Jihadharini na aina hii ya utapeli (true story)

Jihadharini na aina hii ya utapeli (true story)

bigpack1982

Member
Joined
Apr 20, 2011
Posts
75
Reaction score
20
Hizi ni stori mbili tofauti ambazo zimewatokea watu wangu wa karibu.(Za Ukweli Kabisa)

Mwaka 2011
Rafiki yangu wa karibu akaenda kwa mganga mmoja maarufu hapa jijini Dar es Salaam,Mganga huyo sitamtaja jina lake hadharani lakini ni maarufu kwa kuchinja na kunywa damu ya Paka(hope wakazi wa Dar/Tz mtakuwa mnamfahamu).

Lengo kubwa la huyu rafiki lilikuwa ni kupata ufumbuzi/suluhisho ya matatizo yake ambayo alihisi Mganga huyo ndo mwisho wa Matatizo(sitaweka wazi matatizo yaliyomsibu).Kufika kwa Mganga huyo,jamaa kajielezea ,mganga kamsikiliza..akamwambia sasa ntakupeleka kwenye chumba ili ukaongee na ?Wazee? moja kwa moja..

Wakafika kwenye chumba,ambacho kimejaa makororo na vifaa mbalimbali vya kiganga..Mbele kuna sanamu (kinyago) cha mfano wa mtu mzee mwenye ndevu...mganga akakifunika kinyago kile kwa kitambaa cheupe..akaanza zungumza maneno kadha wa kadha.Sauti ikaanza tokea/sikika toka kwenye kile kinyago ambacho kilikuwa kimefunikwa.

Jamaa akajieleza shida zake ,sasa ikaja upande wa masharti/vifaa vinavyohitajika kwa ajili ya matibabu.

Hiyo sauti ya ?Wazee? ikataja vikorokoro kadhaa,mojawapo ikiwa ni Damu ya mnyama Ngamia.Kwamba zinahitajika chupa 4 za damu ya ngamia,tena siku hiyo hiyo kabla jua halijazama.Chupa moja Tsh 80,000/=,Chupa nne Tsh 320,000/=,Pamoja na vifaa vingine na hela ya kazi ya mganga,ikamtoka kama Tsh 600,000/=.Jamaa ilibidi wachukuane na mganga mpaka kwenye ATM ili wakatoke zile pesa.Akaambiwa baada ya siku mbili arejee kwa mganga.

Baada ya siku hizo jamaa akarejea ili kuleta mrejesho wa matibabu(kuna baadhi ya dawa alipewa atumie),maendeleao hayakuwepo kivileee..Mganga akasema tena waende kwenye kile chumba ili wakawape feedback ?wazee?.

Kufika chumbani,kama kawaida wakazungumza na wazee kwa style ile ile kama ya mara ya kwanza.Wazee wakamshukuru kwa zawadi ya Damu ya Ngamia na kumuahidi kuwa mambo yake yatakuwa mazuri sana..wakamwambia kuwa tena,wamechunguza sana kiundani na wamegundua kuwa aliachiwa urithi mkubwa sana wa Hazina (Pesa) toka kwa wazazi wake wa kale(Mzimu ya kwao),na pesa hizo ametunukiwa yeye ndo azipate,japo kuna ndugu kadha wa kadha wamekuwa wakihitaji pia..na kwamba ni utajiri mkubwa mno ambao atautumia yeye pamoja na vizazi vyake vingi tu.

Habari ya utajiri ikamfurahisha sana rafiki yangu..sasa wakampa masharti ya namna ya kuzipata hizo pesa..Kwanza ilikuwa ni kufika ?Mzimuni?,yani sehemu ambayo wale ?wazee? wanaishi ili waonane live na wampatie hizo pesa
Pili ilikuwa ni mahitaji ya vifaa mbalimbali kwa ajili ya shughuli hiyo pamoja na pesa za mganga..Jumla ukipiga hesabu ilifika kama 1.5M..

Sharti la tatu lilikuwa ni kutotoa siri yeyote ile ya huo mchakato mzima wa upatikanaji wa hizo pesa..iwe ni siri yake na abaki nayo kama yeye,asimwambie mtu yeyote yule,maana siri ile akiitoa,kwanza atapoteza zile pesa zote na kuwa maskini na la tatu atakufa!!

