Nguvu Muda na rasilimali wanazotumia kufukuza kukamata kuwashitaki na kuwafunga wamachinga zingetumika kwenye usafi huu mji ungekuwa afadhali. Ukienda mahakama ya jiji utakuta kosa la wapiga debe jela mwezi mmoja. Government hospitality at no cost at all, wakati kama wakamataji na waendesha mashitaka wangekuwa na akili wangewapa community services.
Mkuu, eyesores ziko kibao, just to mention a few, Pitia Railway Station aka Relwe jirani na geti ambalo mabasi ya relwe yalikuwa yanaingilia nia aibu, mwenge nako karibu na kituo cha mabasi, kawe opposite Tanganyika packers Hizi zote ni official dumpsites.
Halafu mameya wanatembea na mercedes metalic, kwenye barabara zenye kinyesi na mashimo sawa na mahandaki, huku wakifunga vioo vya magari ili wasisikie harufu ya takataka zilizojaa kila mahali mjini. Ambazo zimesababishwa na uzembe wao.