Jiji la mbeya na changamoto zilizopo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jiji la mbeya na changamoto zilizopo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mbugi, Jan 7, 2011.

1. Mbugi

Mbugi JF-Expert Member

#1
Jan 7, 2011
Joined: Jan 7, 2011
Messages: 1,488
Likes Received: 100
Trophy Points: 160

JIJI LA MBEYA NA CHANGAMOTO ZILIZOPO

Katika hali ya kawaida na iliyopo miongoni mwa watu wengi na hususani waliopo nje ya mkoa wa Mbeya wanapopata fursa ya kujadili ama kusikia habari za jiji la mbeya huvutiwa sana na hata wengine wamesikika wakidai Mbeya ni zaidi ya Mwanza, na hata Arusha. Hali hii imekuwa ikichukuliwa kama mzaha fulani kwa wenye Mbeya yao, hasa ukizingatia rasilimali asili zilizopo, jiografia na hali ya hewa inayoruhusu mji kukua ikiwa ni pamoja na kujaliwa watu wachapa kazi kwa upande mmoja, jambo ambalo wanaamini Mbeya haipo katika hatua stahili kimaendeleo, na hivyo kuona haja ya kufanya mabadiliko katika nyanja mbalimbali ikiwepo ya kisiasa.

Dhana ya mabadiliko kisiasa inathibitishwa na historia ya mapokeo ya mageuzi katika miaka ya tisini ambapo wananchi waliweza kukipatia chama cha NCCR- Mageuzi zamana ya ubunge na hatimae tena CCM mwaka 2000-2010 na kwa mara nyingine tena Chadema. Naamini watanzania wenzangu kwa mwenendo huwo ni wazi wanambeya wanayo malengo yao wanayohitaji kuyafikia, na kwa lugha rahisi malengo hayo kutofikiwa kwa sehemu kubwa ndicho kimechukuliwa kama kipimo cha viongozi wetu wa kisiasa kuendelea au kuondolewa katika nafasi husika.

Malengo yanayotakiwa kufikiwa na sehemu kubwa ya wanambeya si ya ajabu zaidi ya kuona rasilimali zilizopo zinasimamiwa kwa maslahi ya taifa, kwani mara kadhaa imekuwa ikiwafadhaisha sana wanapopata habari ya matumizi mabovu ya pesa zao katika halmashauri ya jiji kiasi cha kupata hati chafu (Qualified report), Miradi mingi isiyoisha kwa wakati, usimamizi mbovu wa shughuli na raslimali za jiji, kama magari ya taka kusomba mchanga, mawe, na samadi wakati hali ya usafi wa jiji ukiwa tete, na wakati mwingine kupelekea hata uongozi wa mkoa kuingilia utekelezaji wa majukumu hayo. Wanambeya wamesikika mara kadhaa wakilaumu ufanisi na michango kiduchu utolewao na jiji katika kuchangia shughuli za maendeleo na badala yake kuwaachia mzigo mkubwa wananchi, na hata pale wanapojaliwa kutoa basi uwazi wa michango hiyo umekuwa wenye mlolongo mrefu na bila sababu. Miradi kadhaa imesemwa kuhusishwa na tatizo hilo ikiwemo miradi ya TASAF, DADÂ’s, ujenzi wa shule za sekondari, msingi, na hata utoaji wa ruzuku za kimaendeleo ndani ya kata, umekuwa ni tatizo kubwa hasa ukizingatia kuwa haufuati kanuni (formular) inayotaka ruzuku hiyo kutolewa kwa kufuata uwiano wa pato la ndani lililopatikana kwa kipindi cha gawio hilo.

Changamoto ni nyingi ikiwemo kukiukwa kwa makusudi kwa ushauri na maelekezo mbalimbali ya wataalamu wa ndani ya halmashauri yenyewe na hata nje ya halmashauri, mfano ni kubadili matumizi ya fedha za miradi unaoenda sambamba na kujengewa hoja zenye nguvu ya maslahi binafsi mfano badala ya kujenga (NEW BUILDING) wamekuwa wakiishia kukarabati hususani katika miradi ya AFYA, MAJI.

Maamuzi mengi kandamizi yasiyolenga madhara kwa upande wa pili na ambayo mara kadhaa yamekuwa yakitolewa kwa visingizio vya maelekezo ya juu, au chama ni alama kubwa ya uwezo mdogo wa uendeshaji wa halmashauri, migogoro iliyopelekea matabaka yasiyoisha kati ya watendaji wenyewe kwa wenyewe, na hata madiwani wenyewe kwa wenyewe kimekuwa ni kigezo kikubwa kwa wananchi waliowengi kuona Mbeya haiendi na badala yake raslimali zao zinatumika zaidi kutatua migogoro hiyo na si vinginevyo.

Loading...