Jihadhari na Utapeli wa Photo Point ya Mlimani City | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jihadhari na Utapeli wa Photo Point ya Mlimani City

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Idimi, Jul 28, 2010.

  1. Idimi

    Idimi JF-Expert Member

    #1
    Jul 28, 2010
    Joined: Mar 18, 2007
    Messages: 10,222
    Likes Received: 2,086
    Trophy Points: 280
    Ndugu wana JF,
    Sio lengo langu kuvurga biashara ya upigaji na usafishaji picha wa hawa ndugu wa Photo Point ya pale Mlimani City. Lengo tu ni kuwatahadharisha ndugu mnaoenda kupiga picha za matukio mbalimbali pale mahali (kama za Sendoff, Ubarikio, Harusi, birthdays na graduation). Kimsingi huduma hizi zinalipiwa bei kubwa na huambatana na ahadi za zawadi kemkem kama vile kuchapishiwa picha zako katika foronya, mito, vikombe, bakuli, sahani, fulana n.k.
    Mnamo tarehe 10 ya mwezi Julai nilienda kupiga picha pale ofisini kwao Mlimani City. Gharama ya picha zile ilikuwa shilini 96,000, ikiwa ni kupiga na kusafisha picha 20 za ukubwa wa 5'x7' na moja ya ukubwa wa 12'x16' ambazo zingewekwa katika albamu pamoja na kuchapishiwa sahani moja yenye picha ya tukio.
    Mpaka ninavyoongea hivi sasa albamu wanasema hawana, sahani na vikombe hawana, zimeisha, ilhali vimeshalipiwa katika package zao tulizolipia. Nikiwa katika harakati za kufuatilia picha zangu jana nikakutana na kundi la wateja wengine wenye malalamiko kama yangu wakidai kurejeshewa sehemu ya fedha zao walizolipia huduma.
    Mpaka sasa sijajua mustakabali wa albamu na vitu vingine, kwa hiyo ndugu zangu mnaoenda kupiga picha pale Photo Point Mlimani City muwe makini na utapeli huu.
     
  2. Fixed Point

    Fixed Point JF Bronze Member

    #2
    Jul 28, 2010
    Joined: Sep 30, 2009
    Messages: 11,321
    Likes Received: 89
    Trophy Points: 145
    Asante kwa taarifa
     
  3. mfianchi

    mfianchi JF-Expert Member

    #3
    Jul 28, 2010
    Joined: Jul 1, 2009
    Messages: 7,947
    Likes Received: 1,507
    Trophy Points: 280
    Mliandikishiana au ndio mali kauli,kama mliandikishiana au kama kuna sehemu pameandikwa ukipiga picha kadhaa wa kadhaa utapata vitu fulani basi mnahaki ya kudai hivyo vitu mlivyoahidiwa lakini kama hakuna kitu kama hicho basi hiyo imekula kwenu,na hapo ndio ujue biashara za washwahili zinavyoendeshwa kiswahili
     
  4. Bazazi

    Bazazi JF-Expert Member

    #4
    Jul 28, 2010
    Joined: Aug 18, 2008
    Messages: 2,029
    Likes Received: 560
    Trophy Points: 280
    Taarifa nzuri sana
     
  5. M

    Mundu JF-Expert Member

    #5
    Jul 28, 2010
    Joined: Sep 26, 2008
    Messages: 2,719
    Likes Received: 28
    Trophy Points: 145
    Msiogope haijakula kwenu...nahisi jamaa wameishiwa stock tu! Fuatilieni na mtapata haki zenu. Tatizo jamaa walikuwa na uchu wa kukusanya fedhwa bila kuhakikisha kama huduma na bidhaa zao zinaendana na boom hiyo. Polen wandugu.

    Kwa upande mwingine, Photo point ya Mlimani City ni moja kati ya sehemu wanapopiga picha za passport size kwa bei nafuu kuliko sehemu nyingine yeyote Dar. Picha nane za kiwango kizuri unapata kwa buku tatu tu. Bravo them!!
     
