Jihadharani na hii NGO John Snow Inc ya kitapeli iko Masaki

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
56,668
30,554
Ndugu wapendwa,

Naomba niwajulishe hasa wale ndugu zangu wa social work

Ni mmoja wa wahanga wa hii NGO natokea mkoani na nimekuwa nikifanya kazi za kufundisha baadhi ya mikoa. Nimefanya na kampuni mbali mbali ikiwemo USAID.

Hivi karibuni hawa mabwana walipata hela ambazo zinatoka USAID washirikiane na chuo kimoja kufundisha watu mambo kadhaa ya jamii ikiwemo kujilinda na HIV.

Baada ya kufanya kazi wamekuwa wakilipa watu nusu na sasa majuzi wamewapeleka watu Morogoro wakawadanganya wakirudi tu wanapewa pesa zao.

Ajabu kubwa mpaka sasa hawajalipa na walipofwatwa mwanzoni walitaka kukana kulipa na baadae walipooneshwa barua za kuitwa wahusika na hiko chuo kufundisha huku wao wakiwa wadhamini wakadai tutawalipa ooh now hakuna hela.

Kwa yoyote atakehusika na hii NGO muwe makini sana ni wagumu kulipa watu hasa baada ya kumaliza kazi zao.

Kwa bahati nzuri tumeandika barua kwa wizara na wale wote wanaohusika wakiweko USAID kufwatilia malipo yetu.

Pamoja na hayo tunapeleka barua kwa waziri anaehuska na hizi NGOs wajue jinsi wanavyocheza na maisha ya watu.

Mnaombwa muwe makini sana hasa unaposikia kuna kazi za kufundisha na wao wakiwa kama sponsors.
 
Ila mkuu mwandiko wako,jitahidi urekebishe,..
Nowadays jamaa anatumia simu nzuri, ile ya kitambo ndio "batani" zilikuwa zinasumbua na kufanya mwandiko kuwa mbaya.
Members wengi watakubaliana na mimi.
 
Pdidy barua mliyopewa haikuzungumzia mtalipwaje? Na barua ya mwaliko, ilitoka wizara ya afya au hiyo NGO?
 
NGO nyingi zina mambo ya kijinga kama hayo ya malipo..
Pia kwenye mambo ya UKIMWI zimekuwa zikipika takwimu ilizionekane zinapiga kazi..
 
Johns Snow ilikuwa mwanzoni sasa wanaganga njaa tuu. Hivyo hivyo PSI naona toka utawala wa ndg D J Trump
Misaada kwenye hizi Ngo imepunguwa na pia wapo maseneta wapigaji na maproffessor wanaoziongoza hiz ngo huko ughaibuni
 
John snow inc walinifundisha IPC (infection prevention and control) sijui kama wamekuwa matapeli kiasi hicho?!
 
Hawa jamaa kuna service fulani hivi kampuni yetu tunawapatia. But hawajawahi kutusumbua kwenye malipo. Kwa upande wangu sijaona huo utapeli. Inawezekana labda utapeli wanafanya kwa upande mwingine
 
Hawa jamaa kuna service fulani hivi kampuni yetu tunawapatia. But hawajawahi kutusumbua kwenye malipo. Kwa upande wangu sijaona huo utapeli. Inawezekana labda utapeli wanafanya kwa upande mwingine
VESTA
Hata sisi tunaimini na tuliiamini hivyo na ndio wengine wakakubali kutumika..ila ya malipo kwakuwa yanapitia hiko chuo tulipofwatillia sana tulaonyshwa email toka kwa JSI..Kwenda hiko chuo wakidai kwa sasa hawana hela tuendelee kusybiri...Usaid haifanyi kazi kwa style hii..na kwakuwa barua za mwaliko zinatoka chuoni..na email tulioonyeshwa toka chuoni basi tunaa amini Jsi watafwatilia hili wajue shida ikowapi....ila mpaka sasa watu wanadai hela nyingi na wanapugwa tar kama watoto....tumewapa june hiko chuo waje na pesa zetu else tunalufumua mema mwanzo wa july
 
Back
Top Bottom