Jamaa kakubali,kaenda saka ile 1.5,kaiwasilisha kwa mganga,akaambiwa asubiri siku ya kwenda ?Mzimuni? kuoana na wazee live.
Siku ikawadia,akapigiwa simu kwamba aende Kigamboni jijini Dar,afike mida ya jioni hv kabla ya saa moja usiku ili wakutane na mganga waende wote.Mganga yeye alitoa sharti kuwa atakwenda mwenyewe kupitia mbagala kwakuwa sharti ya ile shughuli atakiwi kupanda Pantoni.

Safari ya kwenda mzimuni ikawadia..wakaenda umbali mefu kidogo toka pale Feri Kigamboni mpaka Mbele kidogo ya Kimbiji,wakaingia Porini..Walivyofika Porini kuna sehemu moja wakakuta kama kuna shimo hivi..wakaingia ndani ya lile shimo.

Lile shimo ukiingia ndani yake kuna pango kubwa sana..yani ni kama underground floor flan hv ambayo unatembea freely kabisa..Ndani ya hilo Pango humo shimoni,giza kali sana(walikuwa wanatumia mwanga wa Simu),kuna ndege wengii waliofanana na popo(kwa mujibu wa mganga wale ni majini wadogo).

Mganga akaita wazee wajitokeze..akatokea mtu ambaye alikuwa na umbo la kutisha kiasi,mwili wake umeenea manyoya kama ya ndege,uso wake ulikuwa hauonekani vizuri .Akawambia wazie mwanga wa ile simu.

Mazungumzo yakaendelea..waliongea mengi lakini kikubwa alimuonyesha sanduku lililokuwa limejaa Pesa,Pesa za Tanzania,Pesa za Kigeni..Jamaa yangu akawa very excited..akaambiwa achukue noti mbili za hela ya Tanzania(alichukua elfu kumi Mbili),jumla Tsh 20,000/= ili akazitumie ili apate udhibitisho kuwa ni noti za kweli na kwamba utajiri ule wote ni wake,yale mapesa yote ni yake..

Maelekezo yalikuwa baada ya kutumia ile Tsh 20,000/=,atoe mrejesho ili akapangiwe tena siku ya kwenda kuchukua utajiri wake.
Jamaa akaitumia ile Tsh 20,000/=,,akatoa mrejesho kwamba mambo yalienda vizuri kabisa.

Ila akapewa masharti kidogo,kwamba kwakuwa zile ni pesa za mizimu/majini,kwanza itahitajika kafara kwa ajili ya kuzilinda katika kipindi ambacho atakuwa anasubiria kwenda.Na ulinzi wake inahitajika Ng?ombe wane,wachinjwe kwenye pembe nne za Dunia,ili mali ile isipotee..

Kwa hesabu ya Dar es Salaam kipindi kile,Ng?ombe mmoja alikuwa ni Tsh 500,000/=,Wanne ikawa Tsh 2,000,000/=,jamaa akajipinda,huku na huku akakopa ili kufanikisha zoezi lile..akapeleka kwa mganga.

Akawa anasubiria siku ya kwenda kuchukua mzigo wake..siku ya siku akapigiwa simu na mganga,waende eneo lile lile..Wakafanya safari,wakafika

?Wazee? wakaitwa,kama kawaida mtu yule yule wa ajabu ajabu akatokea..akamwambia kuwa pesa iko tayari kukabidhiwa..lakini ina sharti moja la mwisho..kwakuwa zile ni pesa za mizimu/majini,lazima zichanganywe na pesa za hapa duniani,ambazo zimeshatumika ili aweze zitumia salama..bila hivyo hizo pesa zitamtesa sana..akaambiwa thamani halisi ya zile pesa za kwenye sanduku ni Billioni 20,hivyo inahitajika mafungu ishirini ya pesa za kuchanganyia..na Fungu moja ni Tsh 1M,Hivyo mafungu ishirini ni 20M..!!!!

Na kwamba hiyo inahitajika haraka sana..ili aweze zichukua zile pesa..ikumbukwe kuwa,huyu rafiki yangu tayari alikuwa na madeni kwa ajili ya kukamilisha baadhi ya masharti ya hapo awali,kupata 20M ikawa ni ndoto.Sasa afanyeje?akadiriki kuuza baadhi ya mali zake ilia pate pesa za ?kuchanganyia? ili akachukue mzigo wake.

Huku na huku,akauza baadhi ya mali zake,20M ikapatikana..akapeleka kwa mganga ili utaratibu wa kuchanganya ufanyike..akaambiwa asubiri kupigiwa simu ili akachukue mzigo wake.

