mwanaMtata
JF-Expert Member
- Oct 18, 2014
- 2,393
- 1,433
Habari ya wakati na muda kama huu ndugu zangu watanzania na East Afrika kwa ujumla. Nianze kwa kutoa pole kwa ndugu jamaa na rafiki wote walioko kwenye mfungo. Mwenyezi awajalie wepesi.
Dhumuni la kuanzisha thread hii ni kuwafungua tu macho watu hasa wale wanaopenda biashara ya mtandao. Kuna mitandao mingi sana ila leo naomba tuongee hii site ambayo ni kama "advertising center" www.kupatana.com
Kwa mimi kupatana ndio kama kariakoo yangu na nina uzoefu sana na pia ninmara chache sana inatokea nafanyiwa dhuluma na hii ni pale mtu anaamua kukuuzia kitu kwa ujanja ujanja ila pia mwisho wa siku ukitumia mbinu mbadala anapatikana.
Kuna siku niliingia kupatana nikakutana na tangazo hili
Nilipoona tangazo ninla bei rahisi na namba iko ya nchini kwetu kwanza nikapiga, haikuwa hewani ndipo nikamchatisha whats app
Mazungumzo yalikua hivi
Akaniambia yuko kenya na kujitetea kwingi. Sasa uzuri mimi kenya ni kama nyumbani. Nina marafiki kibao na ndugu pia nikaona sio kesi nikaunda Group kati yangu mimi, yeye na Derick rafiki yangu aloko kenya
Jamaa akawa analefu tuu kila saa ikabidi nimfate inbox nimtulize wenge kwa kumuelewesha
Hatimaye akakubali kua kwenye group nikamrudisha tena na mazungumzo yakaendelea kama ifuatavyo
Nilivoona anataka biashara za yule jamaa mwingine anaesemaga yuko mtwara nikamuuliza jina la kampuni labda ingenipa muongozo
Baada ya kutaja jina la kampuni niliingia Google na kuangalia cha kwanza nikakuta kampuni iko india. Sikutilia maanani kwani majina tu yanaweza kufanana ila nikafanya more digging sijakuta kampuni yenye jina hilo kenya
Baada ya kukosa kampuni hio ilinipasa kuomba blog au website pengine hapo ningepata mwanga. Aliposema pia hata hivo hana nikajua hawa ndo walewale wanasubiri watu watafute pesa kwa jasho wao waje wale kirahisi.
Ombi na pendekezo langu si kwa wamiliki wa kupatana tuu, bali humu jamii forum (matangazo madogo madogo) na hata kina OLX muwe na acccess ya kumwezesha mtumiaji wa hii service yenu kulalamika pale anapofanyiwa fraud, mkiridhika na utafiti kwamba kweli mlengwa au mtajwa ametapeli basi muwezeshe kutiwa nguvuni kwa jangiri hilo.
Najua mnaogopa kupoteza viewers kwa ajili ya CPM na mambo kama hayo, ila ukiangalia kwa undani watu wengi watakua wanatumia mtandao wako kwani wana uhakika walau asilimia 60% kwamba hata wakipigwa (kutapeliwa) kuna msaada.
NI HAYO TUU WAKUU KARIBUNI KWA KUCHANGIA