Jiji la Mwanza limekuwa kero sana sasa

Jiji la Mwanza limekuwa kero sana sasa

Azoge Ze Blind Baga

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2019
Posts
455
Reaction score
1,730
Hii elfu 20 ya vitambulisho vya wamachinga naona itakuja kuleta maafa na hizi akili za watanzania wengi

Leo hii katikati ya jiji la Mwanza hasa Maeneo ya kuanzia Sahara Hadi lilipokua soko kuu pamegeuka kero kwa wapita njia,magari binafsi na ya mizigo

Baada ya soko kuu la Mwanza Mjini kuvunjwa Maeneo ya Tanganyika na kutakiwa wafanyabiashara wote wahamie eneo tengefu la soko kule mbugani, wamachinga wengi wamegoma kwenda

Tangu tar 15 wanatakiwa watoke ile sehemu ya soko kuu ili kupisha ujenzi wa soko la kisasa wakagoma

Wameondolewa kinguvu basi wamama wote wamachinga wamehamia round about ya Nyerere road karibu na kituo Cha mafuta

Hii ni hatari mno kwa usalama wao, magari hayaendi kwa uhuru, wapita njia pia hatupiti kwa uhuru

Barabara zote za mjini Mwanza zimezungukwa na vibanda vya Machinga, hii ni mbaya kwa usalama wao hivi ikitokea gari imefeli breki so itaua wengi kama wale wamama wa Arusha walivyokufa walipokua wakiuza mboga mboga pembezoni mwa barabara

Mwanza imekua kero Sana hasa hapa katikati ya jiji kuanzia Sahara, maeneo ya soko kuu la zamani, Mohamed kuelekea Aga Khan

Halmashauri ya jiji ijitathimini yatakuja kutokea maafa halafu tutangaze msiba wa kitaifa kutokana na tamaa ya Rais wetu kutaka elfu 20 ya kitambulisho Cha Machinga na kuacha wafanye biashara hata Maeneo hatarishi .

Magufuli na serikali yako jichuguzeni kuhusu Uhuru wa Machinga mlio wapa.
 
Mkuu wa mkoa wa Mwanza anaitwa nani? Mkurugenzi anaitwa nani?

Kuna waakati nampa up Makonda. Ni mkuu wa mkoa pekee anayejaribu mambo mengi. Anakosea mengi lakini machache anayofanikiwa huleta raha Dar. Hapo Mwanza kuna shida ya uongozi. Hawafanyi lolote, chochote na hivyo hakuna lolote wala chochote kinachofanikiwa.
 
Kifurushi chako pendwa cha Saizi Yako kimerudi na Bonus. Nunua leo kifurushi Pendwa au kifurushi chochote upate Dk10 BURE Tigo-Tigo Saa24. Piga *147*00# kununua
 
Mkuu wa mkoa wa Mwanza anaitwa nani? Mkurugenzi anaitwa nani?

Kuna waakati nampa up Makonda. Ni mkuu wa mkoa pekee anayejaribu mambo mengi. Anakosea mengi lakini machache anayofanikiwa huleta raha Dar. Hapo Mwanza kuna shida ya uongozi. Hawafanyi lolote, chochote na hivyo hakuna lolote wala chochote kinachofanikiwa.
Mkuu wa mkoa anaitwa John Mongella,mkurugenzi wa jiji simjui ila alitaka kupigwa na Machinga kwenye tar 12-15 hivi baada ya kusimamia zoezi la kuondoa vibanda vyao Maeneo ya mbele ya shule ya pamba
 
Mkuu wa mkoa anaitwa John Mongella,mkurugenzi wa jiji simjui ila alitaka kupigwa na Machinga kwenye tar 12-15 hivi baada ya kusimamia zoezi la kuondoa vibanda vyao Maeneo ya mbele ya shule ya pamba
Huyo mkuu wa mkoa aliwahi kutajwa popote kwa mafanikio? Mongella! Mongella!
 
Hii kero ni kila mahali... Huku Arusha ni kero ntupu.. Kwanza wao ndio namba moja kwa uchafuzi wa mazingira... mitaa michafu kwa kuwa wamachinga wanatupa takataka hovyo... miataro inaziba.. Yani ni aibu na kero ya kutisha..

Mimi kwakweli sijui kwanini Rais wetu hajifunzi kwa swahiba yake Kagame.. Ukienda Kigali leo hii Ulaya wanafoleni mbali sana kwa usafi wa mazingira.. Yani barabarani hakuna machinga hata mmoja...

