Jiji la Dar na vitongoji vyake: Mikasa, vituko, vitimbwi na matukio

Jiji la Dar na vitongoji vyake: Mikasa, vituko, vitimbwi na matukio

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
359,882
Reaction score
828,449
Kuna usemi maarufu wa kilevi chenye kimea aina ya Safari laga. Maji rangi ya mende. Maji ya Ilala moja. Unasema SAFARI MOJA HUANZISHA NYINGINE. Sasa hapa ni tofauti hapa ni uzi mmoja huazisha mwingine.

Tulianza na uzi wa Mfahamu James Ngomero: Bingwa mtuhumiwa wa zile maiti 11 za watoto hospitali ya Mwananyamala uzi huu ukazaa Vituko vya Mwananyamala: Mtaa kwa mtaa (special thread) Tumeona jinsi wana JF wengi ni ama wakazi au walishawahi kuishi Mwananyamala. Uzi umekuwa ni burudani tosha kutokana na vituko na simulizi zake. Lakini Mwananyamala ni sehemu ya Dar na kuna mitaa mingine pia nje ya mwananyamala nayo ina vibweka vyake. Karibuni tutoke nje ya mwananyamala sasa.

Ubungo mpaka Mabibo
Tandale mpaka Magomeni
Manzese mpaka Mburahati, usisahau Kigogo
Kariakoo mpaka Ilala
Temeke, Davis corner, Kwa Aziz Ally kwa Kabuma moja, mtongani hadi Mbagala

Haya ni maeneo yaliyotengeneza headlines na kuna watu mpaka leo hii ukiwaambia umeishi mojawapo ya mitaa hii anakuangalia kwa jicho lingine, Kwa kifupi ni kwamba kuishi mojawapo ya mitaa hii ni darasa tosha sana.

Kuna maeneo mengi sijayataja kutokana na kuwa hayana impact kivile na kama kuna matukio basi yalitokana na huko kwingine.. Kuna Mikocheni, Masaki, Sinza, kijitonyama, Mwenge Chuo kikuu Kawe Bunju, Tegeta Tabata nknk

Tuanzie Ubungo mpaka Mabibo, Hapa ndio ilikuwa kama lango la jiji... Washamba wengi sana waliokotwa hapa.. Wa mikoani, wa kushangaa na kushangaza.. Mahouse girl wapya wa kupotea na kupotezwa, Dili za kupigwa bidhaa bandia marashi maji, simu kipande cha sabuni.. Kuuziwa gazeti la mwaka juzi.. Vidani bandia.. Madini bandia.

Hiyo ni Ubungo Mabibo kuanzia Maziwa. Ujambazi wa kutisha, madawa ya kulevya.. Wapigani na wapanga mipango ya wizi na utapeli.. Mabarmaid wengi wanaishi Mabibo na manzese...

Tandale Tandale Tandale, acha kabisa hii mitaa, wanasema akili kumkichwa.. Hata mtoto mdogo ni mpigani.. Tandale ndio mitaa pekee. Pengine na manzese ambapo kuna watu wanatoza fedha kwa kuuliza njia. Kuuliza kuna bei yake. Kupelekwa kuna bei yake
Magomeni kukiwa na kaustaarabu fulani lakini ni machimbo ya madon wa madawa ya kulevya.. Ishu za kuzamia ulaya Masea men.. Umalaya, ushoga nk.. Mnaikumbuka kwa macheni? Lango la jiji je? Kwa Bibi nyau usisahau Manzese mpaka Mburahati.

Dah mitaa hii, anzia mpakani Magomeni kagera.. Njoo Argentina, tiptop (lambo hotel), panda midizini, Mabibo makutano, Mburahati mpaka Kigogo.... Kwenye asili ya komando yosso, watoto wa mbwa, panyaroad nk.. Huku kunaongoza kwa gesti za bei poa na malaya mpaka wa jero.. Vibaka na wezi wengi wana asili ya huku.. Nani hajawahi kusikia manzese kwa mfuga mbwa?

Chawote bar Kigogo.. Ukitaka burudani za uswazi panda daladala ya Mabibo Kariakoo.. Huko ndio kuna kamusi za matusi na watu wamezikariri

Kariakoo mpaka Ilala... Kariakoo ni pakacha bovu... Achana na wandewa, wamanyema na wadosi.. Pale ni kiwanja cha wote... Kutoka huko kwingine kote.... Yani kariakoo ni sawa na choo cha jiji..

Ilala nyoronyoro sana kubweteka ubishoo na dili Safisafi... japo kuna vilinge vya ulozi pia.. Si haba kwenye hii kaliba... Kina sharifu wanaotibu kwa vitabu.. Vyuo vingi vya ujanja ujanja pia vipo mitaa hii na zile ofisi zetu zile.. Japo wamiliki wake si wenyeji wa Ilala.

Temeke moja hiyo... Hapa sasa usisahau Keko acha kabisa hili eneo, wizi uchawi umayala na mambo yote mabaya na machafu, njoo kurasini yote... Kwa aziz Ally wazee wa mchiriku, temeke Mwisho mpaka kwenye lile soko maarufu walikojaa wapemba Tandika.. Uwanja wa sifa mpaka kwa kabuma... Jongea mtongani mpaka mbagala... Acha kabisa hayo maeneo.

Tumalize na Vingunguti, banana mpaka Goms... Ukisikia JF inawika, inatamba, inashamiri na kukubalika sana mpaka watu wanafikia kudhani wana JF wote ni wakazi wa Dar tambua kwamba inaunndwa na vichwa mahiri kutoka hayo maeneo na mengine ambayo sikuweza kuyataja hapa.

KARIBUNI KWA VISA NA MIKASA TOKA PANDE ZOTE ZA DAR NA VITONGOJI VYAKE
 
Huu mji una changamoto nyingi
Kweli ila nyingi zinasababishwa na wachawi na mambo mengi hapo ni ya giza
Tuombee kwenye vikao wambie watuachie kidogo watu wa dar
Na kuna huyu mchawi mpya wa miaka 14 anachonga kwelikweli
 
Back
Top Bottom