  6. ngoshwe

    ngoshwe JF-Expert Member

    #6
    Jul 28, 2010
    Joined: Mar 31, 2009
    Messages: 4,075
    Likes Received: 33
    Trophy Points: 145
    Hivi Tz hakuna wataalamu zaidi ya hao jamaa?. Zamani zile kupiga picha ilikuwa kama unakaa mkoani ni mpaka usubiri miezi mitatu au minne kupata picha zako. Leo hii kwa teknolojia ilivyo, unapost pics zako kwa wasafishaji, unachagua huduma uitakayo..na muda mfupi unapata kila kitu...ukiritimba huu wa kuwa wafanyabiashara ndio unaoleta shida..poleni sana.
     
  7. b

    bitimkongwe JF-Expert Member

    #7
    Jul 28, 2010
    Joined: Oct 21, 2009
    Messages: 3,034
    Likes Received: 211
    Trophy Points: 160
    Labda kama mashine yao imeharibika, lakini sahani nyingi zisokuwa na mauwa zinakubali picha ikiwa unavyo vifaa muafaka.
     
  8. FairPlayer

    FairPlayer JF-Expert Member

    #8
    Jul 29, 2010
    Joined: Feb 27, 2006
    Messages: 4,166
    Likes Received: 64
    Trophy Points: 145
    Ndugu Idimi,

    Nadhani umetoa changamoto. Ila neno UTAPELI umeitumia visivyo. Tapeli ni yule anayekuzungusha bila SABABAU ya kueleweka. Makampuni makubwa tu mfano SIGARA kuna wakati Sigara ya Embassy ilikua haipo mtaani sembuse hao wajisiriamali wa Kizalendo???

    Wa Tanzania tumezoea mpaka tuone WAGENI wana wekeza ndo tuone SAFI ila akiwekeza MZALENDO basi tatizo DOGO tu utaambiwa TAPELI, ANANYANYASA WAFANYAKAZI, HALIPI KODI n.k.

    Wakati nakubaliana na wewe kuhusu kuishiwa na vifaaa (LABDA) na kutokupa taarifa mapema nadhani umefanya vizuri kuweka wazi ila KICHWA cha habari/taarifa ingekuwa kingine na sio UTAPELI.

    Ila safi sana, wewe ni mteja mzuri..

    Wako FP
     
  9. Sinkala

    Sinkala JF-Expert Member

    #9
    Jul 29, 2010
    Joined: Dec 22, 2008
    Messages: 1,505
    Likes Received: 32
    Trophy Points: 145
    Kuna uzembe pale. Mimi sikuchagua kuwekewa "border" kwenye picha zangu, lakini jamaa wakaniwekea. By default, picha inatakiwa isiwe na border unless umecheck alama ya vema ( √ ) kwenye sehemu ya border katika bahasha zao. Siku nyingine nililipia kusafisha picha kwa size ya 4x6 na ikaandikwa katika bahasha, nikatoka kidogo, niliporudi nikakuta zimesafishiwa kwa size ya 3x5, halafu eti wakasema tunaomba tugawane hasara!
     
  10. B

    BARRY JF-Expert Member

    #10
    Jul 29, 2010
    Joined: Oct 21, 2009
    Messages: 364
    Likes Received: 115
    Trophy Points: 60
    na wewe una roho nyepesi kama kamasi, mlikubaliana biashara/service..........huenda jamaa kaharibikiwa mitambo au vifaa vimeisha......subiri daaaaaaaah
     
  11. Masikini_Jeuri

    Masikini_Jeuri JF-Expert Member

    #11
    Jul 29, 2010
    Joined: Jan 19, 2010
    Messages: 6,809
    Likes Received: 364
    Trophy Points: 180
    Yeah give them the benefit of the doubt! Mie ni mteja wa hiyo kampuni since wakiwa nachumba kimoja kule Mayfair; nyingi ya kumbukumbu za matukio ya maisha yangu Photo point wamenisidia kuyaweka ikiwa hata la ujio wa Junior! Issues zipo na si kitu cha kudumu.
    Ila pia ni angalizo zuri kwa Photo point msituudhi wateja wenu kama hivi...............mwombeni radhi huyu jamaa!
     
  12. Mtazamaji

    Mtazamaji JF-Expert Member

    #12
    Jul 29, 2010
    Joined: Feb 29, 2008
    Messages: 5,972
    Likes Received: 33
    Trophy Points: 0
    haahhaaahaaha eti Vikombe saani vimeisha. Kumbe kuna vikombe na sahani spesho kwa ajili ya kazi kama hii. Nilidhaniunaweza kuweka picha kwenye kikombe au sahani yeyote.

