa CCM pamoja na kuwa na uraia wa nchi mbili, ameisha choka na wala hakuwahi kufanya kitu chochote alipokuwa Katbu mkuu wa utumishi. yeye aliwasaidia Wanyarwanda wengi kuingia ktk utumishi wa umma na kuwasaidia RPF kwenye harakati zao za kukomboa Rwamda
Nasikia katika electons za huko ngara,somebody samuel ruhuza naye anagombania,huyu wasifu wake ni nini?
 
tatizo watu wa karagwe wananunulikwa kwa pesa ambazo ccm wanazo za kumwaga...je wanakaragwe wako tayari kukataa kununuliwa......itategemea mambo mengi...lakini naamini watz wanabadilika kila siku japo sio kwa kasi inayotakiwa yaani ya kutodanganyika....
 
Du! ama kweli. LAkini vema sana wakipata wapinzani kuongeza nguvu bungeni. Tunakoelekea ni nyomi sana, vishindo vya commedy vinakaribia ukingoni. Huyo Marmo akiondoka nitakunywa soda kwa furaha, maana majibu yake siku zote bungeni ni ya kibabbe pasi na logic, kachoka sana yaelekea. Amfuate kaka yake Malekela, nchi hii sasa inao wengi sana wenye uwezo kuiendesha, sio hati miliki ya mtu fulani.
 
Acha Bw. Baija, binafsi naona baada ya yule Kijana Mwarabu kushindwa katika mkakati wake Blandes atapenya kiurahisi kama ilivyokuwa 2005
 
Acha Bw. Baija, binafsi naona baada ya yule Kijana Mwarabu kushindwa katika mkakati wake Blandes atapenya kiurahisi kama ilivyokuwa 2005
=======

Omutwale
Hivi ninavyoongea nipo Kayanga bomani, na viongozi wa CCM wanasema hawataenda kwenye kampeini kwa sababu walimkataa Blandes lakini NEC imemrudisha. Kambi ya yule mwarabu, yote imehamia Chadema. Blandes ana tumaini moja tu, la kutumia fedha za Sir George ambaye anatafuta kumleta mtoto wake Joseph mwaka 2015.
 
Acha Bw. Baija, binafsi naona baada ya yule Kijana Mwarabu kushindwa katika mkakati wake Blandes atapenya kiurahisi kama ilivyokuwa 2005

Bahati mbaya C. Pesha ameamua kuachana na siasa ama sivyo safari hii Chadema wangechukua jimbo la Blandes kiulaini kabisa.
 
=======

Omutwale
Hivi ninavyoongea nipo Kayanga bomani, na viongozi wa CCM wanasema hawataenda kwenye kampeini kwa sababu walimkataa Blandes lakini NEC imemrudisha. Kambi ya yule mwarabu, yote imehamia Chadema. Blandes ana tumaini moja tu, la kutumia fedha za Sir George ambaye anatafuta kumleta mtoto wake Joseph mwaka 2015.

Acha ushabiki huu usio na data. Kwani Kahama ndie aliyempa Ubunge Blandes au wana Karagwe wenyewe ndo waliamua awe Mbunge? au upo kambi ya huyo Kijana uliyemsifia hapo juu Mkuu??.

Mambo mengine ni vizuri mkayaangalia kwa mapana yake na kuacha "bias". Hivi ni vipi Blandes anatumia fedha za Sir George ili kumpitisha Mwanae Joseph Kahama mwaka 2015??? Otherwise ni kutuambia kuwa huko Karagwe hakuna wapiga kura badala yake jimbo ni mali ya Kahama's family ambapo Blandes nae alipewa na Kahama kwa masharti ya kulirejesha mwaka 2015!!! (a joke!!).

...Do you mean kwamba Sir George Kahama nae anahusika kwenye tuhuma za rushwa ulizodai awali zinamhusu Blandes kwa maana ya kuwa anamsaidia Blandes kifedha???
 
Back
Top Bottom