kuna akina dada walimliza mwenye duka la boutique 682,000/-
walifika dukani kwa kujiamini mashamsham kibaao.. Wakaanza kujaribu na kisha wakaomba wafungiwe mzigo wao,maana walikuwa wanawahi airport..
Walichukua handbags,viatu pea kadhaa,na makorokoro mengine.. Baadaye wakamuuliza mwenye duka kama kajiunga na tiGO pesa,mwenye duka akasema hajajiunga,akamuuliza mfanyakazi wake,akasema kajiunga.
Wale wadada wakaomba namba walipe pesa.. Huku wanapiga stori nyingi,na kusema wamepata duka lina collection kubwa,hawatashop maduka mengine..
Mmojawao akamuuliza yule dada wa kazi kama hela imeingia,akajibu haijaingia bado..Basi akamwambia yule dada wa kazi pale dukani ampe simu yake kisha akaichezea kama dakika mbili,kisha akasema ujumbe si huo hapo hela imeingia tayari... Wale wakasoma ujumbe,na wakaagana..
Baada ya muda kidogo waliamua kuangalia salio na kukuta hamna kitu! Wakaja kugundua kuwa wameibiwa! Je mwajua waliibiwaje? Ni kwamba mwizi yule alisave namba yake kwenye simu ya yule dada wa kazi pale dukani kwa jina la TIGO PESA. Kisha akatuma ujumbe kama unavyoandikwa na wenyewe wenye huduma kuwa UMEPOKEA Sh....
Mpo hapo?