Jimbo la Arusha Mjini linarudi CCM

Jimbo la Arusha Mjini linarudi CCM

lenga

Member
Joined
Apr 1, 2012
Posts
12
Reaction score
4
Kimtazamo wa kampeni ziendavyo hapa jijini, CHADEMA inaonekana kama chama tawala kilichoshindwa kuunganisha makundi mbalimbali ya kijamii na kuleta maendeleo, mbunge anaemaliza muda wake Mh. Lema ameshindwa kujipambanua na kueleza kwa yakini ni nini amewafanyia watu wa arusha mjini, hoja zinazotolewa na wapinzani wake juu kudorora kwa maendeleo na biashara arusha zinaelekezwa kwa msheshimiwa Lema.

Mgombea wa CCM maarufu MONABAN ameweza kuteka makundi ya kina mama na vijana na ahadi za uwezeshaji na utulivu wa mji zina mmbeba, mgombea mwengine mwenye nguvu wa tatu anatoka chama cha ACT, NA bila shaka atagawa kura za upinzani. nguvu pekee ya Lema inatokana na nguvu ya mgombea urais ndugu Edward Lowassa ambae atapita kwa siku moja tu jimboni. wadau tusishangae jimbo la arusha mjini likirudi mikononi mwa ccm.
 
lenga

Ni hivi jirani yangu aliibiwa simu siku ya jumapili, wakati anafanya shughuli zake aliingia ndani akaacha sim nje kwa kuwa ni sehemu ambayo haina wizi wizi hakuwa na shaka, kuja kutoka nje kakuta sim ishapitiwa, ikatafutwa haikupatikana, mama yule kada wa ccm akaondoka taratibu hadi kwa mganga siku hiyohiyo.

Yakafanyika yakufanyika mganga akamwambia rudi nyumbani ndani ya siku 7 utapata simu yako, mama yule akarudi kimya kama kaisahau simu yake, jambo la ajabu leo hii asubuhi mme wake anaamka kujiandaa kwenda kazini anakuta sim mlangoni, ndio kuita watu kwa furaha.

Sasa naomba mniunganishie dot,  kuna connection gani ilifanyika kati ya mganga na mwizi hadi simu ikarudi? Bado nina mshangao wa ajabu, mara zote naamini waganga ni waongo na hutumia mchezo wa kisaikolojia zaidi kumwahadaa mtu.
 
Last edited by a moderator:
Jimbo la Arusha linarudi CCM kupitia keyboard ya computer yako mkuu, lakini kwa sanduku la kura na vikatio tulivyonavyo hiyo ni ndoto, jimbo la Arusha ni Lema tu!!!!!!!!
 
Ni ndoto kama ndoto zingine tu. Sijui sababu kuu ya mtanzania anayejitambua kuishabikia ccm.
 
hapa mbezi mitaro ni michafu halafu watu wachafu wanachafuaa mitaro na mitaro haina shida Kychafuka sababu ni mitaro shida ni hao wachafua mitaro wanapo chafuka wenyewe kudhani wanachafua mitaro
 
Aksante sana kwa ndoto zako za mchana. Kura haziibiki jimbo la Arusha mjini. Hivyo, pamoja na vijidubwana vyenyu mlivyovifungulia ofisi ACT hao ndio watagawana kura na maccm si Chadema. Arusha bado ni ngome kuu ya Chadema na sio Arusha mjini tuu bali kila jimbo mkoa wa Arusha kipindi hiki ni Chadema tuuu. Muulize Ole Sendeka anavyotolewa kamasi na mpwa wake. Weye ota tuu. Si vibaya kuota lakini
 
Kumbe ndiyo maana Lenga hujapata likes hata moja, na mimi nakuambia kama utaendelea kupost utumbo wa kuku humu huta kaa uje upate likes hata moja.
 
wakikusikia , mitusi utaogelea humu; hawataki kusikia
 
me mbavu zangu zinauma sitaki kuendelea kucheka,, maana kila nikumuona aliyevaa nguo za kijani nacheka tuu,,

eti unasema arusha nani atapita,,,,!! Kwi,kwi,kwiiiiiiiiiii.....
 
Jimbo la Arusha linarudi likitokea Iraq au Kuwait???
 
arusha wapo busy na shughuli zao za kila siku na kampeni wamekataza chadema kufanya,tayari walishafanya maamuzi...ccm arusha watu wanawaangalia tu wanavyojipitisha,safari hii arusha tumekuwa wapole kwasababu dawa yao sisi tunayo
 
Back
Top Bottom