Ikapita siku,miezi..kimyaaa..mganga kauchuna..akipigiwa simu anasema mchakato bado..full kuzungushana..hatimaye jamaa akakata tamaa..moyoni akawa na woga ule aliotishiwa kuwa akizungumza lile jambo,anaweza kupoteza uhai..hivyo ikawa ngumu kwenda polisi wala kushtaki sehemu yeyote ile..ndo akawa kaliwa hivyo..ila miaka kadhaa kupita..ndo akanielezea kisa chake..

Sasa Mwaka 2015;

Kuna stori kama hii hii,wiki kadhaa zilizopita imemtokea mtu mwingine wa karibu,yeye nae alipitia mchakato kama huo huo,ila sio kwa mganga yule yule,this time mganga alikuwa ni tofauti,alikuwa ni wa Zanzibar,na walikuwa wanaenda mapangoni eneo moja kule Zanzibar inaitwa MATEMA,utofauti wa awamu hii ni kuwa kwenye mapango(mazingira alivyoelezea yanafanana sana na yale ya Dar)isipokuwa wao kwenye mapango walikuwa wanasikia sauti tu..hawakuona sura ya mtu yeyote..nae kaliwa pesa nyingi sana..mamilioni ya pesa,kaachwa solemba,japo ana mpango wa kuifuatilia pesa yake aliyolizwa,lakini ushahidi wa issue kama hizi inakuwa ngumu sana,kwa hiyo kwenda mahakamani au polisi mtu anaweza kata tamaa sababu ya ushahidi kutokidhi vigezo.

Nikasema ndugu zangu kuwa,ni share nanyi aina hii ya utapeli ambao waganga maarufu hapa Tanzania wanaufanya,msikubali kujiingiza katika mtego huo,na kama kuna mtu yuko kwenye process hizo,basi aache mara moja maana atafilisika.

Kwenye hili kuna Maswali ambayo nilijiulizam nikakosa Majibu:

-Hayo Mapango hao waganga wameyagunduaje?Maana inaonekana Tanzania yatakuwa Mengi katika maeneo mbali mbali

-Hv ni mbinu gani wanayotumia ili kusikia sauti za hao wazee Mapangoni?au Wazee kujitokeza kabisa wakiwa katika maumbo ya kutisha?je ni kweli ni Majini hayo ambayo pengine yanashirikiana na waganga kutapeli wanadamu?

-Wanatumia utaalam gani kuweza kutengeneza/kuonyesha kiasi kikubwa cha pesa kwenye hayo masanduku?

Ahsanteni
 
Daah H Mada Ina Meng Ya Kujifunza Asante Mkuu
 
Jamani tusipende vya bure. Hizo pesa zote ni zaidi ya mtaji
au yeye alikuwa ana taka mambo yaende vizuri namna gani?Maana kupata tu hiyo mil 20 ni mambo safi kwa kiasi fulani..

Hapo sasa shangaa na wewe

Ila kuna binadamu wanaabudu sana ushirikina, ndio maana ni rahisi sana kwa kutapeliwa
 
Huyo mganga wa kwanza nilikua ni mimi, ila now days nimeokoka.
 
Wanaonyeshwa hela za bandia wanachanganya na hela za kawaida!! Huyu jamaaa ni tapeli kuna mshkaji mmoja alikuwa anamchana live watu kama hawa dawa yao ni kwenda kuwa chukulia dawa hapo Zaire unawapiga chini wote
 
sio matema bali ni matemwe, kuna jamaa anakaa ndani ya pango na anaitwa bogaboga, uyo jamaa ana uwezo wa kubadilisha kila sauti, hawa jamaa ni wezi sana hawana uwezo wowote wa kiganga
 
sio matema bali ni matemwe, kuna jamaa anakaa ndani ya pango na anaitwa bogaboga, uyo jamaa ana uwezo wa kubadilisha kila sauti, hawa jamaa ni wezi sana hawana uwezo wowote wa kiganga

Duuh..basi huyo jamaa ni hatari mkuu,tujuze kiundani..
 
Tawire Tawire kijana leta utumbo wa sisimizi! Waganga wanajua cheza na psychology sana!
 
Jamani tusipende vya bure. Hizo pesa zote ni zaidi ya mtaji
au yeye alikuwa ana taka mambo yaende vizuri namna gani?Maana kupata tu hiyo mil 20 ni mambo safi kwa kiasi fulani..

Alitaka mtaji mkubwa kiasi baada ya miezi mitatu, Mengi na Bakhresa wawe nyuma yake
 
Back
Top Bottom