We Jiulize barabara ya Lugalo DSM kuanzia Tangi bovu darajani mpaka Mwenge ni Safi na mazingira ni masafi...Kwaini...?? ni kwasababu lile ni eneo la jeshi na machinga au raia haruhusiwi hata kusimama bila kazi....Wamachinga ndi wachafuzi number moja wa mzingira nchini....

Inashangaza wanatenga kiasi kikubwa cha pesa kwajili ya usafi lakini usafi wenyewe haunekani..Why...? kwasababu mchafuzi number moja wa mazingira ni Mmachinga...

Hii nchi inakera san
 
Miongoni mwa vitu vichache ambavyo Serikali awamu hii imepotea ni kuwaacha Machinga kutwaa barabara na Njia za waenda kwa Miguu na hivyo kuwa kero kuuubwa kwa waenda kwa Miguu na hatimaye ajali za kugongwa na Vyombo vya moto.
Uchafuzi wa Mazingira na hatimaye
Gharama kubwa ya Uhifadhi wa Mazingira.
 
  • Thanks
Reactions: Ilu
Kule buhongwa hali tete,mabasi yanapata tabu kupita hasa jioni. Wamachinga wamevamia hadi kingo za barabara
 
Hujakosea Mkuu mfano ukipita ile barabara ya kutoka chini ya mti kuingia stand
Jogoo house kushuka France Kona ,France kona kwenda Five star,na ile ya Mahakaman kwenda Kilombero jamani ni zaidi ya uchafu hapafai
Eti Jiji
Jiji gani halipendezi,halivutii kila mahali wamejazana na huwaambii kitu
 
siasa mbaya sana siku hizi kuanzia graduate hadi kazi za chini ni machinga barabarani na bado kuanzia leo graduate wengine wanaingia mtaani tena nakuhakikishia baada ya miaka kumi vijana wengi watakuwa wamechanganyikiwa na maisha si ajabu hii nchi itakuja kupitia mapinduzi makubwa sana ya siasa ambayo hayajawahi kutokea..

hizi certificate , diploma , degree na masters zinazoachiwa bila uelekeo ni bomu na litalipukaa tu..
 
Kabxaa mkuu naunga mkono hoja,yaan kwanz juz nmepafka nmepotea,hapaelewek kabxa,congestion ya watu plas magar imefanya mjii umekua finyu sanaa
 
H
Mkuu wa mkoa anaitwa John Mongella,mkurugenzi wa jiji simjui ila alitaka kupigwa na Machinga kwenye tar 12-15 hivi baada ya kusimamia zoezi la kuondoa vibanda vyao Maeneo ya mbele ya shule ya pamba
Huyu mkurugenz soon anakalia kuti kavu,kuna shule huk igoma katafuna hela badala ya kubomoa kuanzia chin kweny faundation kabomoa kidogo na kujengea tofali baada ya muda nyufa zikawa kubwa kwa hyo ikawa risk kwa watt,kaamua kuwalundika shule jiran nayo ina madarasa 6,juz tamisem wametuma watu kuja kufanya uchunguz soon ataliwa kichwa
 
Magufuli anaogopa kuwafukuza nachinga sababu hamna ajira ya kuwapa, inabidi watembeze tu bidhaa za mchina
 
Mhhhhh, wenzetu waliotangulia kielimu kama Kenya na Uganda mbona kawaida tu, nani alikudanganya kwamba kila anayesoma lazima aajiriwe
Pole sana.
siasa mbaya sana siku hizi kuanzia graduate hadi kazi za chini ni machinga barabarani na bado kuanzia leo graduate wengine wanaingia mtaani tena nakuhakikishia baada ya miaka kumi vijana wengi watakuwa wamechanganyikiwa na maisha si ajabu hii nchi itakuja kupitia mapinduzi makubwa sana ya siasa ambayo hayajawahi kutokea..

hizi certificate , diploma , degree na masters zinazoachiwa bila uelekeo ni bomu na litalipukaa tu..
 
Hakuna nchi yoyote duniani inayoweza kuwapa kazi wahitimu wote. Muwe mnatumia na akili kidogo mnapojibu hoja.
Magufuli anaogopa kuwafukuza nachinga sababu hamna ajira ya kuwapa, inabidi watembeze tu bidhaa za mchina
 
Inawezekana ulikua na point lakini ni kama umeandika kwa chuki, acha wamachinga nao wapumue awamu hii mmewatesa sana awamu zilizopita.
 
Back
Top Bottom