Jiji la Mbeya na uozo katika Uongozi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jiji la Mbeya na uozo katika Uongozi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Lutala, Jul 9, 2012.

 1. Lutala

  Lutala JF-Expert Member

  #1
  Jul 9, 2012
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 845
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  [h=2]Sunday, July 8, 2012[/h][h=3]SAKATA LA WATUMISHI WASIO NA SIFA JIJI LA MBEYA KUPANDISHWA VYEO LASABABISHA MAKUBWA[/h]

  SAKATA la baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya kupandishwa vyeo pasipokuwa na sifa, limechukua sura mpya ambapo aliyekuwa afisa utumishi wa Jiji hilo aliyejulikana kwa jina la Koming'o ameondolewa katika nafasi hiyo.


  Taarifa za uhakika zilizoufikia mtandao wa kalulunga zimesema kuwa kuondolewa afisa huyo kwenye nafasi yake ni pamoja na kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili zikiwemo za kupokea rushwa kwa watumishi aliowapandisha vyeo.


  Kabla ya Afisa huyo kuondolewa kwenye nafasi hiyo, aliitwa na Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya Juma Idd pamoja na jopo lake ambapo alipopewa kusoma barua ya tuhuma zake aliishika barua hiyo kisha akaishiwa nguvu na kuanguka mbele ya Mkurugenzi huyo na kukimbizwa Hospitalini.


  Kwa mujibu wa habari za uchunguzi ambazo kikosi kazi cha mtandao wa kalulunga kimezinasa, mtumishi huyo akithibitika kuhusika na tuhuma hizo atafukuzwa kazi na kwa taarifa za jalada lake la kazi amebakiza mwaka mmoja kustaafu katika utumishi wake.


  Habari za kuanguka alipokuwa ameitwa ofisi ya Mkurugenzi wa Jiji hilo zimethibitishwa na Mkurugenzi Juma Idd alipohojiwa na mtandao huu ambapo alisema kuwa hakuwa tayari kuzungumzia tuhuma hizo kwa ujumla wake.

  Posted by PASTOR GORDON KALULUNGA at 10:11 PM 0 comments [​IMG]

  [TABLE="width: 100%"]
  [TR]
  [TD="class: reactions-label-cell, width: 1%"]Reactions: [/TD]
  [TD][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Jul 9, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Kama itadhibitika anachukua hela kwa watu ili kuwapandisha vyeo, basi hana maana, aende tu!
  Lakini, kwabahati mbaya au nzuri sheria yetu(ref.Mwal Nyerere) inasema mtoa na mpokea Rushwa wote ni washenzi, hivyo waliotoa nao waanze kutia maji, panga laja!
   
 3. Lutala

  Lutala JF-Expert Member

  #3
  Jul 9, 2012
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 845
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Yaani wote waliohusika wanatakiwa washughulikiwe kwa hasira ya kutosha. Haya mambo ni udhalilishaji wa uongozi kwa kiasi kikubwa sana
   
Loading...