    Inawezekana kuna baadhi ya vifaa vyao vimeharibika na hawasemi ukweli wa tatizo halisi linalowakabili.
     
  13. Mshirazi

    Mshirazi JF-Expert Member

    #13
    Jul 29, 2010
    Joined: Dec 8, 2009
    Messages: 444
    Likes Received: 11
    Trophy Points: 0
    Ambrozi hakua na usumbufu namna hii...
    Mnamkumbuka??!!
     
  14. cocochanel

    cocochanel JF-Expert Member

    #14
    Jul 29, 2010
    Joined: Oct 6, 2007
    Messages: 18,454
    Likes Received: 59,403
    Trophy Points: 280
    Neema Apson vipi tena photo point yako inachemka? labda wafanyakazi wako wanakuchezea hapo kukuharibia biashara.
    Jamani kuna ingine ya Mayfair, Mikocheni mie niliwafurahia huduma zao ila ni picha tu na kusikilizwa kupata nilichotakaga
     
  15. afkombo

    afkombo Member

    #15
    Jul 30, 2010
    Joined: Feb 9, 2008
    Messages: 93
    Likes Received: 3
    Trophy Points: 15
    Pole sana ndugu lakini Jaribu kuuliza vizuri huenda wakakupa sababu maalum za ucheleweshwaji huo.Mimi sijawahi kuwatumia hao jamaa lakini nahadithiwa na watu kuwa Jamaa kazi zao ni nzuri so usikimbilie kuwaita matapeli tu huenda wana sababu iliyo nje ya uwezo wao Ingawaje Watanzania nao sometimes hawako wazi inawezekana wameishiwa bidhaa kwenye stock lakini haweki vitu wazi na badala yake wanakupa tarehe tu bila kukwambia nini hasa kinaendelea.
     
  16. Kiranja Mkuu

    Kiranja Mkuu JF-Expert Member

    #16
    Jul 30, 2010
    Joined: Feb 18, 2010
    Messages: 2,100
    Likes Received: 16
    Trophy Points: 0
    Bongo dalesalama ndio hii.
    Hadi mnara wa askari unauzwa.
     
  17. M

    Majala Kimolo JF-Expert Member

    #17
    Jul 30, 2010
    Joined: Aug 3, 2007
    Messages: 344
    Likes Received: 3
    Trophy Points: 35
    Hobi nyingine bana
    Hivi mpaka leo mnapiga picha ili iweje. Nafuatilia matumizi ya picha hizo naona ni kupoteza kabisa pesa. Sawa! hata kuvuta sigara ndo ivo ivo
    Ila poleni, mngeanza hayo mambo zamani msingefanya leo
     
  18. Pdidy

    Pdidy JF-Expert Member

    #18
    Jul 30, 2010
    Joined: Nov 22, 2007
    Messages: 33,466
    Likes Received: 5,708
    Trophy Points: 280
    ndugu nikusaidiesasa wahuni kama hao nenda nunua kitu angalia wameshachukua machine ya tra....fn..kama sio anzia nao huko huku ukidai madai yako...unajua nasikitika akuna kesi ya nyani kama ya madai nchii hii..ukiwapeleka mahakamani wanaishia kusema awana na watakulipa lini wanataja muda wanaotaka...hiyo ndio upupu wa nchi yetu else wapelekee comedy hao simple wakitoka kwenye tv walahi na kwambia wanakupigia wenyewepole mpwa
     
  19. Pdidy

    Pdidy JF-Expert Member

    #19
    Jul 30, 2010
    Joined: Nov 22, 2007
    Messages: 33,466
    Likes Received: 5,708
    Trophy Points: 280
    Endelea kumpa pole mama yetu mwambie ndio mwanzo wa ndoa hiyo ndoa si kufurahi tu hata majaribu ni moja na nafasi za ndoa ..polen wapendwa
     
  20. Pdidy

    Pdidy JF-Expert Member

    #20
    Jul 30, 2010
    Joined: Nov 22, 2007
    Messages: 33,466
    Likes Received: 5,708
    Trophy Points: 280
    mmmhhh apson wale wale ama???
     
Loading...