Jiji la Mwanza kuna kitu hakiko sawa

Jiji la Mwanza kuna kitu hakiko sawa

Habari Wana jamvi?

Naomba kutoa mawazo yangu kuwa Kuna jambo haliko sawa jijini Mwanza hususani swala la miundombinu. Jijini Mwanza hakuna miundombinu au barabara za kiwango cha jiji Kama ilivyo kwa majiji mengine. Barabara ndani ya jiji la Mwanza ni ndogo, na za zamani.

Ukiangalia barabara ya kutoka Usagara hadi mjini ni ndogo Kama njia moja tu. Barabara Ile husababisha foleni sana, barabara Ile inafaa njia nne. Pia barabara ya kutoka mjini kwenda Igoma/Kisesa nayo inafaa njia nne lkn ni njia mbili kama moja tu kutaja kwa uchache barabara za Mwanza.

Swali; ni kwa nini serikali na viongozi wa jiji hawaoni umhimu wa barabara hizo au barabara zilizopo Mwanza. Jiji la DSM, Arusha na Dodoma kuna barabara nyingi nzuri. Lakini siyo Mwanza. Kwa nini siyo Mwanza?

Cha ajabu, Bukoba ambayo ni Manispaa imepewa mradi wa barabara njia nne. Watu na magari yaliyopo Bukoba ni kidogo sana lkn wanapewa barabara hizo, Mwanza wananyimwa. Unadhani hilo ni sawa? Nina wasiwasi Kuna kitu hakiko sawa Mwanza kwenye miundombinu. Kwa nini Mwanza haizingatiwi, shida ni nini? Shida ni Serikali kuu? Shida ni madiwani na wabunge au shida iko wapi?
Wataletewa tren ya mwendo Kasi kama DSM,ila pia majitu ya Kanda ya ziwa Yanahama sana kwao hivyo legends wa kutetea home wako away watu wanaopenda kuhama kwao hua maendeleo yanakimbia mf Moshi,Mbeya na Tanga
 
Back
Top Bottom